Sijui nini kimetokea sasa hivi wasanii wamekazana kuimba kuhusu ngono

1. Walianza kuhamasisha upendo
2. Wakaanza kushikana mikono
3. Wakaanza kukumbatiana
4. Wakapelekana sebureni
5. Wakaingizana chumbani
7. Sasa wanaimba ya kitandani

Hawajaishia kuyatamka tu bali hadi kuyatenda na kutuonesha kwenye videos zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga amejibu vyema, wanacheza na mahitaji yetu.
Akili za kiafrika zimejaa ngono 90%
JK alisema bungeni...ukitaka kula liwa kidogo.
Unajua kwanini wabunge wote walicheka?
Sababu walitafsiri KINGONONGONO

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo si soko, tatizo ni wafanyabiashara ikichangiwa na media. Sanaa na media zinao uwezo mkubwa wa kuiunda jamii iwe ya namna gani!
 
Nyakati hazifanani YES lakini hao wanaosikika sababu kubwa ni monopoly ya soko waliyofanikiwa kuipata. Mtu ndio ameteka SOCIAL NETWORK, ana MEDIA HOUSE na Ndiye PROMOTER MUANDAAJI wa MATAMASHA anashindwaje KUPUSH UJINGA wake kwenye VICHWA VYA WATU?

Ila ngoma kali zipo nyingi tu ila hazipewi nafasi.

Listen

Umeandika jambo kubwa sana ambalo wengi wao wanalipuuzia mzigo wa lawama wanamtwisha raia msikilizaji.
 
Nyakati hazifanani mkuu. Wanaimba kutokana na mahitaji ya wakati. Hawa jamaa wanajua soko lao vinginevyo wangeacha kuimba. Hapa tulipofikia bado sana, omba Mungu akupe uhai ifikapo 2030 hali itakuwa tete zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ye kaona tu music hajaona wadada wanatembea robo tatu uchi?? Tukifika huo mwaka kila kitu hadharani
 
Mkuu kcamp ni kweli soko la muziki linategemea concept ya demand and supply, lkn kiuhalisia demand ambayo ndiyo hadhira inategemea sana suppliers ambao ndiyo wasanii hapa namaanisha huwezi ku demand kitu ambacho hakipo sokoni, so wasanii wana uwezo mkubwa wa kubadilisha akili ya hadhira hasa wasanii wakubwa mana hawa wadogo wanaangalia nn wakubwa wanafanya, kwa mfano kuna mziki umeibuka kwa ss mziki wa singeli japo ulikuwepo kwa mda kdg lkn ulikuwa unaonekana km mziki wa kihuni usio na maadili na ni wa uswahilini, lkn ghafla umeanza kupewa credibility baada ya wasanii wakubwa kuanza kuuimba, hii inaonesha nguvu ya ushawishi waliyonayo wasanii wakubwa na pengine niseme kitu kimoja, ni kwamba huu mziki wa matusi ya wazi wazi muasisi ni Diamond pamoja na kundi lake la WCB japo ni kweli matusi yalikuwepo huko nyuma lakini c kwa kiwango cha ss, huko nyuma ilikuwa nyimbo ikiwa na tusi hata kwny redio stesheni ulikuwa unafinywa kimtindo lkn kwa ss imeshaonekana ni kitu cha kawaida maana utafinya nyimbo ngp ilihali asilimia kubwa ya nyimbo za ss zinafanana, mm mwenyewe ni mpnz wa nyimbo za Mondi na kundi zima la WCB na huu ndio ukweli wenyewe kwmb kupitia wao wasanii wengine wakaona hii ndio direction na mpk ss tunapoelekea ni kubaya zaidi km hii perception ya wasanii wanaimba kulingana na uhitaji itaendelea kugonga ktk vichwa vya wasanii.

Recommendation

Wasanii wakubwa wanapaswa kujuwa wajibu wao kwmb mbali na kuburudisha pia waangalie namna ya kutoharibu maadili yaliyopo katika jamii kwn wao wanaweza kuamua ni mziki gn wa kuimba na hadhira itasikiliza na kupenda itake isitake
Wengi wao wanadhani uwingi wa wimbi fulani kwenye issues za music wanadhani raia kupenda aina hii ya music ndiyo kitu wanachokihitaji kwa sasa! Wanasahau kuna medias, kuna wasanii wakubwa ambao wana ushawishi mkubwa nao wanao uwezo wa kuiunda jamii iwe ya namna gani!

Media kubwa + wasanii wakubwa wana uwezo Mkubwa sana wa kubadilisha soko la mziki.
 
Shida ni media outlets ndizo zinatufikisha hapa.

Media kuanzia online hadi hizi radio na television channels.... Hizi ndizo huwa zina mobilize upuuzi na wafuasi huwa wanaiga tu bila kujua madhara....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu wasanii wametoka kutukana kwa mafumbo siku hizi wanatukana live kabisa hata mtoto anajua, mtu anaimba eti "gusanisha nyama kwa nyama" asa ndio nini, yaani huu upupu ukiachwa uendelee itafika kipindi utasikia "ingiza ub...o vua chupi kum.. mnato" yaani ni nonesense kabisa mziki wa sasa, hatukatai kila zama zina mziki wake ila tusifike kipindi tukaanza kuu sodomize mziki wetu.
Umesha sodomiziwa kitaaamboooooh lol

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Tembo kutwa nadindisha mkonga" , "mtoto mwaga maji nimwage mbolea". Naomba aliye karibu na Harmonize amuulize maana ya haya aliyoyaimba kwenye "acha lizame" aliyoshirikishwa na Nandy.
😂😂😂😂😂
 
Wamekuwa wengi mno na kila mtu anaimba mapenzi na mapenzi hayana jipya masikioni na machoni pa watu.... Roughly ni kwamba wamefika ukomo wa kufikiria
 
Mjomba wangu nimemsikia anaimba huu wimbo wa Nandy na Harmonize.."unapenda vya giza giza kama hujanizoea...shamba mwaga maji nimwage mbolea.." na nndio kwanza ana miaka 8. Aisee!
 
"Usijidanganye umemkamataa mtoto wa mujini magoli mengi samatta hata uende chumvini"

"Sio tu unakunywa pombe unajua analipa nani,twende nikakupe guu la ng'ombe ukaugulie nyumbani"

Harmonize -one night stand
"Tembo kutwa nadindisha mkonga" , "mtoto mwaga maji nimwage mbolea". Naomba aliye karibu na Harmonize amuulize maana ya haya aliyoyaimba kwenye "acha lizame" aliyoshirikishwa na Nandy.
 
"Usijidanganye umemkamataa mtoto wa mujini magoli mengi samatta hata uende chumvini"

"Sio tu unakunywa pombe unajua analipa nani,twende nikakupe guu la ng'ombe ukaugulie nyumbani"

Harmonize -one night stand
Aisee! Huyu Harmonize kweli amekuwa mwanafunzi mzuri wa boss wake wa zamani Diamond. Hatarii. Ngoja niusikilize huu mdundo.
 
"Tembo kutwa nadindisha mkonga" , "mtoto mwaga maji nimwage mbolea". Naomba aliye karibu na Harmonize amuulize maana ya haya aliyoyaimba kwenye "acha lizame" aliyoshirikishwa na Nandy.
Kwa mashairi kama haya ndio maana Harmonize anadai tuzo
 
Miaka ya nyuma nyimbo zilikuwa zikitoa ujumbe wa mapenzi (zilikuwa zikiitwa nyimbo za mapenzi) kwa mfano:

TID ft Jay Dee - Understanding
TID - Asha
Jaydee ft Matonya - Anita
TID - Zeze
Dully Sykes - Hunifahamu
TID - Nyota Yangu
Jaydee ft Blue - Wangu
PNC ft Mlue - Mbona
Ray C - Unaifuata Nini
Q chief - Uhali Gani n.k


Sijui nini kimetokea sasa hivi wasanii wamekazana kuimba kuhusu ngono in such a way it is too much .sijui kama wanajua kwamba kuna kizazi kinawaangalia na kinawaiga yaan sasa hivi ni mwendo wa "kusafisha mtaro" mara utasikia "Tango" mara sijui "Uno" mara hujakaa vizuri "Tekenya".

Baadhi ya hayo masotojo

Maua sama - Niteke
Rayvanyy ft Lavalava - Tekenya
Diamond - Jeje
Nandy - Na Nusu
Dimpoz ft nandy - Kata
Harmonize - Uno
Diamond - Gere

Na nyingine nyingi mnaweza mkaongezea.

Ushauri: Hao BASATA naona wanadeal na product ya tatizo badala ya kudeal na tatizo lenyewe yaani wanashindwa kuwaita wasanii wakawaelekeza potential waliyo nayo na jinsi wanavyoitumia kupotosha kizazi na jinnsi ya kuitumia kwa usahihi. Wao wamekalia kufungia nyimbo tu halafu wiki mbili zikiisha wanamfungulia mtu anaendelea na utumbo uleule.
umesahau Acha Lizame
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom