Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar, lakini watu wana Gucci

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,519
Sijawahi kuona brick-and-mortar store yoyote hapa Dar na Tanzania kwa ujumla, ya luxury brand yoyote ile.

Lakini huku mitaani utaona watu wamenyuka pamba za Moschino, kapelo za Gucci, mikanda ya Louis, suruali za Burberry, mikoba ya Ferragamo na kadhalika.

Kwa wadada ndo acha kabisa yaani. Siku hizi ni kawaida sana kuona wadada wamebeba mikoba ya Alexander Wang, YSL, Givenchy, Miu Miu, na kadhalika.

Ila kuna ka trend nimekaona hususan hapa Dar. Nako ni Gucci kuwa ndo brand inayobamba kwa sasa.

Naamini kabisa kuwa asilimia 99.99 ya wote wanaovaa Gucci hapa mjini [na hata luxury brands zingine] wanavaa bidhaa feki.

I mean, mtu unaishi uswazi huko ambako hata njia hakuna una ubavu wa kuweza kumudu Gucci halisi kweli?

Sidhani hata kidogo.

Ni muda muafaka sasa serikali pengine kupitia TBS kuanza ku crackdown vendors wote wanaojihusisha na biashara za bidhaa feki.

Cheki hizi Gucci za kitaa

Angalia label ya hii tisheti...

IMG-20170515-WA0010.jpg


IMG-20170515-WA0009.jpg
 
Brand ya Gucci kipindi hiki zimevalika kinyamaa.. Nenda kkoo huone machinga walivyomwaga chini.. Mzgo bei chee
 
Pale unapotoka ulaya uje uswazi ili utambe na nguo yako yenye nembo maarufu alafu unakuta muokota chupa ameivaa then copyright....mbwembwe zote zitakuisha na kuishia JF kulia

Pole mkuu Mchina si mtu mzuri hata kidogo.
 
Pale unapotoka ulaya uje uswazi ili utambe na nguo yako yenye nembo maarufu alafu unakuta muokota chupa ameivaa then copyright....mbwembwe zote zitakuisha na kuishia JF kulia

Pole mkuu Mchina si mtu mzuri hata kidogo.

Usiyemjua humjui tu.

Mimi si mtu wa kuvaa lifulana lina maandishi ya Gucci kifuani.

Siyo zangu kabisa.

Hivyo pole yako ipeleke kwingine maana kwangu umenoa.
 
hakunaga nguo feki mkuu labda useme brand owners ndio walalamikie suala la watu ku-fake label

Kilicho feki ni watu kuiga bidhaa za wengine na kuziuza kwa kutumia jina lao.

Wewe siyo Gucci kwa nini utengeneze kofia ya Gucci halafu uiuze kibandani?

Kwa nini usitumie jina jingine utumie jina lao?

Hapo ndipo ufeki ulipo.
 
Ukitaka orginal brand za hizo bidhaa kwa Dar ni either ununue GSM Malls au Woolworth...


Kwingine kote zinakuwa feki.. Tena feki haswa...


Cc: mahondaw
 
Halafu waambiwe ni feki huku wamenunua kwa elfu labda 25 au hata buku 10 weeee, wataanza vijembe hadi wakijibishana utafikiri walilipa bei ya zenyewe kabisa :D

:D:D:D:D:D

Halafu wengine wala hata hawajui kuwa ni feki!

Ni bora hata ukiwa unajua kuwa ni feki na unaamua tu kununua na kuvaa huku ukijua ni feki.

Wale wanaonunua na kuvaa huku hawajui kuwa ni feki [wakidhani kuwa ni genuine] ndo wanatia huruma maana ni wajinga halafu hata hawajui kuwa ni wajinga!
 
Unajua imebidi nicheke tu...wewe mod uliyebadili heading ni bora unge consult kwanza na mimi kabla ya kubadili heading!

Anyway, sawa....
 
Unajua imebidi nicheke tu...wewe mod uliyebadili heading ni bora unge consult kwanza na mimi kabla ya kubadili heading!

Anyway, sawa....
Sasa ndo naelewa kwamba hiyo headline hukuandika wewe au ilikuwa edited. Nilikuwa najiuliza mara mbili mbili kwa kuwa kwa nondo ambazo huwa unazimwaga humu lazima utakuwa unafahami brick and mortar.
 
Sasa ndo naelewa kwamba hiyo headline hukuandika wewe au ilikuwa edited. Nilikuwa najiuliza mara mbili mbili kwa kuwa kwa nondo ambazo huwa unazimwaga humu lazima utakuwa unafahami brick and mortar.

Brick-and-mortar niliiandika kwenye mada, siyo kichwa cha mada.

Mods ndo wameiongeza kwenye kichwa cha mada.

Kwa hiyo, ni maneno yangu bado na siyo ya mods [hayo ya brick-and-mortar].
 
Kitu gani ni halisi au cha kiwango bora hasa kwenye hizi nchi maskini? Wakati mwingine hata kama unapesa yako na unataka kitu kizuri kukipata chenye ubora inakuwa shida. Ndio maana wengine wanaamua kuelekea kwenye mitumba tu angalau huko watapata vitu vya ukweli japo vimetumika.

Bidhaa nyingi, achilia mbali mavazi, zinazotengenezwa kulenga soko la nchi zetu zina viwango duni sana.
 
Back
Top Bottom