Sikio linauma sana, nahitaji msaada wa Hospital ninayoweza kupata matibabu

Dx and Rx

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,302
3,068
Salamu wakuu.

Ni matuamini yangu mumeingia salama katika huu mwaka mpya wa 2022.

Kwa wale ambao hamjaingia mkiwa salama kama mimi, yote ni kheri, kikubwa tunapumua.

Kichwa cha uzi kinajieleza, mwenye kujua Hospital inayoweza kunitibu tatizo hili hapa Dar es Salaam au popote mikoani naomba anijuze.

Hii ni mara ya tatu sasa sikio kuuma tangu August mwaka jana.

Mara ya kwanza lilipoanza kuuma nilienda Muhimbili nikapatiwa dawa(Amoxclav, Hydrogen peroxide Mouth wash na Paracetamol). Baada ya kutumia liliacha kuuma ila baadaye baada ya muda fulani lilianza kuuma tena na nikanunua hizo dawa nikazitumia na kuacha kuuma tena.

Sasa limeanza kuuma tena kwa mara ya 3. Nahisi tatizo limekuwa kubwa linahitaji matibabu zaidi ya kulimaliza kabisa

Ahsanteni wakuu natumaini nipata msaada wenu
 
Pole sana! Nilisikia kina hospital hapo magomen wanatibu vizuri sikio cjui inaitwaje nimesahau, ila wakat unasubiria kwenda hospital tumia kitunguu maji, kikate vipande hlf vibandike kuzunguka sikio kwa nje halaf acha kwa muda hata wa robo saa au mpaka ukiona vinakuunguza vitoe rudia mara uwezavyo nakuhakikishia ndan ya siku tatu maumivu utayasahau ila usisahau kuleta mrejesho, lakini pia tafuta kuna uzi humu unazungumzia matibabu ya sikio ili upate uelewa zaid! Pole sana!
 
Hospital ya Magomeni inaitwa Ekenywa.

Sawa mkuu nitajaribu na kuleta mrejesho
 
Kwan linatoa usaha au?
Hapana, halitoi.

Ila nahisi kama kuna uvimbe ndani ya sikio la kati/ kwenye ngoma ya sikio kwani maumivu ninayopata ni yale yanayofanana na maumivu ya uvimbe.

Mwaka jana nilipoenda Muhimbili, Daktari alijaribu kuchunguza na kifaa kinaitwa Otoscope ila hakuweza kubaini kama kuna uvimbe ndipo akaniandikia dawa tu
 
Owk sawa.....ila MAFUTA ya kuku mara nying husaidia kutibu kuumwa kwa sikio,,, anyway ngoja watakuja wataalam nao watatoa ushaur zaid mkuu!
 
Hili sikio limeendelea kuonesha sura mpya.

Sasa linatoa maji ya rangi ya njano kwa mbali..

Hivi hili tatizo Madaktari mumeshindwa kulitibu?

Nimezunguka Muhimbili(mara nyingi), TMJ, Ekenywa, Hear Well Audiology Clinic, Agakhan Polyclinic nimeambulia patupu huku tatizo likiendelea kuwa kubwa.
 
Umetumia dawa kama ulivyoelekeza au unatumia unapojiskia bila kujali muda wewe ?

Isijekuwa uzembe wako tu wa kutumia dawa ukashangaa infectiln imefanya resistance.

Tumia dawa kwa usahihi na kwa muda auliopangiwa.

Sikulaumu ila hili ni angalizo
 
pole,una tatizo lako la otitis media linaweza kuwa bacteria aina ya cocii es strepto au stamphylacoc,basi kwa kuwa hatuna uhakika wa gonjwa lenyewe, nikushauri.tumia cefalexin capsule 500mg tds siku 7 pia metronidazole 800mg bd siku 7 hakafu piroxim 1mara 2 siku 5 then tupe mrejesho
 
Inaweza kuwa chronic suppurative otitis media, hivyo utahitaji kufanya culture and sensitivity of the pus, xray and possible other imaging studies , kisha utapata matibabu ipasavyo including aural toilet with antibiotics au surgery kulingana na ukubwa wa tatizo.
 
Lilipoanza kuuma kwa mara ya kwanza nilienda Muhimbili, Dk alichunguza na Otoscope hakubaini chochote akaniandikia dawa( Amoxclav ya siku 7, Paracetamol na Hydrogen mouth wash).

Nilitumia hizo dawa hadi zikaisha na lilipona.

Mwezi wa 10 mwaka jana lilitaka kuanza kuuma tena, nikanunua hizo dawa tena nikatumia likapona.

Sasa kwa mara nyingine tena limeanza kuuma na nimeanza kutumia dawa hizi hizi tangu tarehe 29 Dec nikamaliza dose tarehe 7 Jan(nimetumia dose ya siku 10)

Baada ya hapo(kuanzia ijumaa iliyopita) lilianza kutoa maji maji yenye rangi ya njano kwa mbali huku maumivu yakipungua.

Nimekuwa nikivuta hewa halafu nabana pua na mdomo halafu naisukuma hewa kwa nguvu, hapo nalisikilizia kama linatokota huku likitoa sauti ya mluzi. Kitendo hiki kimesaidia kutoa maji maji mengi zaidi jambo lilipolekea maumivu kupungua zaidi.
 
pole,una tatizo lako la otitis media linaweza kuwa bacteria aina ya cocii es strepto au stamphylacoc,basi kwa kuwa hatuna uhakika wa gonjwa lenyewe, nikushauri.tumia cefalexin capsule 500mg tds siku 7 pia metronidazole 800mg bd siku 7 hakafu piroxim 1mara 2 siku 5 then tupe mrejesho
Asante sana mkuu
 
Inaweza kuwa chronic suppurative otitis media, hivyo utahitaji kufanya culture and sensitivity of the pus, xray and possible other imaging studies , kisha utapata matibabu ipasavyo including aural toilet with antibiotics au surgery kulingana na ukubwa wa tatizo.
Nilionana na Specialist Agakhan nilitarajia aingie deep kwenye kuchunguza lakini kaishia kumulika tu na kuniandikiwa dawa za kutumia.
 
Pole sana Mkuu, inawezekana kilikua kipele na kimetumbuka kimekua kidonda sasa ndio hayo maumivu unayapata. Hayo maumivu nimewahi kuyapitia. Pole sana .

Ukiweza Chukua kitunguu Saumu punje tatu na usage na maji kidogo sana yawe ya uvuguvugu na utatumia kuweka kwenye Sikuo, ukiweza utadondoshea matone matatu kutwa mara tatu. Utapona Kama ni Fungus, kidonda au uchafu umekwama sehemu utatoka na utapona kabisa.
 
Kama bado linakusumbua kawaone madaktari walio bobea Muhimbili. Na mimi yalinisumbua sana.... Nilienda ponea Muhimbili.
 
Back
Top Bottom