Siku 100 Mama Samia zimetosha kusahaulisha msiba wa Rais Magufuli

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nawasalimu kwa jina la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania...na wote semeni kazi iendelee.

Siku 100 za Mama Samia Suluhu Hassan zimekuwa za furaha na amani kwa asilimia kubwa ya watanzania kana kwamba hatukupatwa na msiba wa kiongozi mkuu wa nchi.

Ukipita ofisi nyingi za umma wafanyakazi wanafuraha, kifupi hawana 'muhaho" wala hofu Kama ilivyokuwa miezi kadhaa nyuma.

Ni miezi mitatu tu imepita lakini msiba umesahaulika kabisa labda kwa familia na wale waliomtumainia yeye.

Siku 100 zimefuta utawala na kuleta uongozi.

Siku 100 zimewafanya wale wote walioropoka bila staha miezi michache nyuma kushika adabu na kunena kwa staha. Mtizame Ndugai, Mwigulu au Ole Sabaya.

Siku 100 zimewafanya wenye mawazo kinzani waongee, majaji wahukumu bila hofu, polisi wakamate kwa sheria na wanahabari waandike na kutangaza uhalisia bila kutetemeka.

Hakika siku 100 zimekuwa za faraja na kutusahaulisha Kama tulipata msiba.

Siku 100 zimefuta "one man show" na matamko ya kudhalilisha utu wa wateule. Naamini Kabudi anafuraha ila hawezi toka hadharani kusema.

Siku 100 zimefuta majisifu, majigambo na mbwembwe za kila aina zilizofanya baadhi ya watu wajione wanayo hatimiliki ya Tanzania mfukoni na sisi wengine wote ni wahamiaji tuliopewa hifadhi hivyo masimango na kejeli ni stahili yetu.

Siku 100 za Mama Samia zimewavuta na kuwapulizia "wapinzani" kale ka dawa kanakosifika kwa watanga na sasa wamelewa na wanaimba sifa za kupongeza na kufurahia uongozi. Uongozi wa watu ni limbwata tosha, sisi sote ni Watanzania na hulka yetu tunaijua, kupendana bila kujali itikadi zetu.

Mama Samia amejua kuumaliza msiba kibabe na kuwasahaulisha watanzania machungu waliyopata tangu 2015 kwa siku 100 tu! Kama angeboronga, msiba ungeendelea kuwachoma watanzania, lakini ameumaliza kibabe na sasa marehemu apumzike kwa amani.

Watanzania tukumbuke kusamehe saba mara sabini na kuwa marehemu hasemwi vibaya.
 
Back
Top Bottom