Sikiliza Mjomba...

Jafar

JF-Expert Member
Nov 3, 2006
1,136
52
Baadhi ya maneno kwenye wimbo wa salamu zako mjomba..

Umetupima viatu mwaka huu, baada ya miaka 5 utatuuliza, mlikuwa mnataka viatu gani?

Ukienda msibani, mfiwa utamjua, atakuwa amevaa tofauti na ni mwenye huzuni, ni wewe mwenye huzuni msiba wetu kuubeba.

Vibwaya msiviweke ghalani, iko siku mtavikumbuka ili tuvae na tucheze ngoma yetu iitwayo ya kishenzi.

Mtembea peku hapendi, ila hana viatu.

Jaribu kukaa na kula na watoto wa majalalani, kuliko kukaa kwenye jukwaa na kusema "this country" bwana "is very poor"

Rushwa ni wimbo uliozoeleka kwenye masikio yetu, tuondolee wimbo huu ili tuwe na furaha.

Gima lililosahaulika ni sawa na gogo, katika magogo yote la mvule si la mninga.

Kiumbe mwenye uhai huongozwa na tamaa. Majanga yanapozidi mioyo ya watu huota kutu.

n.k.

Je Mjomba anayepewa salamu hizi ni JK ?

Sikiliza: http://www.box.net/shared/a5kscro5ic
 
Mimi binafsi nahisi kuwa mjomba huyu ni JK. Msanii ametumia lugha safi kweli yenye tafsida nzuri.
Kazi kwake mjomba kusikiliza na kuufanyia kazi wimbo hu
 
Bila shaka Mjomba katika wimbo huu ni JK. Hapa lazima nikiri kwamba wimbo huu ni kati ya nyimbo zetu chache zilizo ''kwenda shule''. Tuwapongeze.
 
Mheshimiwa Huseni Ndovu, sorry Njovu karibu sana JF. Chukua kigoda kile pale usikilize, usome pia uchangie JF ili iweze kwenda mbeleeeeeeeee.
 
Bwana Jafar nafurahi kukaribishwa na mtu kama wewe ambaye ni Senior Member kwenye JF. Kama ulivyonitaka nivute kigoda, nimeshavuta na nasikiliziza, being a junior member nachukua tahadhari kwenye kuchangia nisije nikawa ''boa'' wapenzi wa JF.Nakushukuru sana Bwana Jafar
 
Salamu kwa mjomba ni moja ya nyimbo chache sana zenye kutoa somo kwa viongozi wetu na jamii nzima ya watanzania. Salamu kwa mjomba ni kombora kwa viongozi wote wa serikali iliyopo madarakani. Cha ajabu na kuchekesha huu wimbo unabaniwa na hausikiki mara kwa mara kwenye redio stesheni na hata kwenye televisheni kwa sababu umegusa penyewe kabisa.
 
..............!!!!................PIA NI TUNGO INAYOKUBALIKA KWA RIKA ZOTE......MAADILI PIA YAMO........SIO KUTULETEA WATOTO WA KIUME WALIOTOBOA MASIKIO YAO NA KUVAA CHENI ZA MIGUU,WAKISUKA NYWELE HUKU WAKIIMBA KWA KUBANA PUA....ETI USANII....USANII?
ANGALIENI WENZENI KINA MRISHO NA PROF J...(japo j naye tembo anaanza kulitia maji......eti siku hizi naye ana kihereni kimoja)
 
Wimbo huu ulitakiwa uchezwe siku ya ufunguzi wa kikao cha Butiama
 
Hakuna ubishi ujumbe ulifika kwa mlengwa lakini hawezi kututumikia sisi wakina kabwela kwa kuwa sio tuliomuiingiza madarakani. Wakati umefika sasa nasi wanyonge kutafuta mtumishi wetu muadilifu atakayetusikiliza na kukerwa na shida zetu na hata tukimtazama tutamuona kweli huyu anakerwa na shida zetu. Saa hizi mjomba na mafisadi wake wanapanga mkakati wakushika masikio na kuhakikisha tunawarudisha tena madarakani 2010 ili wakakamilishe malengo yao ya kufuja mali zetu kama ilivyokuwa kwa EPA na Richmond.
Mjomba kumbuka sauti ya wengi ni sauti ya Mungu!
 
Mh haifichiki,

Unakumbuka hadithi ile ya kule wakati Mariamu anamtembelea Elizabeth, katoto ka Eliza kakaruka mara tu aliposalimiwa! unafikiri alificha tena siri.....


Hoja zangu sio ngumu….
Loliondo , Buhemba, masaki beach wameshauza…
wamenogewa na utamu hata kidogo wanakikomba..
Wawekezaji wanatunyanyasa mbona ukimya mjomba..

Gavana hakusahaulika na hekalu lake la mfalme suleimani
 
Asante MM,
Leo unaweza kuonekana mwenye kichwa kidogo, lakini ukweli unatabakia siku yaja na Tanzania itakukumbuka!
God bless you.
 
Its very sad. Kudos Mzee MM, umenikumbusha mbali sana wakati uleee wa kupigania Uhuru
 
Teh teh wa mwaka gani huu ukute wengine tulikuwa bado haijulikani tutakuja lini katika ulimwengu huu.
 
Hongera sana Mwanakiji kwani ni ujumbe murua kabisa ingawa mjomba wako ni Kiziwi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom