Sijui kama jimbo la Nyang'hwale linafahamika

KASEME

New Member
Dec 9, 2012
1
0
Habari wanaJF? kwanza niwasalimu na kuwashukuru Mods kwa kunipokea hapa jamvini. Ninayo mengi ya kusema nanyi hususani kuhusu ufahamu wa wanabodi kuhusiana na jimbo la Nyang'hwale kwani sielewi kama watu wanatambua uwepo wake!!! Ikiwa ni wanajimbo wenyewe, watawala na hata wadau wowote wawao wa maendeleo. Watakaosema lolote, ama watakuwa wamenitoa matongotongo au watakuwa wamenipa pakuanzia kupata taarifa za jimbo hili.
Nawasilisha.
 
Namkumbuka mseminari wa siku nyingi aliyekuwa mbunge wa hapo bunge lililopita
 
Duh. Sielewi ndo nyambari nyangwine au kiumbe kingine!
 
Habari wanaJF? kwanza niwasalimu na kuwashukuru Mods kwa kunipokea hapa jamvini. Ninayo mengi ya kusema nanyi hususani kuhusu ufahamu wa wanabodi kuhusiana na jimbo la Nyang'hwale kwani sielewi kama watu wanatambua uwepo wake!!! Ikiwa ni wanajimbo wenyewe, watawala na hata wadau wowote wawao wa maendeleo. Watakaosema lolote, ama watakuwa wamenitoa matongotongo au watakuwa wamenipa pakuanzia kupata taarifa za jimbo hili.
Nawasilisha......

Umeanza vibaya kaka, Sasa unataka kujua kama waJF wanalifahamu Jimbo la Nyang'hwale au unataka kufahamishwa kuwa jimbo la Nyang'hwale lipo? sababu umeanza kwa kusema hujui kama kuna watu wanatambua uwepo wake ikiwa ni wanajimbo wenyewe, watawala hata wadau wa maendeleo.

Sasa kijana unataka kusema kweli hujui kama watawala hawajui uwepo wa Nyang'hwale? yaani hata wanajimbo wenyewe hawajui uwepo wa jimbo lao? huenda ulikuwa unamaanisha tofauti na ulichoandika. Sasa unataka utolewe tongotongo kuhusu kulifahamu hilo jimbo kama lipo au kuhusu nini?

Then unasema unayo mengi ya kusema na sisi juu ya jimbo hilo mwishoni unataka utolewe tongotongo juu ya jimbo hilo hilo, which is which. Ni sawa huenda unalitaka hilo jimbo lakini gear unayoingilia siyo lazima upime kwanza maneno yako then njoo na hoja kwa nini 2015 wamkatae huyo mwarabu na wakupokee wewe?.

Kwa ufupi jimbo la Nyang'hwale ni moja kati ya majimbo matatu ya wilaya ya GEITA mengine ni GEITA na BUSANDA ambapo najua kuna dogo anakwenda kugombea kule na Inshallah nitakuwa mpambe wake.
Otherwise tupe hayo mengi uliyonayo kuhusu jimbo la Nyang'hwale..

Chief Lugina for BAVICHA CHAIRMAN-GEITA REGION next ELECTION
 
mbunge wa jimbo hilo ni std 7.hata mbunge wa Busanda mbali kuwa graduate kaolewa DAR
 
Ni moja ya majimbo ya iliyokuwa wilaya ya Geita na ni moja ya wilaya mpya ktk mkoa mpya wa Geita. Mbunge wake anaitwa Kazu ni std 7.
 
Anachotaka kujua ni uhai wa jimbo hilo kisiasa, kiuchumi na maendeleo mengine!!!msaidieni wananyang'hwale uenda akawa na la muhimu kuwajulisheni, waswahili wana usemi wao mgeni njoo wenyeji wapone!!!
 
Habari wanaJF? kwanza niwasalimu na kuwashukuru Mods kwa kunipokea hapa jamvini. Ninayo mengi ya kusema nanyi hususani kuhusu ufahamu wa wanabodi kuhusiana na jimbo la Nyang'hwale kwani sielewi kama watu wanatambua uwepo wake!!! Ikiwa ni wanajimbo wenyewe, watawala na hata wadau wowote wawao wa maendeleo. Watakaosema lolote, ama watakuwa wamenitoa matongotongo au watakuwa wamenipa pakuanzia kupata taarifa za jimbo hili.
Nawasilisha.

Kama unamaanisha jimbo la uchaguzi la Nyag'wale ni kweli lipo na linafahamika na NEC, Bunge la JMT, wakazi na wapiga kura jimboni n.k. Sasa sijui unauliza kufahamika kupi?

Kwa taarifa tu ni kwamba Jimbo la Nyag'wale (sasa ni wilaya mpya pia) lipo katika mkoa mpya wa Geita (zamani Mwanza). Jimbo hili limeongozwa na Bw. James Musalika wa CCM kwa vipindi viwili (au zaidi??) kabla ya kuangushwa kwenye kura za maoni (wenye chama caho wanasema kura hazikutosha) na Bw. Ahmed Nassor Amar mwaka 2010, ambaye kwa sasa ndio mbunge wake kupitia chama kiileeeee cha magamba. Tofauti na majimbo jirani kama vile Busanda, Geita na hata Sengerema ambayo angalau yanaonyesha dalili za nguvu ya upinzani kuzidi kuimarika, jimbo hili bado linaonekana kama himaya ya magamba. Yamkini, nguvu zaidi ya upinzani inahitaji kuelekezwa huku kwa wananchi hawa watanzania wenzetu, walima nanasi kwa wingi, wanaoishi kwenye maeneo yenu dhahabu nyingi lakini hali ya maisha yao ni duni. Kila kukicha ni heri ya jana, lakini bado wanaendelea kuimba 'chama chama kimetukomboa chama'........
 
Lile duka la jumla la spea za pikipiki za kichina la Nyamigogo liko maeneo ya msimbazi si duka la huyo mbunge wa Nyang'hwale?
 
Habari wanaJF? kwanza niwasalimu na kuwashukuru Mods kwa kunipokea hapa jamvini. Ninayo mengi ya kusema nanyi hususani kuhusu ufahamu wa wanabodi kuhusiana na jimbo la Nyang'hwale kwani sielewi kama watu wanatambua uwepo wake!!! Ikiwa ni wanajimbo wenyewe, watawala na hata wadau wowote wawao wa maendeleo. Watakaosema lolote, ama watakuwa wamenitoa matongotongo au watakuwa wamenipa pakuanzia kupata taarifa za jimbo hili.
Nawasilisha.

Ndio kwanza nakusikia wewe,
Ni kitu gani hiki?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom