Patrick Elias
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 332
- 108
Wadau huu umaarufu wa Russia hasa huku bongo unatoka wapi? Majanga kibao ya ukame, vita, mafuriko, matetemeko ya ardhi huku kwetu Afrika lakini sijawahi kusikia Russia kasaidia hata chumvi kwa wahanga bali wanaofanya hivyo ni USA na baadhi ya nchi za magharibi na china kidogo. Sasa hawa waswahili wanatumia vigezo gani kuwa pro russia? Make sidhani kama Russia walishawahi kutusaidia kopo moja la aspilin. Mbaya zaidi hawa waswahili pro Russia wanakuwa against USA na wanafanya hivyo huku wao na familia zao wakiwa wamelala kwenye vyandarua vya watu wa marekani, wao na ndugu zao wamekunywa sana ARVs kwa hisani ya watu wa marekani, wao na familia zao wanapata huduma za afya, maji, umeme,nk kwa hisani ya watu wa marekani lakina mswahili bado anaponda tu na kusifia Russia ambaye hasaidii chochote katika jamii yake. Mimi nahisi Russia anapata umaarufu bongo kwa sababu ya kuikoromea Marekani tu na si vinginevyo, umaarufu wa aina hiyo hata Iran, korea kaskazini na iraq wanao lakin hizo nchi hazina lolote za kawaida sana.