Sijui neno hili lilitoka wapi?

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Kwenye Kiswahili hakuna neno "kupelekea".
Hili ni moja ya maneno yaliyopata mashiko siku hizi
lakini ukweli ni kuwa hiyo ni "broken language".

Mfano:
1. Tatizo hili limepelekea kila mtu kujihoji.
2. Kuchekelewa kumepelekea tumkose.
3. Ajali imepelekea vifo vya watu wawili.
............
Kimsingi, neno sahihi ni "sababisha".

1. Tatizo hili limesababisha kila mtu kujihoji.
2. Kuchekelewa kumesababisha tumkose.
3. Ajali imesababisha vifo vya watu wawili.
 
Kwa nini hilo neno ni lugha iliyovunjika (broken)?
Kwa sababu neno "peleka" na "pelekea" yana maana ya "kufikisha mahali fulani". Kwa mfano:
- Tulipeleka fedha benki.
- Tulimpelekea fedha nyumbani kwake.
...........
Lakini matumizi haya "brocken" hayana lengo la kuongelea "kufikisha" mkuu Jose, bali lengo ni kuongelea "kusababisha".
Sasa, neno "peleka" halina maana ya "sababisha"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom