Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,013
- 1,634
Miaka minne nyuma niliamua kuacha kazi na kujitosa rasmi kwenye kilimo, ufugaji wa kuku, kupindi hicho nilikua nachukua mshahara 400,000 ukitoa makato mengine ilikua inabaki around kwenye 350000.
Niliamua kujitesa kwa mshahara huo nikawa na save na kuwekeza kwenye kilimo cha mahindi na machungwa na pia nilikuwa najishugulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji, baada ya kuingia kwenye ndoa niliona tu huko mbeleni maisha yatakua magumu sana kama nitaendelea na hii kazi yangu.
Nikachukua maamuzi magumu ya kuacha kazi na pia nikaua biashara ya ufugaji wa kuku na kufungua biashara ya uwakala wa mitandao ya simu.
Nilipata changamoto nyingi za kukimbiwa na marafiki na ndugu hawakunielewa, na kupunguza ukaribu kwangu kwani waliniona nitakua mzigo kwao.
Nilimueleza mke wangu umuhimu wa haya maamuzi yangu alinielewa na kuniunga mkono. Sasa ni miaka minne imepita tokea nichukue maamuzi magumu.
Wale wenzangu ambao wapo kazini naambiwa mshahara umefikia 450,000 kabla ya makato lakini mimi binafsi mshahara huo usingenitosha kwa maisha ya sasa.
MAFANIKIO
~ Biashara ya huduma za kifedha inaniingizia hicho kiwango cha Mshahara au zaidi.
~ Kilimo cha machungwa now kinaniingizia mpaka milioni 4 kwa mwaka na kitaongezeka mbeleni.
~ Kilimo cha mahindi mwaka jana kiliniingizia milioni 2 mwaka huu nimejipanga zaidi.
HITIMISHO
Ukitaka kufanya yako fanya usikatishwe tamaa na mtu, mimi kwa uwezo wa Mungu naiona kesho yangu nzuri.