Sijawahi ona wala kusikia Russia imetoa hata gunia moja la mahindi kama msaada

Patrick Elias

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
320
195
Wadau huu umaarufu wa Russia hasa huku bongo unatoka wapi? Majanga kibao ya ukame, vita, mafuriko, matetemeko ya ardhi huku kwetu Afrika lakini sijawahi kusikia Russia kasaidia hata chumvi kwa wahanga bali wanaofanya hivyo ni USA na baadhi ya nchi za magharibi na china kidogo. Sasa hawa waswahili wanatumia vigezo gani kuwa pro russia? Make sidhani kama Russia walishawahi kutusaidia kopo moja la aspilin. Mbaya zaidi hawa waswahili pro Russia wanakuwa against USA na wanafanya hivyo huku wao na familia zao wakiwa wamelala kwenye vyandarua vya watu wa marekani, wao na ndugu zao wamekunywa sana ARVs kwa hisani ya watu wa marekani, wao na familia zao wanapata huduma za afya, maji, umeme,nk kwa hisani ya watu wa marekani lakina mswahili bado anaponda tu na kusifia Russia ambaye hasaidii chochote katika jamii yake. Mimi nahisi Russia anapata umaarufu bongo kwa sababu ya kuikoromea Marekani tu na si vinginevyo, umaarufu wa aina hiyo hata Iran, korea kaskazini na iraq wanao lakin hizo nchi hazina lolote za kawaida sana.
 
JustDoItNow

JF-Expert Member
Dec 3, 2013
2,880
2,000
Duh! kaka embu rudia tena.........LOL
au jamani kama kuna mtu kamuelewa nisaidieni kufafanua. Chandarua na ARV ndo misaada?
 
Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Wadau huu umaarufu wa Russia hasa huku bongo unatoka wapi? Majanga kibao ya ukame, vita, mafuriko, matetemeko ya ardhi huku kwetu Afrika lakini sijawahi kusikia Russia kasaidia hata chumvi kwa wahanga bali wanaofanya hivyo ni USA na baadhi ya nchi za magharibi na china kidogo. Sasa hawa waswahili wanatumia vigezo gani kuwa pro russia? Make sidhani kama Russia walishawahi kutusaidia kopo moja la aspilin. Mbaya zaidi hawa waswahili pro Russia wanakuwa against USA na wanafanya hivyo huku wao na familia zao wakiwa wamelala kwenye vyandarua vya watu wa marekani, wao na ndugu zao wamekunywa sana ARVs kwa hisani ya watu wa marekani, wao na familia zao wanapata huduma za afya, maji, umeme,nk kwa hisani ya watu wa marekani lakina mswahili bado anaponda tu na kusifia Russia ambaye hasaidii chochote katika jamii yake. Mimi nahisi Russia anapata umaarufu bongo kwa sababu ya kuikoromea Marekani tu na si vinginevyo, umaarufu wa aina hiyo hata Iran, korea kaskazini na iraq wanao lakin hizo nchi hazina lolote za kawaida sana.

Thinking za kiafrika huwezi pata shida kuzitambua, yaani umekaa unafikiria misaada tu badala ya kufikiria ni jinsi gani tutaweza kukuza uchumi wetu na kuwasaidia wengine wakiwemo hao Russia???
 
SNAP J

JF-Expert Member
Dec 26, 2013
5,261
2,000
Mtoa mada unauhakika na uamyasemayo au umeamua kuanzisha uzi bila kufanya utafiti.
Kama jambo ulijui ni bora ukauliza ili uelimishwe.
 
lumanyisa

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
884
500
nilikuwa mahala akaja mzungu akakaa pembeni yangu.hakuongea kitu mpaka alipopita mtoto mmoja wa mtaani akiwa na nguo zilizochanika na kuchoka mno.akanigusa bega akaniambia "unadhani bajeti yako isingetegemea fedha yangu mtoto yule angetembea uchi?" nikasema labda usingetusaidia asingevaa kitu kabisa.akacheka sana akasema kwani nakusaidia? si utalipa deni langu.na usipolipa ntachimba mafuta kwa miaka 60 na kukuachia faida ya 5%.alisema amevaa nguo iliyotengenezwa UK ila ni pamba ya Tanzania.pamba hiyo ilizalishwa huku kukiwa hakuna kiwanda cha nguo hivyo alipokuja Edward Roberts yule mfanyabiashara wa madini ya tanzanite alipewa kama zawadi baada ya yeye kugawa pen kwenye shule ya msingi majengo.pengine bila shule ya majengo kutegemea pen za Roberts pamba ingebaki na mtoto yule angevaa nguo.....

samahani hivi mtoa uzi kabila gani?? ....ungejua misaada inavtokuumiza usingepoteza muda kuandika uzi kama huu
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,530
2,000
Hutoa misaada ya silaha!kule ni barafu muda mwingi watalimaje?Labda usaidiwe gesi na mafuta
 
Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,202
2,000
Please consult your history. Russia na China toka miaka tunapata uhuru imekuwa ikitoa scholarships nyingi sana kwa vijana wetu.Marehemu Abdulhaman Babu wa Zanzbar ni mmoja wa vijana wa mwanzo kusomeshwa na Warusi.Waalimu wengi wa vyuo vyetu vya ufundi wamesomeshwa kwa misaada ya China na urusi.Askari wetu wengi wamesomea Urusi na China. Au kwa tafsiri yako msaada ni kupewa unga tu ule? Kafanye research kwanza kidogo ndio uje hapa!
 
zugimlole

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
1,903
2,000
Misaada misaada tu unalijua deni la taifa ptuuuu akili za kiafrika mpk asaidiwe ndo ajue urafk wa kwel
 
dexterous

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
1,527
2,000
hao wanaotupa misaaada ndo wanatupa masharti magumu ya kimaendeleo na kutufanya ubongo wetu ulale kuwategemea jamani msifikirie misaaada kuweni kama nchi nyingine zinazoishi bila misaaada ili mjikomboe kwenye ukoloni mambo leo la sivyo tutazidi kuwa masikini mpaka mwisho wa dunia
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,534
2,000
Russia hawataki mambo ya kijinga jinga kuombwa ombwa vitu..we umeona jk kapeleka bakuli russia ..atakula karate na putin atoke manundu...russia hawna mambo ya kihivyo
 
Patrick Elias

JF-Expert Member
Jan 27, 2011
320
195
Bush kasaidia pesa ya miradi kibao, obama kaja na pesa kibao na mradi wake wa power afrika, USAID inapiga jeki hadi visima vya maji vijijini. Huyo putin na russia yake kasaidia nini cha maana hadi mnamkubali kiasi hicho? Si bora hata norway
 
msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,612
2,000
Huna hoja ndo maana umeishia kulalamikia mtoa mada tu

Mtot wa kiume wewe utageuzwa kutegemea vya kupewa.!
Hivi unajua wanapotupa hzo net wanakua wamepewa migodi kwa miaka mingapi bila kulipa kodi.?
Hivi unajua wanapotupa ARV wanachukua vitalu vingapi vya gesi.!

M nilidhan utashangaa kwann hatuna kiwanda cha net ili tusiombe we ndo unafurahia kuomba.!!

Nasisitiza mtoto wa kiume wewe acha hizo utageuzwa..ohooo
 
lumanyisa

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
884
500
Huna hoja ndo maana umeishia kulalamikia mtoa mada tu

Nadhani maneno yako yalipaswa yasemwe na yeye.wewe hoja yako ipi? Urusi hakusaidii? Usihofu hii ni kwa kuwa mgodi wa tanzanite ule wa kule kaskazini kapewa bredford Stuart na sio Nikolai Sergei.hata hivyo hakuna pro Russians bongo sionagi hata vijibendera ila pro Americans kama wewe mpo.una asilimia 60% ya ardhi haijalimwa then unataka msaada toka nje....believe me ungeishi mitaa ya Frankfurt miaka ya 1941 fuhrer angeshatoa kichwa chako...samahani lakini huoni adhabu kubeba jambo kama hilo?
 
Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
12,981
2,000
Please consult your history. Russia na China toka miaka tunapata uhuru imekuwa ikitoa scholarships nyingi sana kwa vijana wetu.Marehemu Abdulhaman Babu wa Zanzbar ni mmoja wa vijana wa mwanzo kusomeshwa na Warusi.Waalimu wengi wa vyuo vyetu vya ufundi wamesomeshwa kwa misaada ya China na urusi.Askari wetu wengi wamesomea Urusi na China. Au kwa tafsiri yako msaada ni kupewa unga tu ule? Kafanye research kwanza kidogo ndio uje hapa!

Naunga mkono hoja, nina Baba yangu hapa nyumbani yeye alipata Elimu ya Mrusi kipindi cha Utawala wa Mwl Nyerere. Kikubwa ni kwamba Mrusi na Mchina huwa hawajitangazi ktk mambo yao kama anavyofanya Mmarekani.
 
Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
12,981
2,000
Mtot wa kiume wewe utageuzwa kutegemea vya kupewa.!
Hivi unajua wanapotupa hzo net wanakua wamepewa migodi kwa miaka mingapi bila kulipa kodi.?
Hivi unajua wanapotupa ARV wanachukua vitalu vingapi vya gesi.!

M nilidhan utashangaa kwann hatuna kiwanda cha net ili tusiombe we ndo unafurahia kuomba.!!

Nasisitiza mtoto wa kiume wewe acha hizo utageuzwa..ohooo

Kuna watu wanakera jamani, anataka na yeye Russia iwe inajitangaza pale inapotoa msaada kama USA, kwa bahati mbaya Urusi sio watu wa sifa na ni taifa ambalo linaogopwa kuchezewa na Nchi yoyote ile. Achana nae huyo.Nisaada wanayotupa na wanavyochukua ni vitu viwili tofautiiiiiiii.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom