Sijisikii Fahari kuhusishwa na Mbunge wala Bunge la Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijisikii Fahari kuhusishwa na Mbunge wala Bunge la Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Aug 7, 2012.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2012
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati nilidhani pengine iko siku nitagombea ubunge, niwe mbunge wa bunge la Jamhuri ya Tanzania

  Nafurahi tamaa hii imepotea kwa kuwa Ubunge na Bunge letu vimekosa hishima na uadilifu mbele ya jamii ya Kitanzania na duniani kiasi kwamba sitamani kuhusishwa navyo.

  Kuna nyakati wahalifu fulani walikuwa wanajisikia fahari kuwa wahalifu au kuhusishwa na kundi fulani la uhalifu. Pale Magomeni mapipa paliwahi kutokea kundi linaitwa vijana wa Yoso, ambao walikuwa waporaji na wabakaji maarufu wanaojisikia fahari kufanya vitendo hivyo pamoja na kujulikana kwamba wao ni Yoso.

  Bunge letu
  linakula rushwa
  limeshindwa kuwajibisha serikali kuhusu ufisadi na mikataba mibovu
  limeshindwa kusimamia serikali kukuza uchumi na kushusha inflation
  limeshindwa kusimamia serikali uporaji wa mashirika na viwanda vya umma
  linapitisha sheria za misamahaa ya kodi kwa wawekezaji na wafanya biashara kubwa
  limeshindwa kusimamia serikali kukusanya kodi kikamilifu
  limeshindwa kusimamia serikali kuboresha huduma za jamii (elimu, afya, maji, etc)
  linatumika na serikali kukandamiza haki
  linajilimbikizia mali na pesa za umma
  linatunga sheria kudhulumu wananchi
  limeshindwa kuwatetea walimu na madaktari waliogoma
  linapitisha bajeti za kifisadi
  linajitukuza kuzidi wananchi
  limegeuka kuwa uwanja wa mipasho na majungu


  Wabunge wetu
  wanakula rushwa, ni mafisadi
  wameshindwa kudhibiti mafisadi
  wameshindwa kusimamia mikataba yenye tija kwa taifa
  wanajiongezea mishahara wakati wafanyakazi hawaongezewi
  wameshindwa kuwatetea walimu na madaktari waliogoma
  hawalipi kodi katika mishahara na posho zao
  hawaungani kutetea maslahi ya wananchi bali maslahi yao
  wanapitisha sheria za dhuluma kwa wananchi
  wanapitisha bajeti kifisadi
  wanajitukuza
  wanapika majungu na mipasho

  Sijisikii fahari kuhusishwa na Mbunge wala Bunge la Jamhuri ya Tanzania
   
 2. Kwisimla

  Kwisimla Senior Member

  #2
  Aug 7, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Uwiiiiii! tutakimbilia wapi jamani............inatisha.
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Unaweza ukasaidia kuleta mabadiliko somedays,who knows????
  Usikate tamaa.
   
 4. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Toka walivyopitisha sheria ya kipuuzi ya SSRA sitamani kusikia kitu kinaitwa bunge wala wabunge,
  labda nitabadilisha msimamo wangu siku sheria hii ikibadilishwa.
   
 5. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Usikate tamaa kuna wabunge wachache bado wana uchungu na nchi yao.
   
 6. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Mkuu kuna kitu hujakitafakari vizuri. Nionavyo mimi, tatizo kubwa lipo kwa wabunge wengi wa ccm kwani wanaendeleza maslahi ya chama chao ndani ya serikali. kIla kitu kwao ni NDIYOOOOOOOO!!!! halafu hii sheria YA marekebisho ya mifuko ya jamii ya ssra baadhi ya wabunge wa upinzani wamezungumza hadharani na kudai hicho kipengele cha umri hakikuwepo wakati wanaijadili. sasa hapa inaonekana KILICHOMEKWA juu kwa juu na serkali ya magamba kwa sababu wazojua wao. ndo maana mi nilipendekeza kama kuna uwezekano tujikumbushe kwa hansard za bunge tujiridhishe hasa ilkuwaje.
  USHAURI WANGU: watanzania tujihusisheni sana na siasa. wanasiasa wana maamuzi nyeti sana yanayohusu mustakabari wa maisha yetu, wao ndo wanapitisha bajeti ambayo ndani yake kuna MISHAHARA, HUDUMA ZA KIJAMII mf MAJI, DAWA, BEI ZA VITU, UDHIBITI WA RASILIMALI ZETU n.k. tukiwaachia wanasiasa mambo nyeti kama haya, halafu bahati mbaya wakawa wahuni, hakyanani watatuchuuza mchana kweupe. Watanzania tujipangeni tuiondoe ccm ili tujipange kivingine. ccm haina jipya na haioneshi dalili za kubadilika. mafisadi ndo tena wanapewa uenyekiti wa kamati za fedha na uchumi, unategemea nini hapo?????????
   
 7. HASSAN SHEN

  HASSAN SHEN JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 428
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kinachonishangaza ni kwamba hata wabunge niliokua nao chuoni enzi zile uanafunzi wakijifanya wanaharakati,wapigania haki makamanda majina kibao wamebadilika na kuiacha misimamo yao. Hivi wamerogwa au ilikua njaa?
   
Loading...