Sijawahi 'perform poor' kiasi hiki mpaka wife ameshangaa

kalisheshe

JF-Expert Member
Mar 19, 2020
1,845
3,438
Habari zenu wanajamvi

Kuna kitu tusaidiane kidogo ndg zangu. Ninaimani wengine pia watasaidika na michango itakayotolewa.

Iko hivi:

Nilikua kikazi mkoani takribani mwezi mzima. Juzi nimepata nafasi kidogo nikasafiri usiku mzima kurudi nyumbani. Nimefika wife kanipokea nikalala.

Kesho yake Kama kawaida ya wanandoa wife kaniita nikaitika tukasafiri Safari ya Kwanza salama. Kimbembe kimekuja wakati tunaianza safari ya pili. Gari limezimika mwanzoni kabisa mwa Safari. Tukiforce linawaka tena linazima.

Mpaka muda huu wife kanuna hatari anapaki aondoke kwa kuhisi nimefanya usaliti ndo maana iko hivyo. Hali hii ni ngeni kwangu na imenishangaza sana.

Leteni michango yenu nijue nafanyeje? Maana yake JF Ni nyumbani.

Naamini wengi watasaidika kutokana na hii ishu yangu
 
Hauna madeni ya kufa mtu? Au unatumiaga booster? Je, ulikuwa umekula vizuri na kwenda choo vizuri? Je, alikuwa anakupa bashasha?
Gari likizimika inabidi liachwe kwa muda mrefu, la sivyo ile hofu ya kuzima tena, inafanya lizimike kweli!
 
Back
Top Bottom