Texas Tom.
JF-Expert Member
- Jun 8, 2013
- 510
- 273
Binafsi nilipata mshawasha wa kusoma kitabu hiki baada ya kuelezwa kwamba Mtei amezungumzia pia mgongano wake wa kifikra na Mwalim Nyerere uliosababisha kujiuzulu kwake nafasi ya Uwaziri wa Fedha. Hivyo basi, badala ya kufuata mfululizo wa sura, nilirukia sura ya 17(Events Leading My Resignation). Unajua kilichotokea?
Ngoja nikuonjeshe nilichokisoma kidogo: Akiambatana na wataalam wa shirika la Fedha Duniani (IMF), Mtei (wakati huo waziri wa fedha) alimtembelea Mwalimu Nyerere nyumbani kwake msasani kujadili hali ya uchumi wa Tanzania. Katika mazungumzo hayo, wataalam wa IMF walimshauri Mwalimu kuongeza ufanisi wa mashirika ya umma na kushusha thamani ya shilingi (Devaluation)!
Mwalimu alionekana kuchukizwa na ushauri wa wageni wa IMF..aliwajibu kwamba yuko tayari kuongeza ufanisi wa Mashirika ya umma kwa wakati na utaratibu autakao! Kuhusu kushusha thamani ya shilingi, aliwajibu kuwa kamwe hataruhusu jambo hilo ambalo alilimithilisha na kuiruhusu serikali yake iongozwe toka Washington!. Baada ya kueleza hayo alinyanyuka kwa hasira na kuwaacha wageni wametunduwaa. Mtei alimfuata kwenye veranda inayotazama baharini alikosimama. Mwalimu alimueleza mtei kwa mkato kuwa awaeleze wageni warudi kwao upesi! Usiku wa siku ile, Mtei hakulala kabisa kutokana na mawazo!
Aliwaza migongano yake na Mwalimu kuhusu masuala ya kisera na uendeshaji wa wizara. Kesho yake, alikata shauri kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri! Kwa vile ilikuwa wikiendi, aliamua kuandika barua yake kwa mkono! Hakuwa tayari kusubiri hata jumatatu ifike. Alipomaliza kuandika barua yake tu, alipokea simu kutoka kwa Waziri wa Kilimo Samweli Malechela kwamba Mwalimu alitaka kuzungumza nao.
Baada ya mazungumzo ambayo yalihusu utaifishaji wa kiwanda cha TPC, Mtei alipokea barua kutoka kwa sekretari wa Rais. Kabla ya kuisoma barua ya Rais, naye akawasilisha barua yake ya kujiuzulu. Alivyoisoma barua aliyopewa, ndipo alipogundua kwamba amefukuzwa uwaziri. Mwalimu alitoa sababu mbili; mosi, ni kile Mwalimu alichokiita kuiruhusu wizara iendeshe toka Washington.
Sababu ya pili ni kile ambacho Mwalimu alisema ni kushindwa kwa Mtei kuwaondosha mapema wageni wa IMF kama alivyoagiza. Baada ya kuisoma barua ya Mtei, Mwalimu aliruhusu taarifa kwa umma iwe kwamba Mtei alijiuzuru na si kufukuzwa. Licha ya tofauti zao, Mwalimu aliendelea kumtumia Mtei kwenye maeneo kadhaa. Kwa mfano, mwaka 1982 Mwalimu alimteua Mtei kuwa mwakilishi wa Tanzania IMF