Sijui huyu msichana nimfanyie nini anikubalie

RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,516
1,776
Wakuu,

Kuna binti mmoja nampenda sana tena sana, basi kidume nikajikunja kumtafuta huyo dada angalau nimueleze kilicho moyoni.

Tukawa na mazoea ya kawaida, nikaamua kumuambia ukweli lakini binti akaanza mizinguo ukimtumia sms hajibu ukimpigia hapokei au hata akipokea anataka muongee kwa mda mfupi, kila siku unajitahidi kumpa hi! Lakini yeye hata siku moja hawezi kukuanza au kukukumbuka, huyu binti ni mlokole mimi ni RC lakini nimetumia kila njia nimeshindwa kumpata, je nifanyeje?

Na ndo msichana ninayempenda, naombeni ushauri ndugu zangu, matusi hayaruhusiwi.
 
du
Kuna mawili

1. Usinikubali haraka

2. Hauna kitu cha kumvutia hapa pesa swaga Muonekano kaelimu dini n.k. mwanamke anaweza kukupendea unavyokohoa tu.

Jifikirie saana hapo no.2
uuuuu sawa mkuu ishu ya pesa no kwasababu tunasoma wote unversity moja hapa bongo na yeye sio mtu wa pesa
 
Sitisha zoezi la kupiga simu na kutuma sms,
Mtafute face to face mwambie akusamehe kwa kilichotokea na ulikuwa unania njema na yeye pengine labda sio mipango ya mwenyezi mungu na urafiki wenu uendelee usiishie hapo, lakini kwa sasa umeamua kutulia kama ilivyo kuwa hapo mwanzo mpaka siku mungu atakapo kuonyesha kwingine kama alivyo kuonyesha kwake.

Baada ya hapo kuwa busy piga kazi,
Boresha muonekano wako (vaa kiheshima) ,
Tulia msikilizie,

Akikutafuta nenda naye taratibu,
Asipokitafuta achana naye.
 
du

uuuuu sawa mkuu ishu ya pesa no kwasababu tunasoma wote unversity moja hapa bongo na yeye sio mtu wa pesa
sio mtu wa pesa? Ahaa bado wewe boy ukiwa mkubwa utaelewa. Hivi utaanzaje kusema yeye sio mtu wa pesa??

Btw, ana mtu wake anaemuhudumia nje ya chuo, ndo maana hana mda wa kujibu visms vyako.
 
Kuna mawili

1. Usinikubali haraka

2. Hauna kitu cha kumvutia hapa pesa swaga Muonekano kaelimu dini n.k. mwanamke anaweza kukupendea unavyokohoa tu.

Jifikirie saana hapo no.2

Wakati niko chuo niliwahi kupendwa na mdada flani kisa eti sitani nywele, ananifananisha na mtu aliyekuwa anachorwa kwenye story ya Gazeti la Amba.
 
Wakati niko chuo niliwahi kupendwa na mdada flani kisa eti sitani nywele, ananifananisha na mtu aliyekuwa anachorwa kwenye story ya Gazeti la Amba.
Hawa watu ni bahati yako tu.

Ulifananishwa na baba ubaya nini. Ni gazeti la ambasada au amba maana hilo silijui
 
Hawa watu ni bahati yako tu.

Ulifananishwa na baba ubaya nini. Ni gazeti la ambasada au amba maana hilo silijui

Kama ulikuwa msomaji wa gazeti la Sani kipindi cha nyuma, waliwahi kuja na gazeti pacha waliliita AMBA au AMBHA kama nalikumbuka vizuri, sasa kulikuwa na story ya mapenzi sikumbuki vizuri ila ilihusisha Pemba na Bara, moja ya wahusika waliokuwa wanachorwa ana nywele za kipemba na alikuwa hatani nywele.

Cha ajabu sasa yule dada alikuwa na matoleo yote ya hilo jarida, na mimi nilianza kuyasoma kwake baada ya kuwa na urafiki naye, sijui kama bado anayatunza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom