Sijasikia wananchi wa kawaida wakiwalilia mashujaa wa CHADEMA waliotiwa nguvuni

1627017685341.png
 
Yaani raia hawana hata mpango na hizo harakati za katiba na wala hawana taimu na hao 'mashujaa' walioshikwa. Twitani sasa na humu jf sasa
 
Mbona hujui kama TANU ilipata sapoti kubwa?
Na nani hapo mwanzoni? Wangapi walijitokeza kuwapa hiyo sapatin hadharani? Wangapi waliandamana kumshurutisha mkoloni aondoke? Watu kama wakina Sykes, Phombeah, Mwakangale, Bibi Titi na vijana walikuwa wachache. Sapoti ilikuwa ya kujificha na ilikuja kuonekana baadae kwenye uchaguzi wa Legco.

Shida yenu ni mnadhani sapotaz wa wakina Mbowe ni wale wanaovaa magwandwa na wanaoenda kwenye makongamano peke yao. Mtashangaa kuwa hata wengine wanaovaa kijana moyoni wanawaunga mkono. Kipimo pekee cha kukubalika kwa chama chochote ni uchaguzi huru na wa haki. Kitu ambacho hamkitaki.

Amandla...
 
Upinzani tunautaka sana, ila sio kama huu Upinzani wa kihuni

Ni upumbavu kuwa mpinzani hasa wa chama viongozi wake wanajihusisha na masuala ya kigaidi
 
Maisha magumu Sana mtaani, huo muda unautoa wapi? Miaka mitano ya Jpm vyuma vilikaza.Mama ameanza Tena purukushani na wapinzani, sijui maisha yatakuwaje..
 
Mbowe hua hapendi siasa za vurugu mstaarabu sana
Yeye ni baba ,babu ,mlezi hivyo ukisema afanye siasa uchwara hawezi MTU wamungu yule anatamani sana kushindani kwahoja kuliko nguvu na marazote amekua mshindi

Shule za zamani zilikua zurisana penyewe Mnamwitaga FoRM six

Form yazamani kiboko
Anapiga mwingi prof hata unabaki mdomo wazi

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Wanaopika vitumbua wako busy, machinga wapo busy, manesi na walimu wanajadili dakika moja na kuchapa shughuli zao.

Waliotiwa nguvuni wanajinasibu kuwa ni wapigania haki na wakombozi wa taifa hili dhidi ya udhalimu wa CCM.

Je ni kweli? Mbowe na Pambalu wamegeuka kuwa mashujaa wa kupigania haki za watanzania? Lwaitama? Nani mwingine?

Lissu ,kidogo ana historia kubwa na nzuri kupigania haki za watanzania, ila aliharibu kujoin CHADEMA, bora angeanzisha chama chake.

Kama kweli waliotiwa nguvuni wanakubalika kwa umma leo kingenuka hapa bongo.

My take; Damu ya shujaa aliyeipigania Tanzania na wanyonge itaitafuna Tanzania kama Damu ya Lumumba inavyoitafuna DRC.
Chadema ni chama kinachopendwa na BAADHI YA VIJANA WA VYUO VIKUU.....wako wangapi ?!!!

Vijana wengi wako mitaani na wanaendelea na SHUGHULI zao tu....

Niko huku mitaani uswazi....watu wala hawana hisia za HURUMA NA KUKAMATWA KWA MH.MBOWE.....wengi wanasema CHADEMA inataka kutuletea MACHAFUKO kwa sababu wanatumiwa na mataifa ya NJE.....

#KaziIendelee
#NchiKwanza
 
Back
Top Bottom