Sijui kama mwenye nyumba anajua haya wanayofanya wadada wa kazi

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
Wakuu habari iwe nanyi!

Ukisoma kitabu cha Mathayo kwenye biblia kuna hadithi ambayo Yesu Kristo alikuwa akizungumza na wanafunzi wake juu ya Bwana moja aliyetaka kusafiri kisha agawa mali zake (talanta) kwa watumwa wake ili wazisimamie . Lengo la Bwana yule ilikuwa wale watumwa wasimamie zile mali kwa faida ili baadaye aje awalipe sawasawa na kazi zao. Hadithi ni ndefu ila unaweza kusoma mathayo 25:14-30,

Hii mada inaweza kuwa ndefu kidogo na ya kufikirisha hivyo kama huwezi kusoma vitu virefu na kushirikisha akili yako ni bora ukaishia hapa. Ipo nchi moja ya kufikirika ambayo waliamua kukabidhi mamlaka yao na maliz zao kwa mfalme wao ili azisimamie na kwavile mfalme pekee yake hakuwa na uwezo wa kufanya yote hayo , wale wananchi wa nchi ile walimpa mfalme mamlaka ya kuteua watu kumsaidia kusimamia yale aliyokasimiwa na wananchi wa nchi ile. Tatizo moja au kosa kubwa alilolifanya mfalme ni kuchagua wasaidizi wake akidhani wana ueledi au ni waaminifu kumbe haikuwa hivyo kwa wote. Wenye uelewa wa mambo walianza kumshangaa mfalme kwa kuteua watu wasio na sifa stahiki kushika uongozi katika mashirika na maeneo mengine nyeti ya nchi vigezo vikiwa ni kujuana na mfalme , wapambe wa mfalme, kugombea na kisha kushindwa katika kura za maoni katika chama cha mfalme, kumsifia sana mfalme miongoni mwa sifaa kadhaa

Kama mnavyojua masikini akipata matako hulia mbwata, baadhi ya wateule wa mfalme walitolewa kwenye sehemu zao za awali walipokuwa wakiongoza watu wasiozidi 50 wakapewa kuongoza watu 800, waliongoza mtaa wakapewa wilaya , mwalimu mkuu akapewa ukurugenzi, hapa ndipo timbwili lilipoanza. Kwa mfano yuko bwana moja katika nchi ile ya kufikirika alipopewa tu Ukurugenzi akasema hataki watu wazima wote waliokuwa pale alipopewa kusimamia. Akataka kuwafuta kazi wote tatizo hakuwa na hela ya kuwalipa ili waondoke. Bila kujua kwamba hao wazee ndiyo walioweka msingi wa shirika husika, bila kujua kuwa hao wazee ndiyo waliotandaza nyaya kibao chini ya ardhi ambayo hao vijana aliokuwa anawataka hawakujua hizo nyaya zilipo. Huyu bwana akaanza kudhoofisha idara nyeti za shirika kwa kuondoa watu aliyowakuta, akitumia kile kinachoitwa rushwa ya ngono ndani ya miaka miwili karibia mameneja wote wamekuwa wanawake hili si kosa kama wanapatikana kwa merits zao. Huyu bwana amekuwa akihutubia vikao vya wafanyakazi hata masaa sita pekee yake bila hata kuwapa wafanyakazi nafasi ya kuchangia, akitumia lugha ya matusi vitisho na kejeli nyingi ili aweze kuogopwa.

Hali ya mambo ndani ya shirika husika ni mbaya kuliko inavyoweza kuelezwa, akitumia gawio kama kiinimacho kumdanganya bosi wake na wenye nchi yao kwamba hali ya shirika ni nzuri kumbe hali ni mahututi. Badala ya kuweka miradi mipya amebaki kung'oa mitambo huku kupeleka pale yaani mfano akiona hali ni mbaya sehemu A basi anang'oa mitambo sehemu B na kupeleka sehemu A ili kudanganya umma wa nchi ile. Akiwa amejiwekea walinzi wa kutosha , wadada wazuri pembeni anazunguka nchi ya kusadikika kufanya kazi ambazo zingefanywa na wasaidizi wake huko mikoani. Ameshindwa kubadili fursa kibao alizozipata na zilizopa kuongoza shirika vizuri, wafanya kazi wake wamechoka mbaya kutwa nzima kufunga na kujifariji kuwa wanafanya diet kumbe hali zao ni dhoofu bina hali. Magari ya shirika yamekuwa kama screpa hakuna kitu. Ilivyo bahati mbaya bidhaa zinazozalishwa na shirika husika zimetapakaa kwa wazalishaji wengine. Huduma imekuwa mbovu kiasi cha wateja kulalamika kila kukicha ila bosi yeye anakula raha, ushindani wa kupata ajira hamna idara ya rasilimali watu imepigwa ganzi kazi yao ni kugawa tu barua za ajira zinazotoka kwa mkuu .

Kibaya zaidi huyu mtu alijua ataitumia taasisi hii ya watu wa kusadikika kama ngazi ya kupata ubunge bado hajaamini msimamo wa bosi wao wa kuwaonya kuacha nafasi zao walizopewa kushika kwa ajili ya ubunge. Alitaka avuruge mambo ili akimbilie ubunge ila sasa kama kumfia kitamfia mwenyewe. Kama ambavyo bahari haikai na uchafu ndivyo ambavyo pia ukweli haiwezi kufichwa hata ikizibwa mdomo iko siku itapiga kelele na kujulikana kwa wote. Najua kuna siku atashindwa kutoa gawio, kulipa mishahara na hata kuendeleza huduma mbovu zilizopo na hapo ndipo mwenye shamba atamwambia wewe ni mtumwa mbaya na kuagiza akatupwe kunako ziwa la moto. Huyu ni moja tu wa dada wa kazi ninayemjua ila najua wako wengi sana wanakula na kunywa maziwa ya watoto najua siku yao inakuja.

Amani iwe nanyi nyote!
 
UKiwa mwoga wa kuandika thread usije huku JF kutupotezea muda. Hakuna mtu ana interest ya kusoma riways zako ndefu za kimafumbo hapa. Sema azi kwa kifupi ueleweke tujue tatizo ni nini, liko wapi, na nani anahusika. Unaficha uchi na watoto bado unataka?
 
Isaidie nchi ya kusadikika kwa kutaja jina la shirika, vipepeo weusi watakuja kunusanusa, kama ni umbeya basi huyo beki tatu ataendelea na kazi yake, kama ni kweli basi kibarua kitaota nyasi.
 
Itakuwa kuna kaukweli fulani. Wateja wa TTCL wanalalamika sana siku hizi. Nadhani ni suala la muda tu tutajua mbivu na mbichi.
 
Mkajipange kwa upya!mnaandika tamthilia humu JF nani mwenye muda huo?andika kinachokuhusu acha umbeya wa kwenye vijiwe vya akina mama
 
Wakuu habari iwe nanyi!

Ukisoma kitabu cha Mathayo kwenye biblia kuna hadithi ambayo Yesu Kristo alikuwa akizungumza na wanafunzi wake juu ya Bwana moja aliyetaka kusafiri kisha agawa mali zake (talanta) kwa watumwa wake ili wazisimamie . Lengo la Bwana yule ilikuwa wale watumwa wasimamie zile mali kwa faida ili baadaye aje awalipe sawasawa na kazi zao. Hadithi ni ndefu ila unaweza kusoma mathayo 25:14-30,

Hii mada inaweza kuwa ndefu kidogo na ya kufikirisha hivyo kama huwezi kusoma vitu virefu na kushirikisha akili yako ni bora ukaishia hapa. Ipo nchi moja ya kufikirika ambayo waliamua kukabidhi mamlaka yao na maliz zao kwa mfalme wao ili azisimamie na kwavile mfalme pekee yake hakuwa na uwezo wa kufanya yote hayo , wale wananchi wa nchi ile walimpa mfalme mamlaka ya kuteua watu kumsaidia kusimamia yale aliyokasimiwa na wananchi wa nchi ile. Tatizo moja au kosa kubwa alilolifanya mfalme ni kuchagua wasaidizi wake akidhani wana ueledi au ni waaminifu kumbe haikuwa hivyo kwa wote. Wenye uelewa wa mambo walianza kumshangaa mfalme kwa kuteua watu wasio na sifa stahiki kushika uongozi katika mashirika na maeneo mengine nyeti ya nchi vigezo vikiwa ni kujuana na mfalme , wapambe wa mfalme, kugombea na kisha kushindwa katika kura za maoni katika chama cha mfalme, kumsifia sana mfalme miongoni mwa sifaa kadhaa

Kama mnavyojua masikini akipata matako hulia mbwata, baadhi ya wateule wa mfalme walitolewa kwenye sehemu zao za awali walipokuwa wakiongoza watu wasiozidi 50 wakapewa kuongoza watu 800, waliongoza mtaa wakapewa wilaya , mwalimu mkuu akapewa ukurugenzi, hapa ndipo timbwili lilipoanza. Kwa mfano yuko bwana moja katika nchi ile ya kufikirika alipopewa tu Ukurugenzi akasema hataki watu wazima wote waliokuwa pale alipopewa kusimamia. Akataka kuwafuta kazi wote tatizo hakuwa na hela ya kuwalipa ili waondoke. Bila kujua kwamba hao wazee ndiyo walioweka msingi wa shirika husika, bila kujua kuwa hao wazee ndiyo waliotandaza nyaya kibao chini ya ardhi ambayo hao vijana aliokuwa anawataka hawakujua hizo nyaya zilipo. Huyu bwana akaanza kudhoofisha idara nyeti za shirika kwa kuondoa watu aliyowakuta, akitumia kile kinachoitwa rushwa ya ngono ndani ya miaka miwili karibia mameneja wote wamekuwa wanawake hili si kosa kama wanapatikana kwa merits zao. Huyu bwana amekuwa akihutubia vikao vya wafanyakazi hata masaa sita pekee yake bila hata kuwapa wafanyakazi nafasi ya kuchangia, akitumia lugha ya matusi vitisho na kejeli nyingi ili aweze kuogopwa.

Hali ya mambo ndani ya shirika husika ni mbaya kuliko inavyoweza kuelezwa, akitumia gawio kama kiinimacho kumdanganya bosi wake na wenye nchi yao kwamba hali ya shirika ni nzuri kumbe hali ni mahututi. Badala ya kuweka miradi mipya amebaki kung'oa mitambo huku kupeleka pale yaani mfano akiona hali ni mbaya sehemu A basi anang'oa mitambo sehemu B na kupeleka sehemu A ili kudanganya umma wa nchi ile. Akiwa amejiwekea walinzi wa kutosha , wadada wazuri pembeni anazunguka nchi ya kusadikika kufanya kazi ambazo zingefanywa na wasaidizi wake huko mikoani. Ameshindwa kubadili fursa kibao alizozipata na zilizopa kuongoza shirika vizuri, wafanya kazi wake wamechoka mbaya kutwa nzima kufunga na kujifariji kuwa wanafanya diet kumbe hali zao ni dhoofu bina hali. Magari ya shirika yamekuwa kama screpa hakuna kitu. Ilivyo bahati mbaya bidhaa zinazozalishwa na shirika husika zimetapakaa kwa wazalishaji wengine. Huduma imekuwa mbovu kiasi cha wateja kulalamika kila kukicha ila bosi yeye anakula raha, ushindani wa kupata ajira hamna idara ya rasilimali watu imepigwa ganzi kazi yao ni kugawa tu barua za ajira zinazotoka kwa mkuu .

Kibaya zaidi huyu mtu alijua ataitumia taasisi hii ya watu wa kusadikika kama ngazi ya kupata ubunge bado hajaamini msimamo wa bosi wao wa kuwaonya kuacha nafasi zao walizopewa kushika kwa ajili ya ubunge. Alitaka avuruge mambo ili akimbilie ubunge ila sasa kama kumfia kitamfia mwenyewe. Kama ambavyo bahari haikai na uchafu ndivyo ambavyo pia ukweli haiwezi kufichwa hata ikizibwa mdomo iko siku itapiga kelele na kujulikana kwa wote. Najua kuna siku atashindwa kutoa gawio, kulipa mishahara na hata kuendeleza huduma mbovu zilizopo na hapo ndipo mwenye shamba atamwambia wewe ni mtumwa mbaya na kuagiza akatupwe kunako ziwa la moto. Huyu ni moja tu wa dada wa kazi ninayemjua ila najua wako wengi sana wanakula na kunywa maziwa ya watoto najua siku yao inakuja.

Amani iwe nanyi nyote!
Nchi hiyo tabia za mfalme zinafanana sana na nchi ninayo ijua mimi
 
Mkajipange kwa upya!mnaandika tamthilia humu JF nani mwenye muda huo?andika kinachokuhusu acha umbeya wa kwenye vijiwe vya akina mama
Hasira za nini mkuu? Mi sio mtoa mada na wala mtoa mada hajataja TTCL. Mimi nimekisia kama watu wengine wanavyoweza kukisia tofauti na mimi. Halafu mimi kama mTz ni shareholder wa TTCL kwa hiyo nikicomment kuihusu jua kuwa linanihusu.
 
Back
Top Bottom