Sijui kama unajua au hujui kuwa sensa imefeli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijui kama unajua au hujui kuwa sensa imefeli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Simba Mkali, Aug 30, 2012.

 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Sina hata haja ya kutoa maelezo mengi, leo Ijumaa ndiyo mwisho wa Sensa na kwa jinsi ambavyo nimeshuhudia zoezi lenyewe lilivyopelekwa pelekwa kwa vyovyote vile limefeli, tungoje idadi ya uongo ya uongo. lakini nadhani kuna fundisho tutakuwa tumelipata. Viongozi wa serikali wanatakiwa kujenga mpango makini wa kudumu katika kufanikisha zoezi hilo kilahisi next time.
   
 2. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,422
  Likes Received: 393
  Trophy Points: 180
  mimi hapa bado sijahesabiwa!
   
 3. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  mimi hawajafika kwangu na kesho mwisho!!
   
 4. M

  Mchaga HD Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sisi mtaani kwetu nyumba kama 4 hawajahesabiwa..
   
 5. c

  christmas JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,603
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  wizi mtupu, wanapika data vyumbani kwao
   
 6. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mapango makini si uuelezee au unabwabwaja tu. Kusema limefeli kabisa siyo sawa ila nijuavyo takwimu za idadi ya watu zitakazotolewa siyo sahihi kwa sababu:
  1. Maandalizi yameingiliwa na ujanja ujanja na rushwa kwa watendaji wa zoezi ngazi za mkoa na wilaya
  2. Watu wa sensa wamepita majumbani mwa watu saa za kazi na kusababisha taarifa za majumbani kutolewa na wasichana wa kazi including nyumbani kwangu.
   
 7. S

  Sangomwile JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 17, 2012
  Messages: 3,091
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Leo ni ijumaa?
   
 8. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  ndo nashanga.....
   
 9. SIM

  SIM JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 1,639
  Likes Received: 792
  Trophy Points: 280
  a,k.a chachandu
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mie sijahesabiwa mpaka sasa!!
   
 11. Sakijoli

  Sakijoli Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sensa hii aisee magumashi kibao, mtaani kwetu jamaa wamekuja j2 tu hawajatokea tena, nikachukua hatua za kwenda kwa Mjumbe nikareport ili nihasabiwe nikaambiwa nitapigiwa simu. Office za serikali za mtaa nao wananiambia nisiwe na wasi nitulie nyumbani wanakuaja. Sasa sijui niende makao makuu wakanihesabu?
   
 12. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Mimi nimehesabiwa kwa simu maana walipofika nyumbani nilikuwa kazini wakapata namba yangu ya simu wakanipigia. Sijui kama huu utaratibu unaruhusiwa na hauwezi kuleta kasoro.
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mmmmhhhh na wasiwasi na uwepo wako hapa dunia leo ni alhamisi au ijumaa.. fafanua hilo ndio tukuelewe...
   
 14. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Usiwe na wasiwasi, mkuu miye ni binaadamu naweza kuchanganya mambo, leo Alhamisi kesho Ijumaa. nashukuru kwa kunikumbusha.
   
 15. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Unajua maana yakubwabwaja? kama wewe ni mgeni, wana JF tumeongea mengi sana kuhusu serikali ilichotakiwa kufanya, pia kila sehemu wenye akili wametoa ushauri wa maana. sikuona sababu ya kurdia hapa. asante kwa kunielewa.
   
 16. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mi ni kama sikuhesabiwa tu, mtu mwenyewe aliyekuwa akituhesabu licha ya kutokuwa na kitambulisho,yunifom pia taarifa zetu alikuwa akizirekodi kwenye kinotbuku kama fundi mwashi akihesabu idadi ya mbao toka kwenye fuso
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  wakuu nipo dar,na bado sijahesabiwa mpaka sasa
   
 18. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  SENSA MWISHO JUMAMOSI... Mnakuwa kama huwa Hamsikilizi TV na Radio.. Sensa ni Siku 7, acheni kukurupuka

  Karani amepangiwa Eneo lenye kaya Zaidi ya 150 halafu mabalozi hawatoi Ushirikiano unadhani atazimaliza kwa siku mbili au Tatu?? Kaya zenyewe zina watu zaidi ya Nane na Anatakiwa kuuliza Maswali 37 au 62 Atamaliza Leo.

  Vumilieni Wanakuja si kuja kulalamika JF wakati mda hata wa Sensa kuisha hamuujui

  UKIONA UNA KAZI SANA MWACHIE HAYA MFANYAKAZI AU MTU MZIMA HAPO HOME

  * Majina ya Wanakaya waliolala jumamosi kuamkia jumapili mkiwamo na Nyie

  *Uhusiano na wanakaya hao[mke,mme,ndugu,rafiki au watoto]

  * Umri wa wanakaya
  *Viwango vya Elimu

  *Kama wana-vyeti vya kuzaliwa au Lah

  *Idadi ya Mifugo[kuku,ng'ombe,Kondoo na mbuzi]

  *Kama wewe na wanakaya wengine ni Wanachama wa Mifugo ya Jamii au Lah

  *Kama kuna Mlemavu yoyote[wa kuöna,kusikia,albino,kutembea]
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  tatizo la kumnya wanzuki iliyokaa kwa wiki moja...
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,825
  Trophy Points: 280
  jamani siku saba za sensa zinaisha tarehe 2 kwahiyo tujipe moyo tutahesabiwa manake mim na familia yangu hatujahesabiwa nikahisi labda kwakua kwang ni mbal sana na majirani nikaenda kwa mjumbe wa nyumba kumi akasema watakuja tu nisubiri hivyo naendelea kusubiri.
   
Loading...