Sijasikia "JIPU" hata moja lililofungua kesi ya kupinga kutumbuliwa

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Namba ya majipu yaliyotumbuliwa ni kubwa na sijasikia hata moja lililokwenda mahakamani kupinga kutumbuliwa huko. Basi tuamini walitumbuliwa kihalali na nashauri utumbuaji uendelee, bado hata hayajasogea.
 
Ninawasiliana na wanasheria Wangu ili nimfikishe ICC ndugu mtumbuaji. Subiri utasikia.

By Mtumbuliwaji anayetafakari.
 
Kwani umesikia mara ngapi watu wameahirishiwa safari za ndege wamefungua kesi? Umesikia mara ngapi mtanzania kaombwa rushwa akaripoti au kufungua kesi? Umesikia mara ngapi watu waliopigwa danadana ya njoo kesho kupatiwa huduma wakafungua mashtaka?

Jibu ni kwamba nchi hii ina very incompetent lawyers na wananchi wapuuzi ambao hata anyimwe haki hawezi kushitaki anamuachia Mungu. Ndio maana watu hata wakipata ajali hawaendi kudai kulipwa bima kwa vile wanaacha haki zao watalipwa na Mungu.

Hata hao waliotumbuliwa hawaendi kushtaki kwa kuogopa visasi vya serikali na kesi kuchukua muda mrefu au watamuudhi mwajiri. Ndio maana hata mtu mkubwa kama Pinda au Ghalibu Bilal majina yao yaliyofyekwa bila utaratibu na Kamati kuu ya CCM walimuachia Mungu tu. Ndio utanzania huo
 
wanasheria mpo????hivi kuna ukomo ktk kushtaki aina hii ya kesi??wakija kushtaki mwaka 2026 wakaishtaki serikali kuwa haikutenda haki??
 
Udom wameshikwa wanafunzi wanaopokea mkopo kinyume na sheria.....ni baada ya kufanyiwa uhakiki
 
Back
Top Bottom