Sijawahi kuona mama mwongo na mnafiki kama huyu mjane | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijawahi kuona mama mwongo na mnafiki kama huyu mjane

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PISTO LERO, Oct 3, 2012.

 1. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  mjane,Asia Ismail ambaye ni mke wa marehemu Ismail Omary aliyeuwawa katika maandamano ya Chadema mnamo januari 5 mwaka jana jijini Arusha akiwa amembeba mtoto wake wa kike,Amina Ismail juzi katika mkutano wa hadhara wa Cuf uliofanyika uwanja wa Levolosi ambapo alikishutumu Chadema kwamba kimetafuna fedha za rambirambi za marehemu mme wake na kisha kumtekeleza pamoja na kuhaidi kumpatia.(picha na mahmoud ahmad)
  .
  Mahmoud Ahmad,Arusha
  MJANE,Asia Ismail ambaye ni mme wake,Ismail Omary aliuwawa katika maandamano ya januari 5 mwaka jana amekishutumu Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) mkoani Arusha kwamba kimetafuna fedha za rambirambi za marehemu mume wake lakini mbali na hilo pia wamemtelekeza.

  Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama Cha Wananchi(Cuf) uliofanyika juzi katika uwanja wa Levolosi,mjane huyo alisema kwamba Chadema walihaidi kumpatia fedha za rambirambi zilizochangwa katika uwanja wa NMC wakati wa kuaga mwili wa mme wake lakini hadi leo hajazipata.

  Huku akiangua kilio katika mkutano huo alisema kwamba alipewa taarifa kwamba Chadema kinachangisha fedha za rambirambi na mara watakapokamilisha mchango hiyo watampatia lakini hadi leo hajawahi kuona fedha yoyote.

  Mjane,huyo aliyekuwa amembeba mtoto wake wa kike jukwaani aitwaye Amina Ismail alitoa machungu hayo na kwamba fedha aliyoambulia hadi sasa ni ile iliyotolewa na kada ya CCM,Mustafa Sabodo kiasi cha sh,5 milioni .

  Hatahivyo,alisema kwamba mara kwa mara alikuwa akifunga safari kufika katika ofisi za Chadema wilayani hapa kwa lengo la kufuatilia fedha za rambirambi za mumewe lakini badala yake alikuwa akipigwa danadana.

  “Nimekuja hapa leo mkutanoni kuelezea machungu yangu ninasikitika sana kwamba Chadema ,mbali na kuchangisha fedha za rambirambi za marehemu mume wangu lakini hadi leo sijawahi kuona hata senti tano”alisema huku akinagua kilio


  Hatahivyo,mjane huyo alisema kwamba pamoja na chama hicho kutangaza kuijali familia yake mara alipofariki mme wake lakini hadi leo hakuna kiongozi yoyote anayejua maendeleo ya familia hiyo.

  Alisema kwamba marehemu mme wake alimwachia watoto wawili ambapo kwa sasa anahangaika kuwahudumia kuwapatia mahitaji mbalimbali kama elimu,malazi na chakula hatahivyo mara nyngine anashindwa kuyatimiza kutokana na kukosa ajira ya kudumu.

  Mara baada ya kutoa kilioo hicho ndipo uongozi wa Cuf uliamua kuitisha harambee jukwaani hapo ambapo wafuasi mbalimbali wa chama hicho walimchangia mjane huyo kwa kumkabidhi fedha hizo mikononi kiasi cha zaidi ya sh,500,000 huku wakilaani kitendo kilichofanywa na uongozi wa chama hicho.

  Alipatafutwa katibu wa Chadema mkoani Arusha ili ajibu madai hayo kwanza alikanusha madai hayo na kusema kwamba wao walimpa rambirambi zote zilizochangwa na wafuasi wao ambazo hawajui ni kiasi gani pamoja na hundi ya kiasi cha sh,5 milioni zilizotolewa na Sabodo.

  Alisema kwamba hata kwenye kumbukumbu ya mauaji ya januari 5 mwaka huu walimpatia kiasi cha sh,200,000 mjane huyo na kudai anaendeshwa na upepo wa kisiasa na kuvitaka baadhi ya vyama vya siasa kumwogopa Mungu.

  Kuhusu madai ya kutekelezwa Gorugwa alisema kwamba hawawezi kuweka utaratibu wa kumpigia simu kila siku kwa kuwa kila mmoja ana maisha yake na hata mjane huyo ana maisha yake huko mkoani Tanga.

  “Jamani tumwogope Mungu huyu mama anapelekwa na upepo wa kisiasa tu lakini tumwonee huruma kwa kuwa ni mjane, sisi tulimpa hela yote na alisaini hundi ofisini kwetu na hata nyie waandishi mlikuja kupiga picha”alisema Gorugwa


  HATAKAMA NI UPEPO WA KISIASA HUWEZI TAMKA MANENO KAMA HAYO,HATAKAMA KULIKUWA NA MPANGO WA KUENDELEA KUMSAIDIA AU KANA KUNA MTU ALIKUWA ANATAKA KUMSAIDIA HUYU MAMA ATAKUWA AMESHA JIHARIBIA NINAWEZA KUSEMA HANA MAANA WALA SHUKRANI.INAMPASA AMWOGOPE MUNGU WAKE NA ATUBU,KWELI INAUTHI,INATIA HASIRA NA KUKATISHA TAMAA SANA.
   
 2. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Akili za maiti
  ndo anatumia!
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Yaani huyu mama kusema kweli mmekula pesa zake kama rambirambi leo amekuwa muongo.
   
 4. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Chadema wengi viongozi wenu ni wasanii! wamejawa tamaa tu,mpeni huyo mjane pesa zake acheni utapeli!
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,749
  Trophy Points: 280
  Sikutegmea useme tofauti na hivi.
  Na zile za wahanga wa mabomu ya mbagala na Gongo la mboto una zikumbuka!

   
 6. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nduguyangu sikufichi huyu mama ni kinyonga,mbona wale wenzake hawalala miki?au alitaka mpaka chumvi apelekewe.
   
 7. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Moods tafadhali msihamishe hii topiki
   
 8. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #8
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kweli CUF tajiri, Inahudumia wajane wote wa kisiasa? Wasimsahau Mjane wa yule aliyeuliwa na Ditopile
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  tuache ushabiki, mama akiwekwa sawa atasema sawa

  chadema wasimdharau huyu mama hata kama anatumiwa
  ila tuangalie serikali iliyomuua inabeba jukumu gani
  na ccm kutumia marehemu ambaye familia yake inateseka sisahihi

  ila naona kama ana nguo mpya, itakua kuna mtaalam anatumia karata za siasa kujipigia pande na siajabu akaishiwa kuwa hata sexually explored sababu ya desperate situation aliyonayo
   
 10. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #10
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Huyo anatafuta wa kumuoa mke wa tatu!
   
 11. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na zile za wahanga wa mafuliko kilosa wamekula chadema,pole
   
 12. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #12
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Majibu yaliyotolewa kuhusu michango binafsi hayajaniingia akilini, yaani mkutano mkubwa kama wa CDM zipatikane 200,000.00 peke yake!!!!!!!

  Hapa tuache ushabiki unless otherwise kuna shida.
   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Oct 3, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Binafsi nikisikia jambo lolte ovu linahusshwa na CCM siwezi kushangaa sana lakini kama CDM nao wataiga tabia hiyo ni wazi watakuwa wamepotea.
   
 14. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #14
  Oct 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  CHADEMA inachagua wahanga! Ismail na Ally hawawajali ila DAUD MWANGOSI wanasomesha watoto wake!
   
 15. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #15
  Oct 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni mikutano ya CUF? Yale yale tu kama ya thithiemu
   
 16. M

  Mboerap Senior Member

  #16
  Oct 3, 2012
  Joined: Apr 8, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kageuza msiba kama mradi. Milioni 5 ni msingi tosha kwa mtu makini.kama hizo ameshindwa kufungua hata genge la nyanya basi hafai huyu !!
   
 17. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #17
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  huzo pesa ni zile zilizopatikana kwenya mkutano wa kumbukumbu ya kuwakumbuka hao marehemu,na pia wako wajane wa tatu.
   
 18. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #18
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hao walikataa msaada wa chama,na badalayake wakaiba maiti na kutokomea nae tanga
   
 19. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #19
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  asante ndugu,anataka mpaka nyanya asaidiwe
   
 20. Wi-Fi

  Wi-Fi JF-Expert Member

  #20
  Oct 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 748
  Trophy Points: 280
  you are right.
   
Loading...