Sijawahi kuishi popote zaidi ya Tanzania, haya yanayoendelea na kwa wenzetu yapo!?

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Ki ukweli natamani sana kufahamu kwa undani yafuatayo :-

1. Namna vyombo vyao vya habari vya ndani vinavyotoa kipaumbele kwenye habari zao - Maana hapa kwetu hata tukio dogo tu la Wema kuhama chama ni mijadala kwenye front page za magazeti na kipaumbele kwenye electronic media

2. Namna viongozi wao waandamizi wanavyojihusisha na mambo ya kijamii - maana hapa kwetu hata kiongozi Mkuu anapotoa msaada kwa muhitaji anataka wote tufahamu

3. Namna vyama vya siasa vinavyoshughulika na kujenga uchumi wa nchi - Maana hapa kwetu, ni kuviziana tu! Huyu akitaka kufanya hili, mwingine anatoa vijembe na wengine hata kuzuiwa kwa kuwekewa vikwazo fulani fulani

4. Hivi ni kweli hata huko wateule wa Mkuu huwa hawawezi kuonyesha weledi wao pasipo kutafuta sifa kwa Mteua!? Hapa kwetu naona kama ipo siku yatatokea mashindano ya kumfurahisha mtu badala ya kulifurahisha Taifa.

5. Hivi hata huko kila kitu kinageuzwa kuwa cha kisiasa!? - Maana hapa kwetu kila kitu kinachoibuka kwenye jamii kinavikwa siasa za upande fulani kulingana na taswira ya jambo lenyewe

Yako mengi sana, mimi naona kama tukiendelea hivi maendeleo ya Taifa kwa ujumla tutaendelea kuyasikia kwa wenzetu!

Sijui wenzangu mnaonaje.
 
Ki ukweli natamani sana kufahamu kwa undani yafuatayo :-

1. Namna vyombo vyao vya habari vya ndani vinavyotoa kipaumbele kwenye habari zao - Maana hapa kwetu hata tukio dogo tu la Wema kuhama chama ni mijadala kwenye front page za magazeti na kipaumbele kwenye electronic media

2. Namna viongozi wao waandamizi wanavyojihusisha na mambo ya kijamii - maana hapa kwetu hata kionhozi Mkuu anapotoa msaada kwa muhitaji anataka wote tufahamu

3. Namna vyama vya siasa vinavyoshughulika na kujenga uchumi wa nchi - Maana hapa kwetu, ni kuviziana tu! Huyu akitaka kufanya hili, mwingine anatoa vijembe na wengine hata kuzuiwa kwa kuwekewa vikwazo fulani fulani

4. Hivi ni kweli hata huko wateule wa Mkuu huwa hawawezi kuonyesha weledi wao pasipo kutafuta sifa kwa Mteua!? Hapa kwetu naona kama ipo siku yatatokea mashindano ya kumfurahisha mtu badala ya kulifurahisha Taifa.

5. Hivi hata huko kila kitu kinageuzwa kuwa cha kisiasa!? - Maana hapa kwetu kila kitu kinachoibuka kwenye jamii kinavikwa siasa za upande fulani kulingana na taswira ya jambo lenyewe

Yako mengi sana, mimi naona kama tukiendelea hivi maendeleo ya Taifa kwa ujumla tutaendelea kuyasikia kwa wenzetu!
Nchi nying zilisha jiwekea misingi ya kudumu ya utawala na vipo vyombo vyenye mamlaka ya kuwajibisha mamlaka nyingine za juu na pia katiba zao kwa nchi zilizo nyingi hazina ubinafsi hivyo kila muhimili unajisimamia wenyewe bila shuruti tofauti na hapa kwetu na nchi zilizo nyingi za africa ambazo katiba zao ziliwekwa kulinda zaid maslahi ya watawala na ubinafsi kitu ambacho kinafanya viongozi ngazi za juu wakikiuka sheria basi tutegemee zaid busara na hekima ya rais na likikosekana hilo basi nikuvumilia mateso hadi atakapo jiridhisha yeye ingawa na yeye kwa mujibu wa katiba nyingi za nchi za kiafrica ni intangible na tatizo kubwa kwa nchi zetu zilizo nyingi za kiafrica ndipo linapo anzia.ni hayo tu.
 
Fanya kazi Kijana usaidie wazazi wako ili kuepuka kuitwa SPERM DONOR na WANAO. Hiki kilichokujaa MOYONI Hatikaleta chakula mezani kwako, Kina MELO Wanakutumia kutunisha ACCOUNTS Zao. Wake Up
 
Afrika ni watoto wa mama mmoja

SA japokua mahakama imemkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha za umma lkn ANC bungeni wakamlinda dhidi ya kura ya no confidence. Hiyo ni nchi at least twasema katiba yao ndio bora. Wakati brexit tu iliondoka na serikali ya kameruni

Nadhani wakoloni kuna kitu walifanya zaidi ya kutawala, si kwa hizi akili
 
Nchi nying zilisha jiwekea misingi ya kudumu ya utawala na vipo vyombo vyenye mamlaka ya kuwajibisha mamlaka nyingine za juu na pia katiba zao kwa nchi zilizo nyingi hazina ubinafsi hivyo kila muhimili unajisimamia wenyewe bila shuruti tofauti na hapa kwetu na nchi zilizo nyingi za africa ambazo katiba zao ziliwekwa kulinda zaid maslahi ya watawala na ubinafsi kitu ambacho kinafanya viongozi ngazi za juu wakikiuka sheria basi tutegemee zaid busara na hekima ya rais na likikosekana hilo basi nikuvumilia mateso hadi atakapo jiridhisha yeye ingawa na yeye kwa mujibu wa katiba nyingi za nchi za kiafrica ni intangible na tatizo kubwa kwa nchi zetu zilizo nyingi za kiafrica ndipo linapo anzia.ni hayo tu.
Nimekuelewa sana Mkuu, hasa hasa hapo kwenye kutegemea busara za kiongozi kuliko kutegemea misingi iliyowekwa!

Na vipi kuhusu vyombo vya habari vya ndani kukuza habari ambazo kwa mtazamo hazina manufaa kwa taifa zaidi ya kukuza umaarufu wa watu tu!?
 
Fanya kazi Kijana usaidie wazazi wako ili kuepuka kuitwa SPERM DONOR na WANAO. Hiki kilichokujaa MOYONI Hatikaleta chakula mezani kwako, Kina MELO Wanakutumia kutunisha ACCOUNTS Zao. Wake Up
Sijakuelewa vizuri, hasa kwenye SPERM DONOR na kutumiwa na kina Melo
 
Fanya kazi Kijana usaidie wazazi wako ili kuepuka kuitwa SPERM DONOR na WANAO. Hiki kilichokujaa MOYONI Hatikaleta chakula mezani kwako, Kina MELO Wanakutumia kutunisha ACCOUNTS Zao. Wake Up
Lazima ujue kazi na siasa ni vitu vinavuo fanya kazi pamoja ndio maana utaona machinga anauza hiki hapa akija mwana siasa anamihamishia pale na akija mwingine atampeleka hapa kila mmoja na maslahi yake kiasiasa ,kama unadhani kila kimoja kinajitegemea basi kuna haja ya kujitafakari namna unavyo fikiri na uelewa wako katika mambo ya kijamii na kisiasa
 
Nimekuelewa sana Mkuu, hasa hasa hapo kwenye kutegemea busara za kiongozi kuliko kutegemea misingi iliyowekwa!

Na vipi kuhusu vyombo vya habari vya ndani kukuza habari ambazo kwa mtazamo hazina manufaa kwa taifa zaidi ya kukuza umaarufu wa watu tu!?
Hayo yoten yanajibiwa na hoja ysngu hapo juu
 
Pole sana kwa kuishi ndani ya chungu cheusi kwa muda wote , Tanzania ndio nchi ya mwisho kabisa kwa kila kitu , ila ni ya kwanza kwa ujinga .
 
Fanya kazi Kijana usaidie wazazi wako ili kuepuka kuitwa SPERM DONOR na WANAO. Hiki kilichokujaa MOYONI Hatikaleta chakula mezani kwako, Kina MELO Wanakutumia kutunisha ACCOUNTS Zao. Wake Up
Hapa ni jukwaa la kutoa hisia, where we dare talk openly. So ukiona mada haikuhusu pita.
 
Back
Top Bottom