Sijasikia ACACIA wakijitetea, namsikia Mtanzania Tundu Lissu akiwatetea!

Lisu ni limbukeni sana wa wazungu.
Na yule aliwaita Barick wanaume si ndio limbukeni maana walichoongea ndani hakukielewa akaja kuwapotosha lumumba wenzake wasiojua kimombo km yeye kuwa wametubu kulipa kumbe aliambiwa tutaingia kwenye njia ya majadiliano km ya kuangalia nani anatakiwa kulipwa hebu kampigeni Rais wenu msasa wa kimombo anatia aibu sana phd holder kichwani akili km ya bashite
 
Huyo unasema wewe. Mimi nimesema Lisu ni limbukeni wa wazungu. Upo hapo?
 
Tundu Lissu ana haki zote za kikatiba za kutoa maoni na mawazo yake bila kuvunja sheria, na hiyo ndio demokrasia ambayo imenenwa kwenye katiba.

Kutaka Tundu Lissu asitoe maoni na mawazo yake ni sawa na kuvunja katiba, labda kama anachoongea kinatishia utulivu na amani. Lakin tuangalie kiini hasa cha tatizo.
Hakuna anayekataa,ila Tundu kwa hili kachemka sana.
 
Ukweli gani wa kuhalalisha nchi kuibiwa?wananchi tuko nyuma ya magufuli chochote kilichoibiwa kiwe kiliibiwa kisheria au kitaalamu tunakitaka waturudishia. Hatutaki mtu asingizie kuwa niliwaibia kisheria na kibaraka wao lisu aje aseme wezi mlikuwa mna uhalali kuiba kwani mliiba kisheria. Shenzi type Hata wakoloni waligawana nchi zetu kisheria lakini watu walipochoka wakasema hatujali mpo hapa kisheria au la ondokeni tuachieni nchi
Mambo hayaendi kama mnavyodhani sasa.kibashite bashite.
Tuko hapa kusubiri hizo fedha kama tutalipwa mi ni na shida gani kwani wakati napata Noah yangu.
 
Tundu Lissu ana haki zote za kikatiba za kutoa maoni na mawazo yake bila kuvunja sheria, na hiyo ndio demokrasia ambayo imenenwa kwenye katiba.

Kutaka Tundu Lissu asitoe maoni na mawazo yake ni sawa na kuvunja katiba, labda kama anachoongea kinatishia utulivu na amani. Lakin tuangalie kiini hasa cha tatizo.
Tatizo lipo ktk lugha ya dharau kuita ripoti iliyo andaliwa na jopo la wasomi ni takataka. Hii kitu ktk jumuiya ya wanazuoni haikubaliki. He went too far with his wide mouth. Hakusomea mambo ya madini wala chemistry kwa kiwango cha angalau ordinary certificate, wala hajui methodology za kuchukua sample na jinsi ya kuandaa kutambua kilichomo. Sasa anapata wapi ujasiri wa kutukana wataalamu wasomi kiwango cha kufikia uprofesa. Kumbuka kuna Prof. Ikingula na Prof. Mruma ni geologist bado wale dokta wengine, na wale wataalamu wa chemical processing engineering. Ile ripoti haihusiki na haikufuatilia fani ya sheria bali ilihusu fani ya madini na miamba. Yeye bora angesubiri ripoti ya pili ya kisheria. Au angesubiri kesi mahakamani akaupata ukweli ktk ushahidi wa serikali hapo angejua ushahidi wa ovyo km ulipikwa au ulikosewa na sio sasa ambapo kuna mengi serikali haijaweka hadharani. Kile tulichokisikia ni sehemu tu ya report.
 
Kuna watu wajinga nchi hii tena wengi sana. Km sio ujinga ni kutetea matumbo yenu.

Lissu kasema wekeni hyo mikataba hadharani ileywe bungeni bado mnasita sifa. Kwann hamtaki? Lissu kasema hawa watu wanatuibia sana na miaka yote mmekuwa mkipitisha hz sheria kwa ndiooo za kutosha leo mnamlaum Lissu? Mwaka 2015 mlileta sheria za mafuta na gesi kwa hati ya dharula mkawafukuza wapnzani bungeni leo mnasema Lissu anatetea wezi?

Wajinga sana nyie watu
 
Sasa hivi tunataka chetu tuwe tuliibiwa kisheria au whatever tunataka chetu to hell with tundu lisu na visheria vyake koko vya kutetea wezi. Akae mbali kwenye hili tulichoibiwa tunakitaka kwa gharama yoyote kirudi

5ab8adfed9ac17ca5e2dc8f3fa7e60bb.jpg
Kamati ya kuongea na Acacia
 
Mleta mada unaonaje tukitayarisha mdahalo Kati yako na Lisu, una ubavu huo? Ama hizi ni propaganda tu za maccm?
 
CCM hebu acheni unafiki.haya madini tumeibiwa kwa miaka mingapi leo mjifanye kuchachamaa kinafiki na kujifanya wazalendo.?

Nisubiri Noah yangu.
 
Unprofessional.
Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu hapa kwa lengo kubwa kabisa la kutaka Watanzania wafahamu.

Je, sheria inasema mchanga ni mali ya ACACIA?

Lissu anasema kuwa kwa mujibu wa sheria mchanga ule ni mali ya ACACIA na hivyo Serikali kuuzuia ni sawa na kuzuia mali ya mtu. Kuhusu hili sijui amezungumzia sheria ipi? Katika Sheria Namba 14/2010 Sheria ya Madini hakuna jambo la namna hii kama Tundu Lissu anavyotaka kuliweka.

Hakuna popote ilipoandikwa kuwa mchanga wote unaochimbwa ni mali ya ACACIA. Na hili linajulikana kwani hata leseni za uchimbaji hutolewa kwa ajili ya uchimbaji madini na siyo umiliki wa ardhi. Ardhi ambayo hujumuisha mchanga hubaki mali ya Taifa.

Lakini pia katika hilo hilo lazima ieleweke kuwa hawakuwa wakichukua mchanga kwa sababu ni mali yao kama Lissu anavyosema. Hata wao hilo wanalikataa. Wanasema wanalazimika kubeba mchanga kwa kuwa hapa Tanzania hakuna kiwanda/mtambo wa kuchenjua mchanga na kupata wanachokitaka. Hawasemi walikuwa wanachukua mchanga kwa sababu ni mali yao, hapana. Ni utetezi wa Watanzania wenzetu unaosema mchanga ni mali yao.

Je, Acacia wametenda kosa lolote?

Lissu na kundi lake wanawatetea ya kuwa hawajatenda kosa lolote. Ni hivi, ukweli ni kuwa kuna makubaliano maalumu kati ya Acacia na Serikali kuwaruhusu kuchukua mchanga kwenda kuuchenjua katika kipindi ambacho Serikali itakuwa haijajenga mtambo wake.

Hata hivyo, lazima ieleweke kuwa makubaliano haya yanakwenda sambamba na wajibu wa kisheria wa kutoa taarifa sahihi kuhusu uzito wa kile wanachochukua pamoja na sampuli zilizomo.

Kuthibitisha kuwa wajibu huu upo, ndio maana mchanga huo hukaguliwa, na wao hukubali ukaguliwe na TMAA, TRA, nk. Mchanga haukaguliwi ili kujifurahisha, hapana. Unakaguliwa ili kujua uzito na sampuli za kile kinachochukuliwa.

Basi, hatua ya wao kukubali kukaguliwa na mamlaka hizi kwa malengo haya ya kujua wanachukua nini inathibitisha hata wao kuutambua wajibu wao wa kusema ukweli kuhusu uzito na sampuli za kile wanachobeba.

Sasa swali ni kama wajibu huu upo na wao wanautambua kwa kiwango hiki; je, kuukiuka kwa kudanganya kuhusu uzito na sampuli ni kosa au si kosa? Akili ya kawaida tu ya mtu ambaye hata siyo mwanasheria itapata jibu. Halafu anatokea Mtanzania anasema hawajafanya kosa lolote.

Lakini pia ukidanganya kuhusu uzito na sampuli utatoa mrahaba ulio chini ya kiwango, chini ya kile ulichotakiwa kutoa. Bado baadhi ya Watanzania wenzetu wanasema hilo nalo si kosa! Inasikitisha sana.

Makala yaliyopita nilieleza kwa urefu kosa la udangayifu hapa kwetu na huko kwenye mahakama za kimataifa. Muda huu itoshe tu kusema kuwa, jamani udanganyifu ni kosa (fraud/deceitful).

Na ni kosa pote mahakama za ndani (local courts) na katika hizo za kimataifa (International Arbitral Tribunal). Na hakuna shaka imethibitika makosa haya wameyatenda. Haya iko wapi hiyo kesi inayopigiwa debe kwa nguvu zote kuwa lazima tunashindwa?

Je, ni kweli ripoti ya Mruma ni takataka kama inavyoitwa?

Lissu anaiita Ripoti ya Tume ya Mruma- takataka, na kusisitiza kwa Kiingereza kuwa ni ‘rubbish’. Kwanza niseme kuwa maneno haya ni ya dharau kubwa kwa Profesa Mruma na wasomi wote aliokuwa naye kwenye kamati. Lakini pia ni dharau kwa rais aliyeunda kamati hiyo.

Kwa mtu mstaarabu na msomi ingetosha tu kusema ripoti ya Profesa Mruma haina ukweli, au haina mashiko, au si ushahidi mzuri, n.k. Kuiita takataka si tu ni uhuni, bali pia ni kudhihirisha kiwango cha hila na chuki aliyonayo kwa kile alichofanya rais.

Wakati mwingine waweza kuwa na hoja nzuri, lakini ukaiharibu kwa lugha. Lazima ifike hatua tujue kuwa staha katika kukosoa ni sehemu ya msingi katika misingi inayojenga demokrasia.

Niseme tu kuwa si kweli hata kidogo kuwa ripoti ya Profesa Mruma haina maana kiushahidi. Ripoti hiyo ni ushahidi muhimu sana tena sana kuthibitisha udanganyifu wa Acacia. Kama leo kesi ya udanganyifu inasimama, ni ripoti ya kisayansi kama ya Mruma itakayotumika kuthibitisha uwepo wa udanyifu.

Lakini pia sisi huo ndio ushahidi wetu tuliokusanya, na wao kama wanao ushahidi mwingine unaosema hawajadanganya, basi watauleta- shida iko wapi? Iko wapi haja ya kuiita kamati iliyopata mamlaka ya rais takataka –‘rubbish’? Hakuna kabisa.

Je, tunayo matatizo ya sheria na mikataba kama wanavyodai?

Ndio tunayo. Yako mara mbili. Kwanza, sheria kama sheria kwa maana ya maudhui. Pili, sheria kwa maana ya usimamizi wake. Sheria kwa maana ya maudhui, yako maeneo yanayohitaji marekebisho na siyo sheria nzima.

Sheria hiyo ya Madini namba 14/2010 inaweza kurekebishwa maeneo yanayohusu leseni za madini, haki za kumiliki madini na ardhi yake, mrahaba na kodi na ile sehemu ya 10 inayoongelea adhabu, nk. Huo ni upande wa maudhui.

Kuhusu sheria upande wa usimamizi. Tatizo la usimamizi wa sheria ni kubwa kuliko upungufu ulio katika sheria yenyewe (maudhui). Kwa mfano, hii sheria iliyopo tunayosema ina upungufu, hakuna popote inaposema tuibiwe hata hicho kidogo tunachotakiwa kupata. Lakini tunaibiwa. Tatizo ni nini kama si usimamizi?

Hata tukitunga hiyo sheria mpya na kila mtu akaikubali, kama hatuna mtu wa kuisimamia ni kazi bure. Kwa hiyo tunahitaji mtu wa kusimamia sheria kuliko tunavyohitaji sheria yenyewe. Na dalili zote zinaonyesha kuwa mtu huyo tayari tumempata na sasa tunaanza kuondokana na tatizo hili. Mikataba nayo halikadhalika inahitaji kupitiwa kimaudhui pia ipate msimamizi.

Tatizo la akina Lissu katika hili ni kutaka kutwambia kuwa kwa kuwa tuna matatizo ya sheria na mikataba, basi haturuhisiwi kuzuia na kudhibiti hata wizi ambao tumebahatika kuugundua na kuuona. Ni upotofu na bila shaka ni hapana. Wizi huu tunaushughulikia na hayo mengine ya sheria na mikataba nayo muda unakuja yatashughulikiwa.

Kitendo cha rais kuunda kamati ya pili ya wachumi na wanasheria ni ushahidi kuwa tayari tatizo la sheria na mikataba limeanza kumulikwa rasmi.

Je, mchanga kuhakikiwa na TMAA kunafuta udanganyifu wao?

Lissu anasema kuwa mchanga huo ulihakikiwa na TRA, TMAA, n.k na kuwa zote hizi ni taasisi za Serikali na hivyo kuwaambia tena wameiba ni kuwakosea. Hivi kwani tunaposema kosa la ACACIA ni kutufanyia udanganyifu maana yake nini?

Maana yake si ni kwamba waliidanganya Serikali? Na Serikali si ni TRA, TMAA, nk? Sasa maajabu yako wapi? Kosa la ACACIA ni hilo kuzidanganya hizo mamlaka za Serikali wakati wa ukaguzi.

Kwa hiyo tunaposema wametuibia maana yake walizidanganya mamlaka hizo. Sisi hatujui walitumia njia gani, iwe rushwa au vinginevyo- sisi hatujui. Tunachojua ni kwamba tulichokuta wanachukua ni tofauti na kile walichosema wamechukua; jambo ambalo ni kosa. Iko wapi hoja hapo?

Mwisho ni kuwa tuache kupinga na kulalamikia kila kitu. Hili hatutaacha kulisema hata zipite karne 100. Madhali linaendelea kuwepo, tutaendelea kulikemea. Pia kurejearejea historia mara mwaka 1998 tulishauri hivi, mara vile nk. haina nafasi wala msaada kwa sasa.

Tumeshampata mtu wa kutushika mkono. Kazi yetu ni moja tu- kuungana naye kwa kuchangia utaalamu ili tutoke hapa tulipo. Kama huna utaalamu hata kumpa moyo nao ni mchango. Kama yote huwezi ni heri kukaa kimya kuliko ukabwabwaja.

Maajabu ni kutumia miaka zaidi ya 18 ukilalamikia jambo, halafu akatokea mtu wa kulitatua jambo hilo, badala ya kushirikiana naye, wewe ukafungua tena mlango mwingine wa malalamiko kulalamikia tena kile kile ulichopigania kishughulikiwe. Ni maajabu yanayostahili kuingia kwenye maajabu ya dunia!

Mwandishi wa makala hii, Bashir Yakub, kitaaluma ni mwanasheria. Anapatikana kupitia namba 0784482959.
Kama una copy ya mkataba kati ya gvt na sijui barick au acacia turushie humu. Halafu nani tunamshitaki hapa na kwa nini. Je wale wanaochimba kule chunya na kwingineko hawa na nongwa nasi. Vipi uranium, tanzanite vipi gas. Nasema ukichaguliwa kuwepo kwenye kamati ya usuluhishi wa hili jambo tumekwisha.
 
Mwambie amesikika! Yakub asipige kelele sana! Mkuu wa kaya kasema jamaa watalipa pesa yote.
.

Bora zije aisee ili ziendeshe nchi japo kwa miaka 20.

Hivi zikija zile bado tutaendelea kulipa kodi hizi za kiuwendawazimu?
 
Back
Top Bottom