Sikio la kufa halikii dawa

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
NIMEKOSA KICHWA CHA MAKALA HII FUPI.

Tuliimba wimbo ulio bora wa 'chaguo la Mungu' mwaka 2005. Mwangwi wa sauti za wimbo ule ulianza kufifia mwaka 2008, miaka mitatu baadae.
Wimbo wa mwaka 2015 uliitwa 'rais mzalendo'/ muadilifu.
Ikumbukwe kwamba Mh. Jakaya Kikwete aliitwa JK wa pili kwa maana ya Julius Nyerere wa pili. Na sasa watu wameanza kumlinganisha Magufuri na Nyerere. Ni vichekesho visivyo na lengo la kuchekesha.
Kama miaka mitatu ilitosha kumchoka JK wa pili aliyeshinda kwa kura halali zaidi ya 80%, ni miaka mingapi itatosha kumchoka Nyerere wa pili aliyeshinda uchaguzi kwa nguvu za dola?

Tumeona jitihada za kupambana na watuhumiwa wa ufisadi, angalau kwa kuanza na wale anaowamudu. Bado tunasubiri. Tunasubiri kuona watuhumiwa wakiwajibishwa na sio kuishia kufukuzwa. Mtu anayejifikirisha atatamani kujiridhisha kwamba mawaziri na makatibu wakuu wa wizara ya fedha wakati wa JK hawakuhusika na ufisadi wakati meneja wa TRA akifanya ufisadi mkubwa.

Mtu anayejifikirisha atatamani kujiridhisha pia kuwa mkurugenzi wa bandari aliweza kufanya ufisadi mkubwa bila mkono wa mamlaka za uteuzi au mawaziri wa wizara husika.

Mh. Zitto Kabwe ametoa rai leo kwenye mkutano wa ACT huko kurasini kwamba bado serikali 'inapapasa' suala la ufisadi. Escrow bado inalipwa visivyo halali.

Pamoja na kwamba wananchi wa kawaida bado kupata ahueni ya maisha; gharama za mahitaji ya msingi kula, kuvaa na makazi bado hazijatengamaa. Kwa kutambua kuwa bajeti yake bado haijaanza, Ndio maana tunasubiri.

Tumeona pia, uwazi katika mgawanyo wa pato la taifa kila mwezi. Mambo mazuri ambayo hayakuwapo awali. Uwazi unaondoa wasiwasi, unaondoa walakini.

Lakini kitendo cha Serikali ya Magufuri kuzuia bunge kuoneshwa moja kwa moja kinastua watu makini. Kitendo hiki kinaipunguzia serikali ya magufuri idadi ya watu makini walioanza kuiamini. Hakuna mzalendo, anayetambua sheria, anayefahamu dhana ya utawala bora, anayetambua umuhimu na maana ya uwazi na uwajibikaji wa serikali atakayeunga mkono kichekesho hiki. Taratibu magufuri anajiongezea wapinzani.

Kwa bahati mbaya wapinzani anaoongeza ni watu wenye akili. Wajinga wanakubaliana na utaratibu huu mpya duniani, kwa kuwa fikra zao zinafuata matendo ya watu walioamua kuwashabikia kwa kila kitu.

Sasa ni wazi kwamba wapinzani wameanza kupata pa kukosoa. Na kwa jambo hili, serikali inakosoleka vizuri sana bila kutumia nguvu. Zaidi kitakachotumika ni mabavu tu, lakini kitendo cha kuficha mikutano ya bunge ni cha aibu. Waziri Nape Nauye anaweza kudhani kwamba anaisitiri serikali, lakini kwa kitendo hiki ameivua nguo serikali, ameidhalilisha serikali inayojitutumua kutafuta kuaminiwa na wananchi.

Nape Nnauye akumbuke kuwa nchi haijengwi na serikali peke yake. Nchi inajengwa na wananchi. Serikali ni chombo cha kuwezesha wananchi ili wajenge nchi yao, sio chombo cha kupambana na wananchi wanaokosoa serikali yao. Kuficha mijadala ya bunge, ni vita dhidi ya wananchi.

Bunge ni mkutano wa wananchi, ni vile watanzania wote hatuwezi kukutana mahali pamoja kujadili mambo yetu, kwa kukosoana, kupongezana, kuongozana, kukumbushana na kufundishana. Kwa sababu hakuna eneo la sisi wote kukutana basi tumewatuma wachache watuwakilishe. Lakini serikali ya Magufuri na Nape Nauye wametupora hakiaya kukutana kitaifa. Ni tendo la aibu.
 
NIMEKOSA KICHWA CHA MAKALA HII FUPI.

Tuliimba wimbo ulio bora wa 'chaguo la Mungu' mwaka 2005. Mwangwi wa sauti za wimbo ule ulianza kufifia mwaka 2008, miaka mitatu baadae.
Wimbo wa mwaka 2015 uliitwa 'rais mzalendo'/ muadilifu.
Ikumbukwe kwamba Mh. Jakaya Kikwete aliitwa JK wa pili kwa maana ya Julius Nyerere wa pili. Na sasa watu wameanza kumlinganisha Magufuri na Nyerere. Ni vichekesho visivyo na lengo la kuchekesha.
Kama miaka mitatu ilitosha kumchoka JK wa pili aliyeshinda kwa kura halali zaidi ya 80%, ni miaka mingapi itatosha kumchoka Nyerere wa pili aliyeshinda uchaguzi kwa nguvu za dola?

Tumeona jitihada za kupambana na watuhumiwa wa ufisadi, angalau kwa kuanza na wale anaowamudu. Bado tunasubiri. Tunasubiri kuona watuhumiwa wakiwajibishwa na sio kuishia kufukuzwa. Mtu anayejifikirisha atatamani kujiridhisha kwamba mawaziri na makatibu wakuu wa wizara ya fedha wakati wa JK hawakuhusika na ufisadi wakati meneja wa TRA akifanya ufisadi mkubwa.
Mtu anayejifikirisha atatamani kujiridhisha pia kuwa mkurugenzi wa bandari aliweza kufanya ufisadi mkubwa bila mkono wa mamlaka za uteuzi au mawaziri wa wizara husika.
Mh. Zitto Kabwe ametoa rai leo kwenye mkutano wa ACT huko kurasini kwamba bado serikali 'inapapasa' suala la ufisadi. Escrow bado inalipwa visivyo halali.
Pamoja na kwamba wananchi wa kawaida bado kupata ahueni ya maisha; gharama za mahitaji ya msingi kula, kuvaa na makazi bado hazijatengamaa. Kwa kutambua kuwa bajeti yake bado haijaanza, Ndio maana tunasubiri.

Tumeona pia, uwazi katika mgawanyo wa pato la taifa kila mwezi. Mambo mazuri ambayo hayakuwapo awali. Uwazi unaondoa wasiwasi, unaondoa walakini.

Lakini kitendo cha Serikali ya Magufuri kuzuia bunge kuoneshwa moja kwa moja kinastua watu makini. Kitendo hiki kinaipunguzia serikali ya magufuri idadi ya watu makini walioanza kuiamini. Hakuna mzalendo, anayetambua sheria, anayefahamu dhana ya utawala bora, anayetambua umuhimu na maana ya uwazi na uwajibikaji wa serikali atakayeunga mkono kichekesho hiki. Taratibu magufuri anajiongezea wapinzani. Kwa bahati mbaya wapinzani anaoongeza ni watu wenye akili. Wajinga wanakubaliana na utaratibu huu mpya duniani, kwa kuwa fikra zao zinafuata matendo ya watu walioamua kuwashabikia kwa kila kitu.

Sasa ni wazi kwamba wapinzani wameanza kupata pa kukosoa. Na kwa jambo hili, serikali inakosoleka vizuri sana bila kutumia nguvu. Zaidi kitakachotumika ni mabavu tu, lakini kitendo cha kuficha mikutano ya bunge ni cha aibu. Waziri Nape Nauye anaweza kudhani kwamba anaisitiri serikali, lakini kwa kitendo hiki ameivua nguo serikali, ameidhalilisha serikali inayojitutumua kutafuta kuaminiwa na wananchi.
Nape Nnauye akumbuke kuwa nchi haijengwi na serikali peke yake. Nchi inajengwa na wananchi. Serikali ni chombo cha kuwezesha wananchi ili wajenge nchi yao, sio chombo cha kupambana na wananchi wanaokosoa serikali yao. Kuficha mijadala ya bunge, ni vita dhidi ya wananchi.
Bunge ni mkutano wa wananchi, ni vile watanzania wote hatuwezi kukutana mahali pamoja kujadili mambo yetu, kwa kukosoana, kupongezana, kuongozana, kukumbushana na kufundishana. Kwa sababu hakuna eneo la sisi wote kukutana basi tumewatuma wachache watuwakilishe. Lakini serikali ya Magufuri na Nape Nauye wametupora hakiaya kukutana kitaifa. Ni tendo la aibu.
wew nawe mnatuchosha Bunge bunge ... live khaa lina faida gani kwa mtu wa kawaida yule kule vijijini
 
Back
Top Bottom