Sijui,lakini nadhani wanawake wanaweza kutupa majibu juu ya hili ......!!!!!

....usishangae kaka, kwani si ushasikia kitu kinaitwa Open Marriage?
Si unajua zile za U Room Mate chuo? sasa "Mkeo" anakuwa #HouseMate!

.....mtapoamua, anaweza pia kuwa mama wa mtoto/watoto wako...Apart from that
kila mtu na lwake....wakati hauruhusu kabisa kuumizana kichwa miaka ya sasa.

Peace of Mind....
Mkuu haya mambo mhh!!!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Kuna trade off kati ya utajiri na furaha (incuding upendo).

Kuna ktabu nilikuwa nasoma jana kuna familia baada ya mama kuamua kutafuta kazi baada ya kuona maisha ya familia yanakuwa magumu na wenzake wote wanafanya kazi na kuendesha magari ya kifahari huku naye ni msomi mzuri; Mungu akashusha neema nyingine mume cheo kikapanda akawa marketing executive,

Baada ya miaka michache kupita, mtoto wao wa miaka 12; baada ya kutafuta courage ya kusema kwa zaidi ya mwezi (it was tough for her to ask); akamuuliza baba 'Dad do you still love mum?'

Maana familia ilikuwa shagalabagala...mara huyu anakimbiza watoto day care; huyu ana appointment na huyu; hawana muda waliokuwa nao zamani kukaa kama familia...mtoto wa miaka 12 ame notice hizo changes.

Mtunzi anasema na sie tukae chonjo tusije ulizwa same question....(Book: '15 minutes alone with God'...hadithi zote zimetokana na ukweli)
Maana maisha yao yalibadilika completely wote muda hauwatoshi jinsi wanavyosaka shilingi...

Hilo ni gumu sana

Siku hizi mwanamke asiyefanya kazi inaonekana kama sio binadam hivi!
 
Yaani kweli kabisa unasema hii ni akili?????

The whole issue is complicated Eiyer na kuielewa inataka ukae pembeni uangalie uhalisia na si kwa jicho la victim
 
Last edited by a moderator:
Hilo ni gumu sana

Siku hizi mwanamke asiyefanya kazi inaonekana kama sio binadam hivi!

Usisahau pia ukweli kuwa wanaume wanawasimanga na kuwanyanyasa wanawake wasiofanya kazi!
When its his money,his car,his house then its his life and she is just living in it!!! Wanaume wabinafsi sana
 
Binadamu tuko complex sana.

Ningumu kujua binadamu ana hitaji nini.
 
Ni muda sasa nimekua nikijiuliza kuhusiana na hili jambo na kuna wakati nimejikuta naishia kushangaa tu,katika kujiuliza huko niliwahi kuanzisha uzi hapa nikijaribu kupata mawazo ya wnawake kuhusiana na hili

Niliwahi kuanzisha uzi hapa ukihusiana na mwanamke kuwa na mume/boyfriend ambae sio mcharuko[kicheche] lakini pia kipato chake sio kikubwa kiviile lakini kikubwa zaidi ni kuwa mwanaume huyo hajali na wala hamuulizi wala kumchunga mkewe hata akichelewa na sio mbishi pale mwanamke anapokuwa anamwambia kuhusiana na mambo kama vile kuchelewa kurudi,kusafiri kikazi n.k

Nilipata maoni ya wanawake wengi wakisema kuwa watampenda sana mwanaume wa aina hiyo na kumheshimu sana bila kujali hali yake kifedha kwakuwa kile kitendo cha kutokuwa kicheche tu kinatosha kumfanya mwanaume huyo kuwa bora,kifupi waliongea mendi sana

Sasa nimejikuta nashangaa sana baada ya kukagua baadhi ya ndoa zenye wanaume wenye sifa hizo au zinazokaribia kufanana na hizo

Nilishangaa kwasababu karibu ndoa zote 7 nilizozifanyia uchunguzi wa harakaharaka,wanawake hao wanatoka nje ya ndoa,sijajua hasa ni kwanini ila nadhani huenda kuna kitu kimejificha kwenye hilo

Ndio hizo mara nyingi wanaume sio wakali kwa wake zao pindi wachelewapo kurudi kazini,waume hao sio vicheche,yaani kwa kifupi wanaume hao karibu chochote watakachoambiwa na wake zao wao hawana tatizo labda kwenye mambo machache sana

Nilivyokuwa najua mimi ni kuwa wanawake huwapenda sana wananume wanaowasikiliza na kuwaunga mkono hasa kwenye mambo "yao" lakini naona kama nilikuwa najidanganya

Najua idadi hiyo ya ndoa ni chache sana lakini nadhani zinatosha kumshtua yoyote na kupelekea kujiuliza,iweje zote zifanane?Kwanini hakuna tofauti hata moja?

Wanawake wanataka mtu wa aina gani?
Kuna wakati jamaa yangu mmoja aliwahi kiniambia kuwa kama unataka mwanamke akuheshimu mgegede vizuri lakini kuna waliofanya hivyo na wakaambulia vibuti

Kuna wengine wanaamini katika hela lakini tunaona kila siku akina shamba boy wakizisambaratisha ndoa za mabosi wao

Kuna wengine wanadhani kuwa handsome ndio komesha lakini ukweli kila mtu anaujua

Wanataka nini hawa watu?
Hebu kujeni hapa mtueleze!

Hizo 7 ni chache kati ya nyingi na bahati mbaya zote zinafanana lakini kutoka nje ni tabia ya mtu.hata umuache free au umbane sanaaaa akiamua kutoka anatoka tu.wapo wengi wanaoheshimu ndoa zao
 
Nakubali kuwa hiyo ilikuwa extreme case; lakini message bado ina hold...ela ikiwa ndio msingi wa ndoa hiyo inakuwa partnership si ndoa ya mfano...mwanamke anakuwa anakaa na mtu kwenye ndoa ili aweze mantain status; kwa mume anakuwa na mke ili apate huduma muhimu pale anapokosa za mtaani au heshima tu kwenye jamii..

Hilo ni gumu sana

Siku hizi mwanamke asiyefanya kazi inaonekana kama sio binadam hivi!
 
Usisahau pia ukweli kuwa wanaume wanawasimanga na kuwanyanyasa wanawake wasiofanya kazi!
When its his money,his car,his house then its his life and she is just living in it!!! Wanaume wabinafsi sana

Kimsingi huwezi kusahihisha kosa kwa kufanya kosa
Kitendo cha mwanaume kumsimanga mkewe kuhusiana na hela ni kosa
Kitendo cha mwanamke kuacha jukumu lake la kuilea familia na kuiacha bila mwangalizi ili kutafuta fedha anazosimangiwa na mumewe ni kosa pia

Kimaumbile mwanaume ndio anapaswa kuitafutia familia mahitaji yake ya kifedha,mwanamke yeye ni kulinda familia nyumbani na kutawala mamlaka yote ya nyumbani.Kama kuna mwanaume asiyejua hilo hafai kuitwa mume

Kitendo cha mwanaume yoyote kumsimanga mkewe kwa sababu ya fedha ni upu.uzi mkubwa na huyo hafai kuitwa mume pia,lakini tatizo linaanzia kwenu nyie wananwake,ukimpata mwanaume anaekupa heshima na thamani yako utamdharau na kukimbilia huko kwa hao wanaowanyanyasa na kuwasimanga halafu mnakuja kuwalaumu wanaume wote,sijui mkoje!
 
Nakubali kuwa hiyo ilikuwa extreme case; lakini message bado ina hold...ela ikiwa ndio msingi wa ndoa hiyo inakuwa partnership si ndoa ya mfano...mwanamke anakuwa anakaa na mtu kwenye ndoa ili aweze mantain status; kwa mume anakuwa na mke ili apate huduma muhimu pale anapokosa za mtaani au heshima tu kwenye jamii..

I agree fully

Siku hizi wanatamka wazi hapa na mitaani kuwa kama mwananume huna hela usiwasogelee kabisa
Wanaolewa na hao wenye hela bila kujua kitu muhimu kwenye maisha ya binadamu sio hela
Wanatendwa wanakuja kuwalaumu wanaume wote
Sijui hili jinamizi limetokea wapi

Tutakapoishia hata shetani hajui!
 
Hizo 7 ni chache kati ya nyingi na bahati mbaya zote zinafanana lakini kutoka nje ni tabia ya mtu.hata umuache free au umbane sanaaaa akiamua kutoka anatoka tu.wapo wengi wanaoheshimu ndoa zao

Wewe uefanya utafiti gani kuthibitisha kuwa "wapo wengi wanaoheshimu ndoa zao"?
Hao wengi wanasifa zipi?

Kwanini 7 ziwe chache?
Hujiulizi tu kuwa kama kuna ndoa 7 zenye sifa na mambo yanayofanana kwanini kusiwe na ndoa 1000 za namna hiyo zinazofanana?
 
I agree fully

Siku hizi wanatamka wazi hapa na mitaani kuwa kama mwananume huna hela usiwasogelee kabisa
Wanaolewa na hao wenye hela bila kujua kitu muhimu kwenye maisha ya binadamu sio hela
Wanatendwa wanakuja kuwalaumu wanaume wote
Sijui hili jinamizi limetokea wapi

Tutakapoishia hata shetani hajui!

Mkuu wanaume maskini huwa hawawatendi wake/wanawake zao? Ni wenye fedha tu ndiyo watendaji?
 
Kimsingi huwezi kusahihisha kosa kwa kufanya kosa
Kitendo cha mwanaume kumsimanga mkewe kuhusiana na hela ni kosa
Kitendo cha mwanamke kuacha jukumu lake la kuilea familia na kuiacha bila mwangalizi ili kutafuta fedha anazosimangiwa na mumewe ni kosa pia

Kimaumbile mwanaume ndio anapaswa kuitafutia familia mahitaji yake ya kifedha,mwanamke yeye ni kulinda familia nyumbani na kutawala mamlaka yote ya nyumbani.Kama kuna mwanaume asiyejua hilo hafai kuitwa mume

Kitendo cha mwanaume yoyote kumsimanga mkewe kwa sababu ya fedha ni upu.uzi mkubwa na huyo hafai kuitwa mume pia,lakini tatizo linaanzia kwenu nyie wananwake,ukimpata mwanaume anaekupa heshima na thamani yako utamdharau na kukimbilia huko kwa hao wanaowanyanyasa na kuwasimanga halafu mnakuja kuwalaumu wanaume wote,sijui mkoje!

Ulishaambiwa na mshangiaji mmoja ke wanataka sifa zote ndiyo watulie... sasa wewe una 5 umemiss 3, je huoni ni sababu za kumfanya partner wako kuchepuka kwa anayezijazilizia hizo 3 ulizozimiss wewe?
 
Ulishaambiwa na mshangiaji mmoja ke wanataka sifa zote ndiyo watulie... sasa wewe una 5 umemiss 3, je huoni ni sababu za kumfanya partner wako kuchepuka kwa anayezijazilizia hizo 3 ulizozimiss wewe?

Unang'ang'ania uende ghorofa ya 3 bila ya kupitia ghorofa ya kwanza na pili

Ni kitu gani kilimfanya akubali kuolewa na mimi at the first place?
Au hayo mapungufu yamekuja kutoka kusikojulikana tu?

Halafu unajua kama kuna mtu mwenye sifa zote hizo duniani?
Na una uhakika kuwa hicho ndio kinawafanya watoke nje ya ndoa?
 
Samahani nadandia fuso mbele! Ukiwa mume ni halali kwa wake zako kutumia fedha za matumizi kuopolea marioos?

Kama umejua unadandia fuso kwa mbele halafu ukaendelea kuidandia utakuwa ni mzima kweli?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom