Uteuzi wa Wakuu wa Wilaya uliofanyika Juni 2021 umeshusha hadhi ya nafasi hiyo

Japo mie siipendi CCM Ila amechemka this time. Amebeba watu hata ambao hawapo kwenye siasa sio sawa, kuna watu wanahangaika na chama kila uchwao na wanatumia Hadi gharama zao kiukweli asingeweza kuchukua wote Ila nafasi hizi ndio huwa za kueapooza japo wapate jina.

Pia aleta watu ambao hawajawahi hata kujua minute sheet inaandikwaje mtu ametoka shule hajawahi kukaa kufanya kazi kidogo. In short secretary ndio anageuka mwalimu wa DC kumuelekeza namna ya kuendorse mafaili.

Kachemka sana na kwa huu mwendo nimeanza kumchoka mapema sana.
Hahahaha hahahaha vita vya panzi
 
Nafasi wapewe lakini sio ukuu wa wilaya. Wanaelewa nini kwenye utumishi na ulinzi na usalama.
Ni swala la kuwaelekeza misingi ya kazi yao na majukumu ya ukuu wa wilaya..

Kwani kuna mahali huyo unaemuita mtu mzima kasomea ukuu wa wilaya..???

Kulikuwa na watu wazima lakini wakaishia kuwaambia wananchi watulize matako chini
 
Watanzania siyo waelewa kabisa mama hajakosea mnataka ateuwe ma classmates wake,kabila lake, ndugu zake marafiki wa familia zao hivyo acheni hizo habari wangeteuliwa watu wasiyo na umaarufu kelele hizi zisingekuwepo sijui ni wivu au nini

Tatizo la hao walioteuliwa ni nini
Umaarufu wao?
Mlitaka wateuliwe wakina Musiba,Makonda hawa wawili ukiwajulisha hawana busara za Mchopa lakini mngeona ni sahihi tu

Sijaona tatizo katika teuzi inabidi namna yetu ya kufikiri ibadilike watanzania

Wengi wa walioteuliwa wana kiwango kizuri tu cha elimu angalau kwa nafasi hiyo waliyopewa siyo mbaya
busara fulani ni watu wanaojielewa sioni makosa wanafaa kuwa viongozi
Ni nani hakustahili na kwanini

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Wewe nani mpaka useme hivyo cha kushangaza wewe ni mateka wa Mbowe unataka Rais Samia, akufurahishe? Nyie kupinga ndiyo kazi mliotumwa na Mfalme Mbowe, Rais kawambia mpo huru kufanya mikutano yenu nchi nzima au nyie mnafanyie JF.
Mkuu mbona POVU jingi hivyo? Kama povu limezidi hebu vua tamang'eo yake ufulie. Wewe shambulia hoja usimshambulie mtoa hoja. Hapa ndipo watanzania wengi mnapokwama.
 
Inasikitisha sana Tanzania sijui inaelekea wapi. DC ni nafasi nyeti ya kuunganisha watendaji na jamii inayowazunguka. Kusimamia mambo ya ulinzi na usalama. Hii ni nafasi ya waandamizi kutoka katika utumishi au chama, wakiwa wamejaa utu uzima na busara za kumwagika. Leo unaenda kuokoteza wasanii na watu mitandaoni.

Naona Tanzania inapoteza uelekeo kabisa. Hawa jamaa wanatupa kazi sana kuirudisha Tanzania kwenye reli.

Mimi sijawahi kushuhudia uteuzi wa hovyo kama huu toka nizaliwe.

Kiufupi rais kaelemewa na majukumu
Kuna jamaa yangu kateuliwa wilaya flani kanda ya ziwa mkoa unaanzia na S. Yaan huyu jamaa ni 0 brain wa kutupwa, yes ana kadegree ila akili nzito hajui kila kitu, ana 40+ hana mke, hana nyumba yaan maisha ya kuungaunga, mlevi kupindukia. Sijui wateuliwa kama wanafanyiwa vetting
 
Aisee uteuzi mbovu 75% .Yaani vyuo vya adminstrative vina changamoto,Kuna ma professor ,wahitimu weredi wakubwa wa siasa na uongozi.
Leo hii bongo movie,bongo fravour,Journalist wawe ma DC.
Nchi Bado inasafari ndefu Sana ,acha waendelee kututukana mpaka tuishike adabu
Maprofessor wamefanyia nini hii nchi miaka yote hiyo mambo yamebadilika
Sasa leo mitandao iko active viongozi hawabweteki hawana uhakika wa kudumu kwenye nafasi kama watakuwa wazembe

Zama za hao maprofessor mambo yalikuwa hayaendi kwa kuwa akiteuliwa ndiyo imeisha miaka na miaka

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kweli bhana cheo cha mkuu wa wilaya kimeshuka sana thamani tangu awamu ya tano iingie madarakani......ni bora viondolewe tu wabaki meya na viongozi wa halmashauri waongoze maeneo yao.
 
Kwa mara ya kwanza katokota..watu kama kina Msando hao wanamsaidia nini? Au la yuko kwa system
Kimsingi huyo mama hana jinsi ya kuacha kuwapa vyeo baadhi ya watu waliowatoa upinzani. Ifahamike mbinu za ccm kuendelea kubaki madarakani ni pamoja na kuwachukua wapinzani na kuwapa vyeo, ili kushusha imani ya wapinzani na upinzani nchini. Hivyo iwapo wapinzani wenye uchu wa madaraka wanaoribuniwa na kuingia ccm baadhi yao wasipopewa vyeo, wengine hawatahamia ccm, na ccm itaendelea kujikuta katika wakati mgumu sana wa ushindani wa kisiasa.

Kiuhalisia ccm imeshapoteza ushawishi kwani tayari ni chama cha kizazi kilichopita. Hivyo inabidi kutumia mbinu za kughilibu wapinzani hasa kwa njia ya vyeo, ili kupunguza nguvu ya upinzani. Mbinu hizi ni za kawaida sana kwa vyama vyote vilivyo madarakani hasa kwenye nchi masikini, ambapo watu wengi wako kwenye siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, kisha itikadi baadae. Hivyo chama kinachokuwa madarakani hutafuta wapinzani wenye uchu wa madaraka na kuwapa vyeo, kisha kuwatumia kuchafua taswira ya upinzani ili kujijengea imani.
 
MATAGA ni kama vile leo hawapo
Kununa hawawezi sababu new supporters wa mama wakiboreka nae wao wanalazimika kujifanya wanaomsifia ili aharibu zaidi lakini mionyoni mwao wanaumia sana.

Na alifanya vizuri anasifiwa na new supporters Jambo ambalo bado wao linaendelea kuwauma.

In short wanaumia kotekote tu, ningekuwa MATAGA ningepumzika siasa kwa muda kama akina Bashiru walivyoamua kukaa kimya au bashite.
 
Aisee hizi ni chuki binafsi kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi kama ana akili timamu
 
Joketi kaweza kipi .Watu wa kisarawe wengi wao ni wakulima Bora kama angewasaidia kupata masoko ya mazao yao hapo tungeona kaweza.Eti mnadai kajenga shule .sasa kama ni shule mbona zimejengwa nchi nzima.nachokiona kwake anabebwa na midia tu ,Hana ubunifu wowote.
Naomba tupe mfano wa aliyeweza kwa vigezo vyako ili tupime huko kushindwa kwa jokate.
 
Kimsingi huyo mama hana jinsi ya kuacha kuwapa vyeo baadhi ya watu waliowatoa upinzani. Ifahamike mbinu za ccm kuendelea kubaki madarakani ni pamoja na kuwachukua wapinzani na kuwapa vyeo, ili kushusha imani ya wapinzani na upinzani nchini. Hivyo iwapo wapinzani wenye uchu wa madaraka wanaoribuniwa na kuingia ccm baadhi yao wasipopewa vyeo, wengine hawatahamia ccm, na ccm itaendelea kujikuta katika wakati mgumu sana wa ushindani wa kisiasa.

Kiuhalisia ccm imeshapoteza ushawishi kwani tayari ni chama cha kizazi kilichopita. Hivyo inabidi kutumia mbinu za kughilibu wapinzani hasa kwa njia ya vyeo, ili kupunguza nguvu ya upinzani. Mbinu hizi ni za kawaida sana kwa vyama vyote vilivyo madarakani hasa kwenye nchi masikini, ambapo watu wengi wako kwenye siasa kwa ajili ya maslahi binafsi, kisha itikadi baadae. Hivyo chama kinachokuwa madarakani hutafuta wapinzani wenye uchu wa madaraka na kuwapa vyeo, kisha kuwatumia kuchafua taswira ya upinzani ili kujijengea imani.
Acha zako wewe!

Mshamba na dhalimu wako si kafa?

Sasa unalialia nini?
 
Back
Top Bottom