Sikia swali lake ,Kama kweli CCM haipendwi, inashindaje chaguzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sikia swali lake ,Kama kweli CCM haipendwi, inashindaje chaguzi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Dec 22, 2011.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Na Abdul Mitumba
  21st December 2011
  Ukipita katika mikoa, wilaya na vijiji mbalimbali nchini na ukabahatika kuzungumza na watu wa kada tofauti, kauli utakazosikia zikisemwa ni watu kwamba hawakipendi Chama cha Mapinduzi (CCM) kinachotawala nchi wakidai kinachangia maisha ya walio wengi kuwa magumu na duni.

  Eti watu wadai kuwa ukitaka kujua kama CCM haipendwi na wengi, angalia hata katika matumizi ya vipeperushi vyenye rangi ya chama hicho katika magari ya umma na yale binafsi yamepungua huku baadhi ya watu waliokuwa wakipeperusha bendera katika maskani nyingi pia wanapungua.

  Achilia mbali katika maeneo hayo, hata matumizi ya nguo zikiwemo skafu, khanga, mashati na kofia za chama hicho pia zimeanza kuadimika mitaani ulinganisha na ilivyokuwa miaka mitano nyuma.
  Wanadai kuwa, hapo kabla watu waliona fahari kufaa nguo zenye nembo ya CCM na kupita mitaani au katika shughuli zao tofauti na sasa ambapo sehemu kubwa ya wanaovaa wanasubiri sherehe za chama au jumuiya zake au ni wale viongozi tena wa ngazi za matawi.

  Haieleweki kama hizo ndiyo dalili za watu kuichukia CCM au hawana nguo za kutosha kuvaa ama wamekuwa makini kuvaa nguo hizo zenye nembo ya CCM kwa kuzingatia siku maalum tu kama ilivyokusudiwa.
  Wakati ule ukipita katika maeneo mbalimbali nchini, utaona bendera za CCM zikipepea na ilifika wakati hata watu wasio waaminifu walitumia bendera hizo kama kivuri cha kufanya maovu.
  Lakini wakati huu hata bendera za CCM zinazopeperushwa zimeanza kupungua na kuonyesha hofu kuwa huenda madai yanayotolewa kuwa imeanza kuchukiwa yanaweza kuwa kweli.

  Wakati hayo yakiendelea, takwimu zinaonyesha kuwa badi CCM inaongoza kwa kufanya vizuri katika chaguzi nyingi zikiwemo za udiwani, ubunge na uraisi.
  Hata katika ngazi za mitaa, vitongoji na vijiji ambako wenyeviti wa serikali na wajumbe wao huchaguliwa na kwa kupigiwa kura, ambapo serikali kupitia wagombea wake wa CCM wengi wameshinda.

  Takwimu za karibuni kabisa zinaonyesha kuwa katika zaidi ya robo tatu ya kata zote Tanzania Bara, wagombea wa udiwani kutoka CCM wameshinda na kupata uhalali wa kikatiba kuongoza halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji.
  Hapa ndipo swali la kama kweli CCM haipendwi na wengi, inawezaje kushinda karibu katika kila nafasi zinazojitokeza za uchaguzi katika ngazi mbalimbali hapa nchini!
  Au hiyo ndiyo moja ya sababu zinazotajwa kwamba kuna malalamiko ya kuibiwa au kuharibika kwa kura nyingi wakati wa uchaguzi.

  Baadhi ya wanasiasa wanasema ni kweli CCM haikubaliki zaidi katika maeneo ya mijini lakini imeendelea kukubalika vijijini ambako takwimu zinaonyesha ndiko Watanzania wengi hadi kufikia theluthi mbili ya watu wote wanaishi.
  Ndiyo maana vyama vya upinzani vimeendelea kufanya vizuri maeneo ya mijini hasa katika majiji ya Dar es Salaam, Arusha, Mbeya na Mwanza ambako Chama cha Demokrasia na Maendeleo kishinda karibu kila ngazi za uongozi.

  Mfano Chadema imeshinda jimbo la Mbeya mjini, Arusha mjini, Moshi mjini, majimbo mawili ya Dar es Salaam, Iringa mjini, majimbo yote ya Mwanza mjini, Musoma mjini, huku Chama cha Wananchi (CUF) nacho kikishinda jimbo moja la Lindi mjini.
  Huu ni ushahidi kuwa, wapinzani wanafanya vizuri majibo, kata na mitaa ya mijini ambako ni wazi hakuna watu wengi kulinganisha na vijijini ambako CCM imekuwa ikizoa kura nyingi.
  Kwa maana nyingine ni kwamba siyo kweli kuwa CCM haikubaliki bali inakubalika na kuaminiwa na wengi wanaishio vijijini huku wapinzani wakiwika mijini.

  Historia ya siasa duniani inaonyesha kuwa, mageuzi huwa yanaanza mijini na kusambaa hadi mikoani, wilayani hadi vijijini hivyo kuonyesha ni kwa kiasi gani CCM ina kazi muhimu ya kufanya mbele ya uso wa wapenzi wake ili kikubalike kila pembe.
  Pia hii ni changamoto kwa wapinzani ambao kila kukicha wanalalamikia kuwa wanaibiwa kura wakati ukweli ni kwamba hawakubaliki zaidi vijijini ambako ndiko waliko wapiga kura wengi.
  Kuimarika kwa CCM na wapinzani kutaimarisha siasa hivyo kuchangia kukua kwa uchumi hasa ikizingatiwa kuwa siasa ni uchumi.
  0785 (977676) 0713
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kwani kibaka ni lazima apore simu tu?
   
Loading...