Sikia ya Mtei na mwl. Nyerere waliposhindwana... Kweli Mwalimu alikua Hashauriki!

Texas Tom.

JF-Expert Member
Jun 8, 2013
510
273
Binafsi nilipata mshawasha wa kusoma kitabu hiki baada ya kuelezwa kwamba Mtei amezungumzia pia mgongano wake wa kifikra na Mwalim Nyerere uliosababisha kujiuzulu kwake nafasi ya Uwaziri wa Fedha. Hivyo basi, badala ya kufuata mfululizo wa sura, nilirukia sura ya 17(Events Leading My Resignation). Unajua kilichotokea?

Ngoja nikuonjeshe nilichokisoma kidogo: Akiambatana na wataalam wa shirika la Fedha Duniani (IMF), Mtei (wakati huo waziri wa fedha) alimtembelea Mwalimu Nyerere nyumbani kwake msasani kujadili hali ya uchumi wa Tanzania. Katika mazungumzo hayo, wataalam wa IMF walimshauri Mwalimu kuongeza ufanisi wa mashirika ya umma na kushusha thamani ya shilingi (Devaluation)!

Mwalimu alionekana kuchukizwa na ushauri wa wageni wa IMF..aliwajibu kwamba yuko tayari kuongeza ufanisi wa Mashirika ya umma kwa wakati na utaratibu autakao! Kuhusu kushusha thamani ya shilingi, aliwajibu kuwa kamwe hataruhusu jambo hilo ambalo alilimithilisha na kuiruhusu serikali yake iongozwe toka Washington!. Baada ya kueleza hayo alinyanyuka kwa hasira na kuwaacha wageni wametunduwaa. Mtei alimfuata kwenye veranda inayotazama baharini alikosimama. Mwalimu alimueleza mtei kwa mkato kuwa awaeleze wageni warudi kwao upesi! Usiku wa siku ile, Mtei hakulala kabisa kutokana na mawazo!

Aliwaza migongano yake na Mwalimu kuhusu masuala ya kisera na uendeshaji wa wizara. Kesho yake, alikata shauri kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri! Kwa vile ilikuwa wikiendi, aliamua kuandika barua yake kwa mkono! Hakuwa tayari kusubiri hata jumatatu ifike. Alipomaliza kuandika barua yake tu, alipokea simu kutoka kwa Waziri wa Kilimo Samweli Malechela kwamba Mwalimu alitaka kuzungumza nao.

Baada ya mazungumzo ambayo yalihusu utaifishaji wa kiwanda cha TPC, Mtei alipokea barua kutoka kwa sekretari wa Rais. Kabla ya kuisoma barua ya Rais, naye akawasilisha barua yake ya kujiuzulu. Alivyoisoma barua aliyopewa, ndipo alipogundua kwamba amefukuzwa uwaziri. Mwalimu alitoa sababu mbili; mosi, ni kile Mwalimu alichokiita kuiruhusu wizara iendeshe toka Washington.

Sababu ya pili ni kile ambacho Mwalimu alisema ni kushindwa kwa Mtei kuwaondosha mapema wageni wa IMF kama alivyoagiza. Baada ya kuisoma barua ya Mtei, Mwalimu aliruhusu taarifa kwa umma iwe kwamba Mtei alijiuzuru na si kufukuzwa. Licha ya tofauti zao, Mwalimu aliendelea kumtumia Mtei kwenye maeneo kadhaa. Kwa mfano, mwaka 1982 Mwalimu alimteua Mtei kuwa mwakilishi wa Tanzania IMF…
 
kama ulikisoma kitabu vizuri utajua maana ya maadili ya wazeeaaaaaa;hakuna hata sehemu moja ametumia lugha ya matusi au ubabe dhidi ya MWALIMU NYERERE
 
Baada ya kueleza hayo alinyanyuka kwa hasira na kuwaacha wageni wametunduwaa!!! yaani hapo ni kama namuona nyerere live alivyokunja ndita.
 
Ngoja nikusaidie kuifanyia Editing hii Thread yako lakini naomba usikasirike!

Binafsi nilipata mshawasha wa kusoma kitabu hiki baada ya kuelezwa kwamba Mtei amezungumzia pia mgongano wake wa kifikra na Mwalim Nyerere uliosababisha kujiuzulu kwake nafasi ya Uwaziri wa Fedha. Hivyo basi, badala ya kufuata mfululizo wa sura, nilirukia sura ya 17(Events Leading My Resignation).

Unajua kilichotokea? Ngoja nikuonjeshe nilichokisoma kidogo: Akiambatana na wataalam wa shirika la Fedha Duniani (IMF), Mtei (wakati huo waziri wa fedha) alimtembelea Mwalimu Nyerere nyumbani kwake msasani kujadili hali ya uchumi wa Tanzania. Katika mazungumzo hayo, wataalam wa IMF walimshauri Mwalimu kuongeza ufanisi wa mashirika ya umma na kushusha thamani ya shilingi (Devaluation)!

Mwalimu alionekana kuchukizwa na ushauri wa wageni wa IMF..aliwajibu kwamba yuko tayari kuongeza ufanisi wa Mashirika ya umma kwa wakati na utaratibu autakao! Kuhusu kushusha thamani ya shilingi, aliwajibu kuwa kamwe hataruhusu jambo hilo ambalo alilimithilisha na kuiruhusu serikali yake iongozwe toka Washington!. Baada ya kueleza hayo alinyanyuka kwa hasira na kuwaacha wageni wametunduwaa.

Mtei alimfuata kwenye veranda inayotazama baharini alikosimama. Mwalimu alimueleza mtei kwa mkato kuwa awaeleze wageni warudi kwao upesi! Usiku wa siku ile, Mtei hakulala kabisa kutokana na mawazo! Aliwaza migongano yake na Mwalimu kuhusu masuala ya kisera na uendeshaji wa wizara. Kesho yake, alikata shauri kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri! Kwa vile ilikuwa wikiendi, aliamua kuandika barua yake kwa mkono! Hakuwa tayari kusubiri hata jumatatu ifike.

Alipomaliza kuandika barua yake tu, alipokea simu kutoka kwa Waziri wa Kilimo Samweli Malechela kwamba Mwalimu alitaka kuzungumza nao. Baada ya mazungumzo ambayo yalihusu utaifishaji wa kiwanda cha TPC, Mtei alipokea barua kutoka kwa sekretari wa Rais. Kabla ya kuisoma barua ya Rais, naye akawasilisha barua yake ya kujiuzulu. Alivyoisoma barua aliyopewa, ndipo alipogundua kwamba amefukuzwa uwaziri. Mwalimu alitoa sababu mbili; mosi, ni kile Mwalimu alichokiita kuiruhusu wizara iendeshe toka Washington.

Sababu ya pili ni kile ambacho Mwalimu alisema ni kushindwa kwa Mtei kuwaondosha mapema wageni wa IMF kama alivyoagiza. Baada ya kuisoma barua ya Mtei, Mwalimu aliruhusu taarifa kwa umma iwe kwamba Mtei alijiuzuru na si kufukuzwa. Licha ya tofauti zao, Mwalimu aliendelea kumtumia Mtei kwenye maeneo kadhaa. Kwa mfano, mwaka 1982 Mwalimu alimteua Mtei kuwa mwakilishi wa Tanzania IMF…












 
mtoa mada.....what have we achieved so far after deceiving those IFM ideas in term of our social, economic and political development
 
Good as a leader that is the good approach.....halafu hao wanaopingana na mawazo ya mwalimu ...can i ask them one question? what have we achieved so far in term of economic development since the time we started deceiving IMF ideas and policy
 
Bwana Texas Tom,

Namheshimu sana na kum-admire mzee Mtei na binafsi ninamuombea chama chake kichukue dola 2015. Lakini katika tukio hili la ku-resign Uwaziri wa fedha amekuwa akinichanganya anavyolisimulia.

Kabla ya kuandika kitabu chake hiki, niliwahi kusoma article moja akisimulia hili tukio na alisema sababu za kujiuzuru ni yeye kugombezwa kwa kuwa-entertain hao wageni wa IMF yaani Bo Karlstrom na wenzake. Kwamba alitakiwa na Nyerere waondoke mara tu ya kutengana Msasani lakini yeye akawa-entertain jijini kwa vinywaji na outings.

Lakini ukikisoma kitabu hiki kwenye ukurasa wa 151 hadi 157 anaonyesha story nzima ya kuelekea Msasani na hadi walivyoondoka na hadi alivyo-resign na hadi magazeti yakatoa habari yake ya kuresign, hakuna anapoonyesha kuwa alifukuzwa au ku-resign kwa sababu ya kuwa entertain hawa akina Bo Karlstrom.


Pia naomba kuanzia hapa, pata mtiririko wa terehe {chronology} ya tukio hili hasa kwa tarehe na siku nilizoweka kwenye RED.
Ukikisoma tena kwenye kurasa hizo inaelekea kwamba ugomvi wa Nyerere na Mtei na wale akina Bo Karlstrom (IMF) uliisha baada ya Nyerere kuwaacha kikaoni akaelekea baharini kama ulivyoeleza.

Mtei anasema hiyo ilikuwa ni November 29, 1979 saa 10:00 jioni, {pg. 151, para. 1, statement. 03}. Sasa hii tarehe kama ndiyo walikutana hapo Msasani basi kalenda zinasema ilikuwa ni Thursday.

Baada ya kikao Mtei anasema kwamba yeye na hao IMF waliondoka Msasani baada ya kuwaeleza kuwa Nyerere kakataa pendekezo la kushusha thamani shilingi.

Kuhusu siku hapa Mtei anasema hivi: {they would be glad to leave for Washington the next day but their bookings were on Saturday and it was difficult to get connection in Europe for such short notice. It was Wednesday and I suggested that they transfer from Kilimanjaro Hotel to the Bahari beach}.

Hebu angali ahap alivyojigonga. Kama walikutana na Nyerere on Thursday, iweje tena igeuke kuwa Wednesday baada ya kumaliza kikao na Nyerere yaani siku moja nyuma ya kikao na Nyerere????!!!

Hapohapo Mtei anaendelea kusema kwamba {The IMF mission left in Saturday morning, the next day wa public holiday}, {pg. 152, para. 2, statement. 01}. . Kalenda zinaonyesha kwamba Saturday hiyo waliyoondoka IMF ilikuwa ni December 01, 1979.

Na siku hiyo walipoondoka hawa IMF, usiku hakulala kama unavyosema na alijiandaa na akaandika barua ya ku-resign ili Jumatatu aiwasilishe kwa Nyerere. Jamatatu inayoonyesha kuwa angewasilisha barua kwa Nyerere baada ya wekend hii ni Monday, December 03, 1979.

Lakini akiwa anapumzia weekenda ya Jumapili, ameshamaliza kuandi resignation(Sunday, December 02, 1979), ndiyo siku alipoitwa yeye na Waziri wa Kilimo, John Malecela wakaenda kujadili suala la serikali kununua kiwanda cha Tanganyika Planting Company (TPC) kilichokuwa kinamilikiwa na wadenmark.

Mtei anasema aliwakatalia Nyerere na Malecela kwamba serikali haina fedha na kwanza ina deni kubw ala nje na alishawaeleza na hata Gavana anajua hivyo. Nyerere na Malecela wakabaki wanaduwaa (page 154, para 1).

Baada ya Nyerere kumaliza kuduwaa, akasisitiza kwamba lazima serikali ikinunue kiwanda hicho. Mtei akamjibu kwamba uamuzi ni wake kama Rais na si wake kama Mtei na hivyo fund atajua yeye (Nyerere) atakakopata. Mtei akaondoka na Malecela naye akaondoka Nyerere akabaki pale Msasani (page 154, para 2).

Kumbuka yote hayo ni Jumapili, December 02, 1979.

Mtei anasema alipotoka Msasani, alikimbia moja kwa moja kumalizia barua yake kwa mkono, hakutaka tena kusubiri Jumatatu kesho yake ichapwe na typewritter. Hapana. Aliona a-submite dakika hiyohiyo. Akamaliza kuandika. Akaamua kurudi Msasani kumpa Nyerere kwa mkono wake.

Wakati anaingia kwenye gari ndipo akakutana na Batao mmoja wa masekretary wa Nyerere amemletea barua. Kumbe inaelea kuwa Mtei alipoondoka Msanani wote Nyerere na Mtei walikimbilia kuandika barua. Ya Nyerere kumfukuza Mtei na Mtei ku-resign. Mtei akaiweka pembeni kwenye kochi na hakuisoma, kwa sababu alipewa nje ya jengo. Akaendesha moja kwa moja hadi Msasani akampa Nyerere resignation letter.

Nyerere akamwuliza kama alipata ya kwake akasema amepata na hajazsoma hajui kimeandika nini mle. Nyerere akamruhusu resignation yake na papohapo akamwita Paul Sozingwa aite waandishi awatangazie kwamba Mtei kajiuzulu.

Habari zikatangazwa jioni. Hivyo, kwa mujibu wa haya maelezo yake ni kwamba Mtei ali-submit resignation Jumapili, December 02, 1979, na Redio Tanzania ikatangaza jioni hiyo.

Hivyo, ukiulizwa kwamba Mtei ali-resign lini, utataja tarehe hii Jumapili, December 02, 1979.

Lakini ona sasa mwenye anavyoeleza tena kwenye ukurasa wa 156 para, 1, statement 03. Hapa anasema kwamba habari za kuatngazwa ku-resign kwake zilijaza magazeti yote ya December 01, 1979!.

Mimi hapa ndipo liponiacha hoi, kwani hiyo December 01, 1979, tumeshona kwamba ilikuwa ni Jumamosi yaani siku walipoondoka wale maafisa wa IMF kwa ndege kwenda Washington, ambayo usiku wake hakulala vizuri akijiandaa kuandika resignation ili Jumatatu a-resign.

Iweje magazeti yaandike tukio la ku-resin kwa Mtei siku moja kabla ya terehe yenyewe??????!!!!!!

Vilevile mkanganyika wa tarehe ni pale kwenye pg. 152, para 1 aliposema kwamba maafisa hawa baada ya kuonana na Nyerere alikuwa wamepanga kuondoka on Thursday. Lakini Thursday ilikuwa ni November 28, 1979 siku moja kabla hata ya kukutana na Nyerere pale Msasani!

Ndiyo maana ninasema, sijui ni kwa sababu gani Mtei amechanganya hivi tarehe hadi kwa mfuatiliaji mzuri linamchanganya badala ya kumwelewesha!

Hivyo, binafsi nina tatizo sana na masimulizi ya tukio hili kwa ujumla.

JADILINI.

Cc: Kombesana, Swiper, Ndalo, Mzeemwanakijiji
 
Namheshmu sana mwalimu nyerere lakini tatizo lake kuu na ambalo watawala huwa wanaogopa kulisema ni kwamba mwalimu nyerere alikuwa hashauriki alikuwa anajiona Mungu mtu ata Sokoine alishawah kujiuzulu zaid ya mara mbili na mwalmu akawa anamuomba inazmwa kmyakmya kwanza sokoine alkuwa strctly kulko nyerere waliopata kufanya kaz na mwalimu wanasema mwalimu ni mzur ktk kuhamasisha ila si kiongoz imara kama sokoine adi ikafkia mahali wakamsilent sokoine kwa tofaut zao na mwalimu...pia karume na mwalmu walitofautiana kwa sababu nyerere alkuwa hashaurki ni hayo tu,,,,
 
Namheshmu sana mwalimu nyerere lakini tatizo lake kuu na ambalo watawala huwa wanaogopa kulisema ni kwamba mwalimu nyerere alikuwa hashauriki alikuwa anajiona Mungu mtu ata Sokoine alishawah kujiuzulu zaid ya mara mbili na mwalmu akawa anamuomba inazmwa kmyakmya kwanza sokoine alkuwa strctly kulko nyerere waliopata kufanya kaz na mwalimu wanasema mwalimu ni mzur ktk kuhamasisha ila si kiongoz imara kama sokoine adi ikafkia mahali wakamsilent sokoine kwa tofaut zao na mwalimu...pia karume na mwalmu walitofautiana kwa sababu nyerere alkuwa hashaurki ni hayo tu,,,,

Argument yako ya siku haibadilishi mantiki na mtiririko wa story nzima.
 
Namheshmu sana mwalimu nyerere lakini tatizo lake kuu na ambalo watawala huwa wanaogopa kulisema ni kwamba mwalimu nyerere alikuwa hashauriki alikuwa anajiona Mungu mtu ata Sokoine alishawah kujiuzulu zaid ya mara mbili na mwalmu akawa anamuomba inazmwa kmyakmya kwanza sokoine alkuwa strctly kulko nyerere waliopata kufanya kaz na mwalimu wanasema mwalimu ni mzur ktk kuhamasisha ila si kiongoz imara kama sokoine adi ikafkia mahali wakamsilent sokoine kwa tofaut zao na mwalimu...pia karume na mwalmu walitofautiana kwa sababu nyerere alkuwa hashaurki ni hayo tu,,,,

Sasa ni ushauri gani mzuri ambao alipewa akaukataa? Mtu mzima hukubali tu kiholela kila ushauri uanopewa ili uonekane unashaurika!
 
Yule mzee alikuwa hashauriki, kumlaumu tunapoteza muda bure lakini ametulostisha sana kiukweli.
 
Namheshmu sana mwalimu nyerere lakini tatizo lake kuu na ambalo watawala huwa wanaogopa kulisema ni kwamba mwalimu nyerere alikuwa hashauriki alikuwa anajiona Mungu mtu ata Sokoine alishawah kujiuzulu zaid ya mara mbili na mwalmu akawa anamuomba inazmwa kmyakmya kwanza sokoine alkuwa strctly kulko nyerere waliopata kufanya kaz na mwalimu wanasema mwalimu ni mzur ktk kuhamasisha ila si kiongoz imara kama sokoine adi ikafkia mahali wakamsilent sokoine kwa tofaut zao na mwalimu...pia karume na mwalmu walitofautiana kwa sababu nyerere alkuwa hashaurki ni hayo tu,,,,

Sokoine hakuwahi kujiuzulu kwa sababu ya kutofautiana na Nyerere. Kama kuna mtu aliyekuwa karibu kikazi na Nyerere alikuwa ni Sokoine. Alijiuzulu kwa ajili ya matibabu na pia fursa ya kujiendeleza kielimu. That is a fact. Lete jingine.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom