Sijawahi Kuwaelewa Watu Hawa

Masulupwete

JF-Expert Member
Feb 15, 2012
2,366
2,397
Kuna watu huwa hawajui kununa. We ukimuudhi yeye anacheka tu. anaweza kuwa kwenye hali ngumu ya kutatiza lakini utakuta mtu bado anatabasamu tele usoni.

Hivi watu ni wa kawaida kweli au?
 
Ukinichekesha sicheki, ukitaka nikusikilize kwa umakini siwezi ila tupo simple
 
eeh ndio hivyo..ila wakati mwingine pasipo wewe kuwepo watu wa namna hiyo hucheka pekeyao..na wanamambo ya kujinga sana, pu..u zinaweza muwasha akajikuna uku anacheka ama kurembua...we waache tu kama walivyo
 
Kuna watu huwa hawajui kununa. We ukimuudhi yeye anacheka tu. anaweza kuwa kwenye hali ngumu ya kutatiza lakini utakuta mtu bado anatabasamu tele usoni.

Hivi watu ni wa kawaida kweli au?
Tafiti nyingi zinaonyesha tabasamu ni kitu muhimu sana katika maisha ya mwanadam yeyote yule iwekwenye mahusiano ya kimapenzi au kawaida. Kwa mfano, tabasamu huwa ni kichocheo cha kuwavuta wengi kusikiliza au kutambua umuhimu wa mtu anayetoa tabasam hilo.
Watu wengi pamoja na kampuni nyingi zenye mafanikio kwa kujua hili, ndio maana zimeajiri watu wenye nyuso za bashasha au tabasamu pale mapokezi. Hivyo, Kama unataka kukubalika katika jamii, jifunze namna ya kutengeneza tabasamu zuri litakalo wavuta wengine kwako.
Pia tafiti hizo zinaendelea kuonyesha kila unapotasamu inasaidia kuwasisimua wengine kujaribu kukusikiliza. Hiyo ikiwa na maana kwamba hakuna mtu ambaye anapenda kumsikiliza mtu aliyenuna nuna. Ni lazima uwe na tabasamu fulani ili usikilizwe.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom