Ipi tathmini yako kuhusu siku 100 za Rais Samia madarakani?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Mama katimiza siku 100 madarakani baada ya kifo cha Magufuli

Ukiachana na kicheko kwa wafanyakazi weka tathmini yako ya haki hapa
  • Alikopatia
  • Alikokosea
  • Alikochapia
  • Alikozembea
  • Alikokurupuka
Weka projection yako na ushauri wako kwake. Anatusoma a ametuasa tusikosoe tu na kujibishana mitandaoni bali tushauri kwa weledi na tutoe ushauri wa kujenga
 
Hakuna tena anaeogopa kukosoa.

Iwe Jf au hata ma group ya watsap.

Hakuna anaeogopa kutekwa wala kufatiliwa na Nissan nyeupe.

Kila mtu anajiona Yuko huru kutoa mawazo yake.

Wabunge wa CCM sasa wanaikosoa serikali.

Upinzan wanatembea nchi nzima kufanya siasa.

Mahakama zinafanya kazi bila maagizo ya wanasiasa.

Wanamuziki wanaimba bila kuogopa.

Asasi za kiraia zimeanza kufufuka.

Tra imeacha kenyanganya hela kibabe.

Siku 100 za neema tupu kwa waungwana na wenye akili...
 
Sijui kwanini wanazi na vijana wa chama chake wamemnunia na wanamsimnga kila kona
Tatizo ni kwamba mama ameziba mianya yote ya wale walokuwa wakimsifu mkulu huku wakila keki ya Taifa gizani.

Na teuzi za ukada hakuna tena...Hapo ni lazima wamnunie mana walipigana kufanya mapambio lakini hatimaye mama kageuza meza.

Ili nchi iendelee lazima demokrasia ifuatwe, na mama ndo analoamini. Sasa wenzangu na mie watu wa mapambio na wale wa kutumia dola leo hii hawana demand tena.
 
Waione
Mataga
Lmb7
Skm gang
 
Mama amenikosha tu kwenye usawa.
Hataki dhuluma
Hataki uonevu
Hataki mabavu
Anataka usawa
Anataka uhuru kwa kila mtu
Ameruhusu kukosolewa (anajiamini hapo)
Yan ni rais anaetufaa

Kakosea tu hapa
Kumteua Mwigulu kuwa waziri wa fedha
Na hizi teuzi za maDC
Lameck kawekwa pale kimkakati ila akizingua atazinguliwa ASAP
 
Back
Top Bottom