Sijui kama hii nayo ni breaking news au vipi: Hatimaye JK avunja baraza lake!

Wow,at least ameonyesha courage ya kukubali kuna matatizo...hope atatuwekea watu wenye kujua nini wanafanya & wenye visions za maendeleo na sio wala rushwa na wazembe wasio na ujuzi wowote wanachokifanya,safi sana imenikumbusha zile termination za wazungu huku...we've to let you go,hahahhaha haha haha!
 
..waungwana swali la chap chap,hivi Baraza likivunjwa na Waziri mkuu naye nje au? mwanakiji unajua hili jibu najua upo mtandaoni sasa
 
najua kama angekuwa anajua kupanga ni kuchagua, kwanza angeniteua niwe mbunge, kisha anikabidi wizara ya utamaduni....

Najua baadhi ya mawaziri breki ya kwanza itakuwa Aghakan Hospito au Muhimbili kushusha presha. Na hii itatikisa sana jiji walah ameamua kiume. Kwa mara ya kwanza sauti ya umma imesikilizwa...

Naomba mnijuze hali ya karamagi
 
yap waziri mkuu naye anakuwa out. hiyo ni kikatiba na ndiyo nia rahisi ya kumweka pembeni maana njia nyingine zina ukiritimba wake na inawezekana zikashindikana...
 
waungwana kama naanza kurudisha IMANI na nchi yetu sasa,namtakia JK apate nguvu asione huruma ,awaweke wanaostahili ,watu wachape kazi sasa,nchi ibadilike.nimekuwa nafwatilia JF kwakaribu wengi wenu mnamawazo yaliyokomaa na yenye uchungu na nchi yenu,endeleeni naamini kuna siku Tanzania itabadiika sana.
 
Katika yote, kilio changu kikubwa ni ukubwa wa baraza la mawaziri. Tafadhali mheshimiwa punguza baraza hilo. Ni mzigo mkubwa kwa sisi walipa kodi.
 
Hii mbona kama haijatulia vile? Isije ikawa ni Hasara mwingine.

Kama kweli baraza limevunjwa itakuwa safi sana, afadhali kuanza upya.
 
Mkjj ukiconfirm hii story niambie ili nijiandae kusherehekea ushindi wa pili dhidi ya Kikwete.

Atakuwa amesalimu amri kwa alichokiita kelele za wapinzani au vyura (ana dharau huyu baba). Najiandaa pia kumtumia senti 84 kama nilivyomuahidi!

Keep me posted!
 
msianze kufurahi hata kama ni kweli hakutokuwa na jipya sana watu ni walewale watabadiliswa tu,wachache sana watapigwa chini na waziri mkuu atakuwa yuleyule.
 
Jamani,

Hii habari sio kweli, baraza la mawaziri haliwezi kuvunjwa saa sita usiku.

Nafikiri JF imeingiliwa na virus, inatakiwa tujitahidi kupata anti-virus vinginevyo JF itaharibika.
 
Katika yote, kilio changu kikubwa ni ukubwa wa baraza la mawaziri. Tafadhali mheshimiwa punguza baraza hilo. Ni mzigo mkubwa kwa sisi walipa kodi.

Hawezi kupunguza; washikaji zake aliowaihidi wakati wa kampeni itakuwaje? Tusubiri tuone.
 
Jamani,

Hii habari sio kweli, baraza la mawaziri haliwezi kuvunjwa saa sita usiku.

Nafikiri JF imeingiliwa na virus, inatakiwa tujitahidi kupata anti-virus vinginevyo JF itaharibika.

Kama hii habari nayo itakuwa feki, basi tumeingiliwa, na itatushushia hadhi sana! We must find a way of fixing this sooner than later!
 
Habari hii hadi hivi sasa nimeshindwa kuiconfirm nyumbani.. na vyanzo vya karibu kabisa... Rais yuko Lindi sasa hivi na kesho anaelekea Arusha kukutana na mjumbe toka Marekani (nadhani Waziri wa Fedha)...
 
Please Admin Remove This Thread As Soon As Possible Kama Hakuna Ukweli,what's The Point Watu Kupoteza Nguvu Kujadili Kwa Vitu Visivyo Na Uhakika.
 
Back
Top Bottom