Sikiliza 'beat' kwa makini, sauti tamu isikupoteze!

Coloneli

Member
Aug 24, 2020
35
151
MSANII mahiri na nyota kabisa kuliko wote nchini ametoa wimbo mpya. Katika suala la nyimbo mpya, hakuna sehemu huyu amewahi kushindwa, kwa sababu hata kama hautaki kuukubali muziki wake, utalazimika kuupenda kwa sababu media zote lazima ziupige, tena mara kwa mara kiasi kwamba japo huupendi, lakini unaufahamu!

Anachowashinda wasanii wenzake ni uwezo wake wa kifedha. Amehonga media zote, zinapiga nyimbo zake tu, na kidogo za wasanii wanaomuunga mkono ambao hata hivyo, hawaruhusiwi kutoa 'kazi' kali kumzidi.

Wale wasanii wa lebo pinzani anaoona wanahatarisha himaya yake, anawanunua na kuwaweka chini ya lebo yake. Wakijifanya jeuri, kwa sababu ya uwezo wake, anawanunua polisi ambao wanawabambikia kesi za uongo na kweli, wanapotea, au anawakodia majambazi na cha moto wanakiona.

Mwanzo mashabiki walikuwa hawaelewi nini kinaendelea, lakini kadiri siku zilivyokwenda, wakaelewa. Pamoja na kuwa media zote zilipamba nyimbo na matendo yake, wakazipotezea. Redio zote zilizopiga nyimbo zake watu wakaacha kusikiliza, magazeti yaliyompamba kurasa za kusomeka nayo yakakosa soko, televisheni nazo zikapoteza watazamaji ambao walizikimbilia zilipofika zamu za filamu, vichekesho au mpira.

Lakini wimbo wa safari hii, umekuja wakati ule wa zamani ukiwa bado unabamba na wenye mashabiki lukuki. Hakuna aliyeutegemea. Hii yote ilitokana na tetemeko kubwa kutokea, ambalo liliharibu miundombinu ya studio, kiasi cha wengi kushikwa na bumbuwazi na kusubiri kuona nini kitaendelea.

CD ya wimbo iliharibiwa vibaya na tetemeko hilo na kwa hakika, isingechezeka tena. Mahasimu wa msanii huyu mwenye mbinu nyingi, wakaanza kushangilia, wakiamini sasa mwisho wake umefika.

Ambacho bado hawajajua, ni ubora wa msanii huyu katika kucheza na akili za mashabiki. Anajua ni wakati gani wimbo wake umeisha, anajua ni wakati gani apate kiki na anajua jinsi ya kucheza na media!

Ghafla bila kutegemewa, nyota huyu wa muziki wa Tanzania ameibuka na wimbo mpya, mtamu kwelikweli, kiasi cha kuwashangaza hata mashabiki wake kindakindaki. Ajabu ya wimbo huu, hata wale mashabiki wa lebo pinzani nao wanaushangilia.

Hata hivyo, hawa wanaushangilia kwa kuamini kuwa wanawakomoa wale wenye lebo yao, ambao kwa mbali ni kama hawajapenda spidi ya wimbo mpya jinsi ulivyotrend.

Lakini nina kitu kimoja nataka kushare na wale wa lebo pinzani. Najua umependa wimbo mpya, hasa utamu wa sauti yake, lakini hebu sikilizeni beat kwa makini, mtagundua wimbo ni uleule.

Kilichofanyika ni kubadili mashairi na vionjo vya kinanda, lakini hati miliki bado ni ya prodyusa yuleyule. Kama huamini hiki ninachokuambia upe muda wimbo huu!

sdp��^�
 
Kama wewe ni mgeni hapa, unaweza kudhani hapa anaongelewa Diamond Platinum's na Ali au konde boy; sina hakika, hi code nayo inahitaji connection kui decode?
 
CCM ni ileile eeh ilele wapinzani mnasemajeeeee?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom