Siku 119 za Watanzania mikononi mwa maharamia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku 119 za Watanzania mikononi mwa maharamia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, Mar 5, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  WATANZANIA 14 waliotekwa na maharamia wa Kisomalia katika meli ya MV Aly Zoufecar, Novemba Mosi mwaka jana, wameokolewa wakiwa hai nchini Madagascar.

  Watanzania hao ni miongoni mwa watu 28 waliookolewa na Jeshi la Wanamaji la Madagascar kutoka mikononi mwa maharamia hao baada ya kuishi melini wakiwa mateka kwa siku 221.

  Gazeti la Mwananchi.

  Vilevile leo ni siku ya 119 tangu watanzania karibu wote tutekwe na maharamia ya NEC tutaishi kwenye meli ya CCM hadi lini? je tutaokolewa lini?
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280


  Hahaaaaa, nimeipenda, nadhani na sisi tusubiri hadi zifike 221 pengine jeshi la wana maji la CDM litakuja kutuokoa na maharamia hawa ambao ni waongo, wazushi na wazandiki....

   
 3. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,206
  Trophy Points: 280
  Hadi siku hiyo tutaokolewa hai?
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Tuombe miujiza Mpwa
   
 5. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wasemaji wa wizara hawajui chochote aibu kubwa , jamani tuna viongozi au Vioo-Ngozi?
  andgalia nukuu hii hapa chini -Source Mwananchi:

  Siku 119 za Watanzania mikononi mwa maharamia Send to a friend Saturday, 05 March 2011 09:32 0diggsdigg

  Geofrey Nyang'oro na Mashirika ya habari

  WATANZANIA 14 waliotekwa na maharamia wa Kisomalia katika meli ya MV Aly Zoufecar, Novemba Mosi mwaka jana, wameokolewa wakiwa hai nchini Madagascar.

  Watanzania hao ni miongoni mwa watu 28 waliookolewa na Jeshi la Wanamaji la Madagascar kutoka mikononi mwa maharamia hao baada ya kuishi melini wakiwa mateka kwa siku 221. Wakati meli hiyo inatekwa nyara ilikuwa na abiria 29; Watanzania 14, WaComoro kumi na moja na raia wa Madagascar wanne.

  Meli hiyo ilitekwa ilipokuwa ikisafiri kutoka Moroni, Comoro kuja Dar es Salaam ikiwa na watu 29 na mmoja kati yao aliuawa kwa kuchinjwa muda mfupi baada ya utekaji huo.

  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam, wakala wa meli hiyo, Seif Athuman alisema meli hiyo imeokolewa Jumapili ya Februari 27, mwaka huu na kwamba tayari imewasili katika ufukwe wa Madagascar Watanzania wote wakiwa salama.

  "Meli yetu imepatikana hii ilitokana na kazi iliyofanywa na Jeshi la Madagascar na hivi ninavyokuambia nimepatiwa taarifa kuwa watu wote waliokuwa mateka wamewasili salama isipokuwa mmoja tu aliyeuawa muda mfupi baada ya kutekwa kwa meli hiyo," alisema Seif.

  Alipoulizwa jana kuhusu kupatikana kwa Watanzania hao, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Assah Mwambene alisema serikali haijapata taarifa hizo.

  "Hadi sasa hakuna taarifa hizo pengine katibu mkuu angekuwa katika nafasi ya kufahamu hilo lakini kwa bahati mbaya aliyepo ni mgeni hivyo si rahisi kufahamu taarifa hizo na yule aliyekuwepo ameishaondoka hawezi kujibu jambo lolote kuhusu wizara," alisema Mwambene katika mazungumzo yake ya simu na gazeti hili.

  Mwambene alisema serikali itafuatilia suala hilo mwishoni mwa wiki na pengine itatoa taarifa mwanzoni mwa wiki ijayo.

  Meli ilivyopatikana
  Seif alisema muda wote meli hiyo ilipokuwa chini ya maharamia hao ilikuwa ikitumiwa kwa shughuli za kihalifu hadi ilipofika kwenye Pwani ya Madagascar baada ya kuishiwa mafuta na chakula.

  Alisema kutokana na hali hiyo, maharamia hao waliteua ujumbe wa watu sita wakiwemo Watanzania wawili, nahodha, mfanyakazi wa ndani wa meli hiyo na maharamia wawili kwenda kutafuta mafuta kwa ajili ya kuendelea na safari yao.

  Alisema Jumatatu ya Februari 21, mwaka huu watu hao sita wakiwa katika boti ndogo (mtumbwi) walifika katika bandari ndogo ya Antsiranana iliyopo kaskazini mwa Madagascar.

  Alisema walipowasili katika moja ya visiwa vya nchi hiyo, mwanzoni mwa wiki iliyopita, nahodha wa Meli hiyo ambaye ni raia wa Comoro, Soilihi Boinaheri alizungumza Kireno na baadhi ya wakazi wa Madagascar akiwaarifu kwamba wao ni mateka wa maharamia wa Kisomali.

  Alisema wananchi walitoa taarifa Polisi na ndipo watu hao sita wakiwemo maharamia wawili walipokamatwa na Polisi na kuwekwa kizuizini kwa mahojiano.

  Alisema baada ya mahojiano ya muda mrefu, polisi waliendelea kuwashikilia na kupeleka kikosi cha wanamaji katika meli hiyo ambacho kilifanikisha mpango wa kuokoa meli hiyo na mateka wote wakiwa salama.

  Walivyokamatwa
  Habari kutoka Madagascar zinasema kuwa meli hiyo ilikamatwa na mateka wote kuokolewa baada ya msako wa siku tatu ulioendeshwa na vyombo vya ulinzi vya Madagascar vikisaidiwa na mpango wa kukabiliana na maharamia wa Jumuiya ya Ulaya (EU) uitwao, Atalante.

  Mratibu wa Oparesheni dhidi ya Uharamia Madagascar, Rolland Rasolofonirina aliliambia Shirika la Habari la AFP kuwa: "Ilikuwa ni operesheni salama na hakukuwa na msuguano. Watuhumiwa hawa wa uharamia hawakuwa na silaha na walipotuona walijisalimisha mara moja."

  "Kulikuwa na watu 37 na 12 kati yao walikuwa ni watuhumiwa wa uharamia na abiria 25 kutoka Madagascar, Tanzania na Comoros. Watatu kati yao ni wanawake."

  Kwa mujibu wa Rasolofonirina, wanawake hao watatu walikuwa wamedhoofu kutokana na kuishi mikononi mwa maharamia kwa muda mrefu na walipewa huduma za tiba mara tu baada ya kufikishwa katika boti ya uokoaji.

  Wote waliokuwa katika boti hiyo bado wanashikiliwa na mamlaka ya Madagascar katika bandari ndogo ya Antsiranana. Serikali ya Madagascar haijatoa tamko lolote kuhusu ni lini raia wa nchi nyingine wakiwemo Watanzania watarejeshwa katika nchi zao na kwa utaratibu gani.

  "Bado tuko kwenye mchakato wa kufanya uamuzi ni njia ipi tuifuate katika kushughulikia suala hili na hatimaye kuwezesha watuhumiwa kufunguliwa mashtaka."

  "Chombo hiki kilikuwa umbali wa maili 70 mashariki mwa Cape Amber," alisema Rasolofonirina akimaanisha kisiwa kilichopo kaskazini kabisa mwa Bahari ya Hindi na kuongeza: "Waliishiwa mafuta kabisa na walikuwa wamebakiza lita 30 tu za maji safi ya kunywa."

  Majina ya mateka
  Watanzania ambao walikuwa miongoni mwa mateka ni Tomas Hussein ambaye ni mfanyakazi katika meli hiyo, Augustin Ilias, Rosemary Maati, Paul Gue, Didas Kitabazi, Bary Omary, Azizi Juma na Mohamed Bundala.
  Wengine ni Abdallah Mketo, Shandali Mang, Rahma Mbaba, Stephen Ndane, Othuman Seleman na Tai Hamisi.

  Mhandisi katika meli hiyo, Ali Ben Youssouf (Sulla) wa Comoro ndiye aliyeuawa kwa kuchinjwa na maharamia hao muda mfupi baada ya kutekwa kwa meli hiyo.

  Raia wa Comoro ambao walikuwa kwenye meli hiyo ni Soilihi Boinaheri ambaye ni nahodha, Backri Ibrahimm Mohamed Hamadi na Youssouf ambaye kwa sasa ni marehemu hawa ni wafanyakazi wa meli.

  Wengine ni Maissara Mhadjou, Ascar Alphonse, Kubama Fadhili, Kassimou Ismaila, Abouobi Soeuf Toilab Mlomri na Dhoihikou Athoumane ambao ni abiria. Raia wa Madagasca ni Abdou Ali Meca, Hassan Bao (Bosco), Dodo Leonad na Robi Matelot wote wakiwa ni wafanya kazi ndani ya meli.

  Safari ya Meli hiyo

  Kwa mujibu wa wakala wa Meli kutoka Kampuni ya Transworld Shipping Co. Ltd, Seif Athumani, meli hiyo iliondoka mjini Moroni Novemba 3, mwaka jana kuelekea Dar es Salaam ikiwa na watu 29 ambao wafanyakazi ni tisa na abiria 20.

  Mara baada ya kuiteka, maharamia hao walitaka walipwe dola za Marekani 150,000 sawa na Sh222 milioni ili waweze wawaachie huru mateka pamoja na meli hiyo.

  Kiasi hicho cha fedha kilimshtua mmiliki wa meli hiyo ambaye alisema hawezi kulipa na kwamba suala la usalama wa watu waliokuwemo aliziachia serikali za nchi zao

  Hapo nilipopigia mstari panatia shaka juu ya umakini wa viongozi wetu kutojali raia wake.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Hhhaaaaa, hata hilo jina lake, cheo chake vyote full utata
   
Loading...