Sikieni hawa TCU:vyuo vingi havina sifa tanzania-tcu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikieni hawa TCU:vyuo vingi havina sifa tanzania-tcu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Mar 11, 2012.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TCU) imesema iwapo itasimamia ipasavyo sheria yake Vyuo Vikuu vya Tanzania vitalazimika kufungwa kutokana na kukabiliwa na uhaba wa wahadhiri.
  Tamko hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Ithibati wa Tume hiyo, Dk Christine Hongoke, alipokuwa akizungumza na Kamati ya Maendeleo ya Wanawake na Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wawakilishi Makao Makuu ya Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
  Alisema kwamba TCU imebaini kuwa kuna upungufu mkubwa wa wahadhiri wenye sifa za kufundisha katika vyuo vikuu hapa nchini jambo ambalo ni kinyume na sheria.
  Alisema kwamba Vyuo Vikuu vya Tanzania vimekuwa vikinyangÂ’anyana wahadhiri na kulazimika kuwatumia kwa zamu kufundisha wanafunzi kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.
  Hata hivyo, alisema kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kushirikiana na Serikali ya Ujerumani imeanzisha utaratibu wa kusomesha wahadhiri wa Vyuo Vikuu vya umma kwa kushirikiana na Shirika la DAAD la Ujerumani.
  Alisema kwamba Ujerumani imekuwa ikitoa nafasi za masomo (Skolashp) ngazi ya Shahada ya Uzamili mpango ambao ulianza utekelezaji wake mwaka 2009.
  Hata hivyo, alisema pamoja na Ujerumani kutoa hofa ya nafasi 20 za masomo ya ngazi ya shahada fursa hiyo haitumiwi ipasavyo kutokana Tanzania kushindwa kupeleka wanafunzi.
  Akitoa mfano, Dk. Hangoke alisema mwaka jana Tanzania ilipeleka watu sita kati ya nafasi 20 kutokana na wahadhiri kutojitokeza kuomba nafasi hizo.
  Dk Hangoke, alisema kwamba tangu kuanza mpango huo tayari wahadhiri 32 kutoka vyuo vikuu vya umma wamenufaika na mpango huo wa kusomeshwa nje ya nchi.
  Alisema kwamba tangu kuazishwa kwa TCU jumla ya vyuo vikuu 26 vimesajiliwa vikiwemo vyuo vikuu vishiriki Tanzania.
   
 2. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  Nahisi huyu dk na wenzake ni wendawazimu kujaktuambia vina mapungufu wakati sheria iko wazi akuna wahdhiri tuna funga anakuja kueleza iwe nini wakati ada wanaendelea kuchukua nahisi hii tcu imegeuka mkusanyiko wa wehu waliosoma na sasa wanapewa huruma ili wajifie na vijisent wakati elimu yetu inaelekea kuzimu
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  sifa za kupata scholarship ni zipi?kwa nini watanzania tunakosa sifa hizo ili tuweze kujirekebisha!
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwakuwa TCU ndio yenye mamlaka ya kutoa accreditation kwa vyuo vikuu, na ili chuo kikuu kiweze kupata accreditation lazima kitimize masharti kadhaa na hili la kuwa na wahadhiri wenye sifa stahiki za kitaaluma na tena wawe idadi ya kutosha ni kigezo cha lazima.
  Kama TCU inakiri kwamba vyuo vingi havijakidhi vigezo, sasa walivipa accreditation based on vigezo gani? Si ajabu sasa tuna wahitimu wengi wa vyuo vikuu lakini ni ''half cooked''!
  Nimekutana na baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu wasioweza ''ku manufacture hata sentensi'' moja kwa lugha ya malkia elizabeth kwa ukamilifu! Kumbe sababu kubwa ndio hii ya uzembe wa TCU. Sasa kuna haja gani wao kuwepo na kuendelea kutumia rasilimali za umma kuiharibu elimu ya juu badala ya kulinda ubora wake kama sheria inavyotaka na inavyoelekeza?
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hawa ndio wataalamu legelege sheria ziko wazi yeye anaweka utashi wake,kweli kuna muda mrefu kufikia maendeleo!!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Bongo zaidiya uijuavyo
   
 7. Manjagata

  Manjagata JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,750
  Trophy Points: 280
  Yaani hata huku wanachakachua? Hii nchi bwana! Kumbe ndo maana wasomi wetu wako shallow sana kwene mambo mengi tu! Yaani na vi-Diploma vyetu lakini tunawatoa jasho kwenye usaili! Kaazi kweli kweli!
   
 8. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Sasa km wanajua hivyo kwanini wasifatilie hilo swala? Mf kuna chuo kimoja kipo IRINGA kinatoa shahada na stashahada za ICT na fani nyingine yani upande wa ICT ni aibu...kwanza hakuna Walimu wenye sifa pili ata hao waliopo baadhi hasa wenye vyeo hawafundishi mpaka wanaICT waandamane ndo ataingia km mara tatu tu then haonekani huyo mwalimu na mbaya zaidi chuo hakimchukulii hatua zozote za kisheria, mwl mwenyewe ni mlevi anytime darasani haingii mitihani yake anacopy somewhere yani ni kero...TCU lazima kifatilie baadhi ya vyuo kwani bodi inatupa mikopo ambayo tutawajibika kulipa sasa tutalipaje kwa hali km hizi.....TCU simamieni sheria
   
 9. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #9
  Mar 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha...
   
 10. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #10
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kama nakijua vile hiki chuooooooooo!!!!!
   
Loading...