Sikio kupungua uwezo ghafla baada ya kutumia pamba za masikio

Los santos

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
955
2,023
Habari za majukumu wapendwa leo kuna mwenzangu kapatwa na shida, asubui wkati anaamka anasema alisikia sikio linawasha ,Sasa akachukua pamba ya kusafisha masikio akaanza kusafisha,ghafla sikio la kulia likawa kma vile limeingiwa na maji na uwezo wa kusikia ukapungua ...je kabla ya yeye kwenda hospital ushauri wenu wadau afanyeje.....
 
Pitia huu uzi pia

Wale wapenzi wa kuchokonoa masikio kwa kutumia pamba stick na vijiti yaliyonikuta mimi iwe funzo kwenu
 
Pitia huu uzi pia

Wale wapenzi wa kuchokonoa masikio kwa kutumia pamba stick na vijiti yaliyonikuta mimi iwe funzo kwenu
Habari
Pole kwa yaliyotokea.
Kwanza, swala la kusafisha masikio kwa pamba huwa haushauriwi kufanya hivyo. Masikio yana utaratibu wake binafsi wa kusukuma uchafu nje/kujisafisha. Jukumu lako ni kutoa ule uchafu unaoonekana ukifika pembeni/nje ya sikio.

Pili, inawezekana kitendo kilichofanyika kimesababisha kusukuma nta ndani na kusababisha kuziba kwa njia/mechanical obstruction.

Ni vyema kufika kituo cha afya ili kuweza kuangaliwa/kufanyiwa uchunguzi na kupata tiba sahihi.
 
Kitunguu saum kisage changanya na mafuta yanazi yawe moto kwambali then ajitie ata matone mawili
Kitungu saumu hakiwezi kutibu maradhi hayo aliyokuwa nayo kwani ameharibu ngoma ya ndani ya Sikio huenda amepasua ngoma ya masikio ndio maana hawezi kusikia vizuri .Kuna dawa ingine lakini sio Kitunguu saumu.
 
Habari za majukumu wapendwa leo kuna mwenzangu kapatwa na shida, asubui wkati anaamka anasema alisikia sikio linawasha ,Sasa akachukua pamba ya kusafisha masikio akaanza kusafisha,ghafla sikio la kulia likawa kma vile limeingiwa na maji na uwezo wa kusikia ukapungua ...je kabla ya yeye kwenda hospital ushauri wenu wadau afanyeje.....
Mkuu pole sana kwa hayo matatizo yaliyo kukuta nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom