Sijui kama siku hizi zipo hizi

swanga

Member
May 21, 2012
79
17
[h=5]SIJUI KAMA SIKU HIZI ZIPO HIZI[/h][h=5]1. Kupakwa GV kwenye kidonda
2. Kung'olewa jino kwa uzi
3. Ubwabwa kupikwa j2 tu
4. Kidonda kuwekwa unga wa 'rangi mbili'
5. Kupamba kadi sebuleni
6. Ukumbi wa sherehe kupambwa kwa toilet paper
7. Kunyolewa na mkasi
8. Kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
9. Kwenda kuangalia sinema za Ukimwi na Lishe sokoni
10. Ku rewind kanda kwa peni
11. Ndala kuchemshwa ili zisiishe
12. Kucheza umeshikilia kaptula sababu mpira umekatika
13. Kuchonga penseli na meno
14. Kukata ndala, ati ni kifutio
15. Kunyolewa msalaba shuleni kisa nywele ndefu
16.Kwenda shuleni na tofali na kidumu cha maji

Wewe unakumbuka nini...?

[/h]
 
1.Kuvaa kaptula shuleni 2. Kuninginiza engachifu nyuma ya mfuko wa suruali ili ionekane.
 
-kumiliki vidonda kama vi5 hivi kwa wiki
-Kusingizia unaumwa siku za usingizi mzuri ili usiende skuli
-kupiga picha huku umepakata radio aina ya phillips(sauti safi sauti kubwa)
-Kupiga picha kwa kamera za filim
-Kuchonga kabati kubwa la tv lenye kufuli na kuliweka sebuleni
-kupaka mafuta ya rays na shant
-kuitikia salam'' ayeya''''dole tupu''
-Barua za mapenzi zenye picha za mikuki inatoboa mioyo
 
kuchoma nywele na kuweka kalkit
walikua wanapika bulga (chakula kama uji wa rangi ya machungwa) sijui unakumbuka?,
kuvaa dangris (jeans pana)
kuvaa viatu vya soli ndefu (nyanza shoes)/viatu vya kuchongoka mbele tuliviita "wanchoma"
na hii sikia wakati vita vya nduli amin wanajeshi walikua wanateremka kwenye meli na maredio makubwa (stereos),nakumbuka mbali sana maisha yalikua poa sana.wasaalam.

 
-kucheza kumbolela nyakati za jioni
-kwa wale mpira wa miguu kucheza "one touch"
-
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom