sikieni story ya rafiki yangu huyu..

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,508
216
Kila tarehe 10 march huadhimisha siku ya watoto wa mitaani kwani miaka kadhaa iliyopita tarehe na mwezi kama huo aliingia rasmi mitaani kama mtoto aishiye kwenye mazingira magumu hadi miujiza ilipotokea akakombolewa baada ya kusota huko mitaani zaidi ya miaka miwili. Baadhi ta shida alizopata akiwa huko mitaa ni ni pamija na

1. Kunusurika kuuwawa na watu wenye hasira akidhaniwa mwizi, baada ya kukurupushwa usiku kwenye vilabu vya pombe za kienyeji alikokuwa amelala, aliokolewa na msamaria mwema aliyekuwa akimfahamu
2. Kulala kwenye vilabu vya pombe za kienyeji, stand za mabasi na madarajani hata wakati wa masika
3. Kulimishwa mashambani, madukani na migodini kwa ujira wa ugali, nk.

Anasema katika maisha yake amewahi kujaribu kujinyonga mara mbili ……anaongeza kuwa hajawahi kuona mtu akimpenda kwa dhati maishani mwake………….. hata wanawake alianza kuwapata baada ya kupata kazi na hivyo kuwa na pesa za kuwahonga.

Ilitokea miujza, akatokea mtu akamuingiza shule na kumtunza kwa miezi sita tu kabla hajasema mzigo wa kulea umemuelemea na kumfukuza nyumbani……..lakini kamwe hamsahau mtu huyo, kwani kwake ana hadhi ya malaika wa Mungu kwani milango ya elimu aliyomfungulia, hakuna shida wala dhiki wala mtu yoyote aliyeweza kuifunga hadi leo!!!!!!…………….. kuna maelezo marefu hapo yanafuatia lakini sasa tuko naye chuo kimoja huku nje ya nchi, yeye akichukua PhD,………….

Amenisimulia haya baada ya kumkuta amepamba chumba chake kwa maua na akisikiliza nyimbo za gospel kwa wiki nzima mfululizo (kumbuka tarehe 10 march ni jumatano ijayo), ndivyo anavyoadhimisha siku hii kwa mwaka huu,………… kweli story yake inasikitisha sana……… machozi yamenitoka leo…………

je, tumfariji namna gani huyu ndugu?...............
 
nnnhuuu!!! Mungu hapangiwi, hupanga mambo kwa ajili ya utukufu wake mwenyewe, wala huwezi kumhoji, tena hawezi chapwa!!!
 
"Mungu huandika kwa mistari iliyopindapinda". Njia zake si njia zetu. Ndiyo maana ni Mungu!
 
nimesoma nimesisimka...kwa sisi tulio mbali tutamuombea kwa Mungu azidi kumbariki..wewe uliyekaribu nae nakushauri ujiunge nae katika maombi yake hayo ya shukurani maana mkutanapo zaidi ya wawili mahali kwa ajili ya neno la Mungu,basi yeye hushuka na kuwa pamoja nanyi...m'barikiwe sana
 
inasikitisha ila nimefurahi sana kusikia ametoka mtaani na ameweza kufika alipo.MUNGU ni mkubwa.
 
asikomee kuliitia jina la bwana siku zote za maisha yake ,mie namuombea kwa mungu ampe na kumzidishia makubwa zaidi ya haya, na akumbuke hayo yalikuwa mapito ya maisha kwake habari inasikitisha sana lakini iko na neema na faraja siku zote
 
I have been here before.. de javu!

Mungu amuinue
Amsimamishe juu ya miamba
Amkinge na maadui wajao kama rafiki
Amponye na mkono wa mtesaji
Ampe furaha alalapo na aamkapo
Amwagie baraka zake kwa mujibu wa Kumb. 29
Na amletee karibu yake marafiki wa kike na wakiume
Ambao ni ndugu kuliko wale wa damu
Ambao hawatamuacha upweke; katika giza na katika nuru
Katika mvua na kati hari
Katika majanga na katika ya neema
Katika huzuni na katika furaha
Katika yote yaliyo mema.
Siku hii ambayo nilikuwepo leo.. ninamuinua kwake yeye Baba wa Mianga ambaye kwa jina lake "ubaba wote mbinguni na duniani" unaitwa!
 
Azidi kumuomba Mungu maana hakuna kinachoshindikana mbele zake, tuko naye katika maombi.
 
kwa kweli imenigusa sana namna anavyomshukuru Mungu na kumrudishia utukufu. licha ya kukosa malezi katika umri mdogo, mtu huyu havuti sigara wala bangi wala madawa ya kulevya ingawa maisha aliyoishi yalikuwa na vyote hivyo......... akiwa dar, wiki kama hii hutumia kula na watoto wa mitaani na kuwanunulia nguo.............

hivi sasa tunasikiliza wimbo huu hapa chini........... tujumuike kutafakari kwa paoja maudhui yake................ unaweza ukaanza ubeti wa mwisho halafu ukaridi wa mwanzo kama unataka kuuelewa vizuri..........CHOZI LA DAMU!

HAPA NINA MFANO HAI WA HILO CHOZI LA DAMU LILILOFUTWA KWA BARAKA ZA MUNGU

Wimbo: Chozi la Damu
Kwaya: RC, Parokia ya Makuburi
Watoto wa nyumba zote, njooni tuungane,
Tuwalilie wazazi chozi la damu,
Tupaze sauti zetu za majonzi na kwikwi,
Kwa wachache wenye huruma watatusikia,
Haki ya malezi bora tumenyang'anywa,
Urithi wa maadili tumefutiwa,
Dunia, dunia , dunia unatutesa,
Aaa dunia, dunia, tumekusea nini?
Oo dunia, dunia, mbona hupendi watoto!!!
Oo dunia, dunia, sikia kilio chetu.

1.
Dada zetu na mama zetu, tunajua mnajipenda
ingawaje tungetamani na sisi mtufikirie,
mavazi mnayovaa leo yanatufundisha nini,
mnafikiria nini kwa kizazi mnachokilea,
msije mkashagaa dunia siku zinazokuja,
viwanda vote vya nguo vitakapofungwa.

Watoto wa nyumba zote njooni tuungane…………..

2.
Kila siku tunapolala baba zetu hamjarudi
asubuhi tukiamka baba zetu mmeondoka,
siku tukibahatika kushituka usiku wa giza,
tunachokishuhudia ni mama anapigwa makofi,
na vitisho vya talaka, matusi na harufu ya pombe,
darasa gani mnatupa wazazi wetu.

Watoto wa nyumba zote njooni tuungane…………..

3.
Tukiruditoka shuleni madaftari hamkagui,
eti kwa kuwa tumechoka burudani mwatuwekea,
video mnazowasha picha za vita na mauaji,
au mikanda iliyorekodiwa sodoma gomora,
hamkumbuki ya kuwa mnayafuta ya darasani,
urithi gani mnatupa watoto wenu.

Watoto wa nyumba zote njooni tuungane…………..

4.
Kwenye chakula cha usiku siku zote baba hayupo,
kusali sala za pamoja, kwenye nyumba yetu ni mwiko,
anachelewa kutoka kwa mama mdogo yule wa siri,
au giza likizidi hatarudi mpaka asubuhi,
na mama akishajua mbio kwa anko ah usiseme,
familia moja baba na mama watano.

Watoto wa nyumba zote njooni tuungane…………..

5.
Kwa sababu ya mambo haya ndugu zetu wanaumia,
wapo wanaorandaranda mitaani bila makazi,
wengi wamelazimika kuajiriwa bado wadogo,
hawana tena nafasi ya kusoma wapate elimu,
na wengi wanajiuza miili yao ili waishi,
mbona dunia umetugeuka watoto.

Watoto wa nyumba zote njooni tuungane…………..
 
nimesoma nimesisimka...kwa sisi tulio mbali tutamuombea kwa Mungu azidi kumbariki..wewe uliyekaribu nae nakushauri ujiunge nae katika maombi yake hayo ya shukurani maana mkutanapo zaidi ya wawili mahali kwa ajili ya neno la Mungu,basi yeye hushuka na kuwa pamoja nanyi...m'barikiwe sana

nshukuru mpendwa......... kweli tuko pamoja naye hata sasa na hatuombolezi bali tunamsifu, tunamshukuru na kumtukuza Mungu kwa rehema zake zinazodumu vizazi hata vizazi.........
 
Jamani Mungu amtie nguvu, ampiganie katika kila jambo maana yeye ndiye muweza wa yote.naamini mungu hajamuacha kwa kumtesa ila hayoyote ni mapito na pia majaribu ni mtaji wakuongeza imani so umefika wakati anatakiwa kushukuru kwa kila jambo maana kama asingekutana na hayo asingepata chakuhadihia leo. kupitia shuhuda watu wanaokoka kwa hiyo kupitia habari hiyo inatufanya na sisi kujua kuwa kumbe hata sisi tunapopitia magumu ipo siku mungu atatufungulia milango. maana alisema jaribu lijapo kwa mlango mmoja yeye atalitoa kwa milango saba.
 
Jamani Mungu amtie nguvu, ampiganie katika kila jambo maana yeye ndiye muweza wa yote.naamini mungu hajamuacha kwa kumtesa ila hayoyote ni mapito na pia majaribu ni mtaji wakuongeza imani so umefika wakati anatakiwa kushukuru kwa kila jambo maana kama asingekutana na hayo asingepata chakuhadihia leo. kupitia shuhuda watu wanaokoka kwa hiyo kupitia habari hiyo inatufanya na sisi kujua kuwa kumbe hata sisi tunapopitia magumu ipo siku mungu atatufungulia milango. maana alisema jaribu lijapo kwa mlango mmoja yeye atalitoa kwa milango saba.

Hapo mimi nakubaliana na wewe kaka Zeddie!

Nakumbuka nilipokuwa nasubiri majibu ya darasa la saba,majibu yaliyotoka hayakuwa mazuri,hapo niliamini sitaweza kwenda form one,lkn kitu cha ajabu nilisukumwa kumwomba Mungu anipe shule nzuri,bahati nzuri nikapata shule nzuri 3 tofauti katika mikoa tofauti lkn nimejifunza mengi katika utofauti wa hizo shule 3 tofauti katika O level. Nilipomaliza form four majibu yalikuja mazuri,nikamwomba Mungu anipe shule nzuri zaidi ya hizo nilizotangulia akanipa shule ambayo sikuitegemea kuipata nzuri zaidi ya hizo nilizopitia. Form six majibu hayakuwa mazuri hapo sasa nikakata tamaa (na sitasahau katika hiki kipindi nimepitia magumu mengi sana) lkn bahati nzuri alikuja mama moja akaniambia Mungu ni mkubwa kuna kitu kikubwa kizuri amekuandalia wewe katika maisha yako,hivyo huna budi kumshukuru kwa kila alichokutendea basi tukamshukuru kwa pamoja, muda si mrefu nikapata chuo kizuuuri sana yaani mazingira ya kusoma ni mazuri zaidi hadi unajisikia raha,nikasoam mpaka nikamaliza hapo ilikuwa level ya Diploma, kwa kutumia Diploma hiyohiyo nika apply vyuo vingine for further studies,hali ikawa mbaya, nikarudi kwa yule mama aliyenishauri tumshukuru Mungu, nikamwambia yaliyonisibu, jibu alilonipa nilishangaa kumbe ilikuwa ni kitu kidogo sana, nilijiinua moyoni mwangu, nikamwomba msamaha Mungu hatimaye nikapata Chuo kizuri hapahapa Tanzania na kuchukua Bachelor.

Nilichojifunza:
1. Ukikwama mahali popote katika maisha yako the only solution ni kwa Mungu tu lkn wakati huohuo ni lazima ujishughulishe/utatue na hilo tatizo linalokukabili hapo Mungu ataongezea la kwake(Mfano huyo mama Mungu aliniongezea maarifa kupitia huyu mama).

2. Kitu kingine nilichojifunza ni kuchunga sana mioyo yetu, ukijiinua tu tayari lazima mikwamo itakuwepo, hapo dawa yake ni kujishusha, usijione kwamba wewe ni dhahabu kuliko wengine, usijione wewe una kila kitu kuliko wengine,nimegundua katika pita pita yangu kuna watu wengine Mungu anazungumza nao na anawalinda katika kila njia wanayopita.

3. Kila njia atakayopita/anayopita/aliyopita mwanadamu ni njia iliyoandaliwa na Mungu ili mwanadamu ajifunze na kuna vitu anataka huyo mwanadamu apate ili iweze kumsaidia huyo mwanadamu na wanadamu wengine wanaomzunguka popote pale atakapokuwa/atakapoenda katika maisha yake. So usidharau kabisa maisha aliyopitia mtu hata kidogo, wewe binadamu huwezi kujua kwanini huyo aliishi hivyo/anaishi hivyo mengine yawezekana ni adhabu au mafundisho kwake yaani kuna mambo mengi sana kama mchanga wa baharini.

4. Kingine ni kama vile Mungu anakuonesha mambo fulani fulani, haya watu huwa tunajisahau tulikotoka, na ndo maana unakuta tunapata wakati mgumu kwa namna mbalimbali, kama vile wastaafu hawapati mafao yanayostahili wao kupata hilo linatokana na wale wanaofanya kazi kutowakumbuka mema waliyotutendea hawa wazee huko nyuma, watoto yatima wengine hapa hawakumbuki walezi waliowalea utakuta kumbe Mungu aliwapelekea mtoto/watoto kwa hao walezi ili wamlee/awalee kwa maana anajua huyo mtoto/watoto w/atafika pale ambapo Yeye anataka w/afike,yaani kuna mambo mengi sana.

Mwisho: Tumshirikishe Mungu kwa kila jambo jamani,kuanzia nyumbani kwako hadi ngazi ya Taifa kwa namna yoyote ili Mungu asikie kutoka kwako na wengine.

Jumapili njema.
 
Mungu alisema, "Njoni kwangu ninyi nyote mnaosumbuka na kuelemewa na mizigo, nami nitawapumzisha"
Namtakia kila la kheri katika masomo yake, na asahau yote yaliyopita kwani yalikuwa ni mapito tu.
Akumbuke pia, maisha ni mafupi ,hivyo atumie nafasi hii kufurahi na kuwasaidia wale wote ambao wako katika mapito kama yale aliyopitia.
Hata mbuyu, ulianza kama mchicha!!
 
Anasema katika maisha yake amewahi kujaribu kujinyonga mara mbili ……
kaa nae katika siku yake hiyo (tar 10 March), mfariji tu kwa kuwa naye pamoja! mnaweza kutoka kuwasaidia watoto yatima na wengine waliomtaani!
 
Namtakia kila la heri...Kila jambo lina wakati wake na MUNGU hufanya kwa makusudi kabisa ili yeye atukuzwe Milele..Wala hahitaji faraja kwa sasa kwani huzuni na mateso vilishaisha...Ana bahati kwani amepata hata fursa ya kusoma PHD wapo ambao wanatamani lakini hawataweza kufikia malengo hayo kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao.
 
Mungu amzidishie baraka na elimu zaidi, ili nae siku moja aweze kuwasaidia wengine waliomitaani bado kupata msamaria mwema!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom