GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Kwanini Watanzania mliosheherekea Sikukuu ya Christmas ya leo mmevaa nguo mbaya mbaya kiasi kwamba hata hamjapendeza huku wengine mkivalia nguo zile zile za kupandia Madaladala tulizozoea kuwaona nazo na kama haitoshi leo karibia nyumba ( Kaya ) nyingi chakula kilichotawala ni Makande, Ugali na Dagaa au Ugali na Maharage huku tembele likionekana kutocheza mbali.
Je tatizo ni nini Watanzania hadi leo kuharibu hivi? Halafu na cha ajabu zaidi huwezi amini katika Siku Kuu za Christmas ni hii tu ya leo ndiyo nimeweza kuona Watanzania wengi wakilala mapema kwani kwa mji huu tu wa Dar Watu wamelala Saa 3 na nimeambiwa kuwa huko Mkoani Kilimanjaro Watu wamelala leo Saa 1 na nasikia huko Mikoani Geita na Mwanza Watu leo wamelala Saa 12 na si ajabu hata sasa wanaota ndoto zao za nne au za tano huku nikiambiwa kuwa Mkoa wa Arusha leo mjini kumekauka kabisa Watu na pombe za Baa zimedoda kabisa huku wengi wao wakishindia tu Mirungi kama moja ya Kiburudisho chao cha Siku ya Noele ( Christmas ).
Shikamooni Watanzania ama hakika sasa tumenyooka!