Sijaridhishwa na Namna Waandishi wa Global walivyomhoji Binti aliyedai amebakwa!!!

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
GLOBAL PUBLISHER MUMETUMIKA KUMUSAFISHA PROF KAPUYA!!
Mimi nimesikitishwa na uandishi uliofanywa na magazeti ya Global Publisher baada ya kumhoji anayeitwa Binti aliyezaa na Kapuya.
Kwanza kabisa Prof Kapuya ni mtendaji wa Serikali kupitia Chama tawala ambaye anatakiwa kuwa mfano kwa maadili ya Jamii hivyo tulitegemea gazeti lihoji mambo kadhaa yakiwemo yafuatayo:
Part1:
Mwezi Februari mwaka huu, mtu asiyefahamika alienda nyumbani na kutelekeza gari aina ya T.199 BGY Mercedes Benzi ya Blue wakati wanafunzi hao wakiwa shuleni, kisha kuacha ufunguo kwa jirani yao kwa maelekezo kuwa wakifika awapatie.Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo, 24 Januari 2013, alifika mtu nyumbani kwao mtu mmoja (jina tunalihifadhi) na kujitambulisha kuwa yeye ni jambazi na kuwa alitumwa kwenda kuwaua
Hapa tunataka ukweli nani mumiliki wa gari hii na Prof Kapuya ,alikuwa anatuma la nini gari hii kwa mototo mdogo kama hajazaa naye??. Ni kwa nini Pro Kapuya anakuwa Munyonge kwa motto mdogo tena Yatima??? Ikumbukwe kuwa kama Prof Kapuya haukuwatuma majambazi hawa kwa nini anaendelea kutuma msg za kutishia kua ???? Ninani aliyejuu ya sharia??? Ni nani mwenyehaki ya kumuua mtu mwingine???Kama serikali hiwezi kushughulikia vitisho vya Prof Kapuya maana yake ni kwamba Serikali haiwezi kuwakamata wauaji wowote wakiwemo waliomuua Dkt Mvungi
Part2
Alfajiri saa 11:21 kupitia simu yake ya mkononi yenye namba 0784993930, Profesa Kapuya alituma ujumbe ufuatao kwa mtoto huyo: "chagueni kunisubiri tuje tuongee au mnataka kufa?"
Baadaye saa 1:07 asubuhi, alituma ujumbe mwingine kutoka simu hiyo hiyo kwenda kwa mtoto huyo, ukisema: "Mkiuawa, itakuwa nzuri, itawapunguzia gharama za kuishi. Usitake kugombana na serikali, mtoto mdogo kama wewe. Sisi ndo wenye nchi yetu.
"Mwambieni Mbowe mwenye hilo gazeti awape nyumba ya kuishi.

Si mmemuingizia hela leo? Mnatumika bure watu wanaingiza hela nyingi, mmenitibua lazima niwauwe wiki hiii haitaisha, nitapanga kambi popote. "Jana si wamekuficha? Tuone kama utalindwa milele. Kazi ya kulindwa imeisha, maana wameshatengeneza hela. Lazima mvae sanda. Hilo sio ombi, ni wajibu wenu. Mnajitia mafia watoto sio? Watoto wetu wanauza unga, nani anawakamata? Nani atapigana nasi?"
Manenno haya yametolewa na Prof Kapuya tena kupitia simu yake na ushihidi umethibishwa na TCRA kwamba Prof Kapuya ametukana na kutihia.
Kwa ufupi hapa Prof Kapuya hajamtishia Binti huyo peke yake bali kawatishia na waandishi Jambo ambalo ni hatari.Suali ni kwanini Kapuya anawatishia waandiushi wa Tanzania Daima na hawatishii waandishi wa glbal Publisher????Ni kwanini waandishi wa Glbal wafanye harassment wakati wa kumuhoji bint huyo???


Part 3
Hata hivyo, baada ya kuhisi kuwa watoto hao wamedhamiria kumchukulia hatua, na wamewasiliana na taasisi mbalimbali za kiraia na serikali zenye uwezo wa kumtia adabu, mbunge huyo alimtumia mtoto huyo ujumbe wa kuonyesha alikuwa anafikiria kunywa sumu. Ujumbe huo uliotumwa kwa mtoto huyo saa 11:2 3 ulisema: "nimwakosea sana, acha nife mie nakunywa sumu nijiue, na nyie mje mnizike."
Hasira za Profesa Kapuya dhidi ya mtoto hao zilitokana na hatua ya mtoto huyo na dada yake kufichua unyama wanaodai kutendewa na mbunge huyo, ambaye amewahi kushika nyadhifa kadhaa za uwaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.
Tangu alipogundua kuwa mtoto huyo alizungumza na gazeti hili juzi, saa 5:17 usiku wa kuamkia jana alituma ujumbe usemao: "Si mpo Bilz? Sasa tupo pamoja na nyie mpaka usiku." Baadaye saa 5:31 alituma ujumbe huu: "Hivi hamkubali kushindwa? Leo ulifuata nini ofisi ya CCM?"

Hapa inaonyesha Prof Kapuya yupo juu ya CCM na Serikali !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Part4
Mwanafunzi huyo alisema baada ya kutambulishwa aliitwa katika hoteli moja jijini Dar ambapo baada ya kufika mapokezi wafanyakazi wa hoteli hiyo walimkataza kuingia chumbani katika maana kwamba umri wake alikuwa mdogo (mwaka 2011 alikuwa na miaka 14), lakini Kapuya aliamrisha aje chumbani pamoja na dereva na kumwingiza kwa nguvu. Akiwa chumbani alimlazimisha kulala naye kisha kumpa sh laki saba, badala ya sh elfu sitini na saba kiasi ambacho kilikuwa ndio mahitaji halisi ya ada.
Mwanafunzi huyo amesema baada ya muhula mmoja aliitwa tena na mbunge huyo katika Jengo la Biashara Complex lililoko Mwananyamala tarehe 3 June 2012, ambapo pia alimlazimisha kulala naye kwenye zulia la ofisi yake, kisha kumpa sh 350,000/.
Alisimulia kwamba wakati anatoka kwa huzuni ofisini kwa mbunge huyo, mmoja wa wahudumu wa hapo alimuuliza kwanini anatoka kwa huzuni, alimweleza kisa hicho, na huyo mama aliangua kilio kwa kumwambia "mwanangu umekufa pole tu, huyu baba ni muathirika wa ukimwi". Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa vile alilia na kufanya fujo hapo mapokezi hadi alipokamatwa na walinzi wa kisha kupelekwa kituo cha polisi kufunguliwa mashtaka, lakini akiwa polisi alipoeleza mkasa wote, Polisi walilazimika kumwita Kapuya na wakawasuluhisha kwa makubaliano kwamba Kapuya atakuwa anamlipia ada, na kumpa pesa za matumizi sh. laki tatu kila mwezi, jambo ambalo amekuwa akilitekeleza kupitia simu yake ya mkononi 0755993930.
Ujumbe huo kutoka simu namba 0784993930 inayomilikiwa na Kapuya kwenda kwa namba inayomilikiwa na binti huyo, unasomeka hivi: "Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Samweli Sita asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi! We unadhani nani atakayenifunga? Ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone!" inasomeka sehemu ya ujumbe huo unaodaiwa kutoka kwa Kapuya.

Part5
Katika kuthibitisha kwamba Kapuya amekuwa na mawasiliano na binti huyo na kwamba anamjua tofauti na anavyodai kuwa hamjui, gazeti hili limenasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda kwa binti huyo.Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo. Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: Juma Kapuya(0755993930).
R93NY448 Imethibitishwa
Umepokea Tsh505,000

kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000
U26UG365. Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000
kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000
V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000
kutoka kwa JUMA KAPUYA
Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM
Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040
Kwa nini Kapuya akubali kumusaidia mwanafunzi huyo kwa njia ya simu badala ya kwenda kulipa moja kwa moja Shguleni??????????
First Name: Prof. Juma
Middle Name: Athumani
Last Name: Kapuya
Member Type: Constituency Member
Constituent: Urambo Magharibi
Political Party: CCM
Office Location: P.O. Box 11365, Dar es Salaam
Office Phone: +255 784 993930/+255 776 784185
Ext.:
Office Fax:
Office E-mail: jkapuya@parliament.go.tz
Member Status: Current Member
Date of Birth 22 June 1945
University College of Wales Aberystwyth
PhD (Botany)
1972
1975
PHD
University of Dar es Salaam
MSc. (Botany)
1971
1972
MASTERS DEGREE
University of Dar es Salaam
BSc. (Education) Hons
1968
1971
GRADUATE
Katholicke University, Nijmegen
Certificate
1982
1983
CERTIFICATE
International Atomic Energy Agency
Certificate
1986
1986
CERTIFICATE
MAMBO YA KUJIULIZA
1.Kapuya anasema huyo Binti ni mtu mzima nay eye amegundua hilo sasa kwa nini anaendelea kusadia mtu mzima wakati tayari ameshagundua hilo.
2.Kapuya anasema Binti ni tapeli sasa kwa nini anaendelea kumutumia msg tapeli?? Anaendelea kumtumia M-Pesa mtu tapeli???
Hivi CV ya kapuya ni ya mtu wa kutapeliwa???
Kwa nini akubali harakaharaka kuwa Binti ni tapeli???
3.Kama kapuya ambaye ni Prof na aliyewahi kuwa waziri anaweza kutapeliwa kirahisi namna hiyo basi nchi hii ipo Gizani!!!
4.Ni kwa nini serikali isichukue hatua kwa lugha za vitisho za kuua zinazotolewa na Mtu wao???
5.Kwa nini Bi Helen Bisimba yupo Kimya kwa vitisho vya mauaji kama haya???.

WITO WANGU NI KWAMBA NCHI HAIWEZI KUONGOZWA NA WATU WABABE KAMA KAPUYA HARAFU RAIS ANANYAMAZA KIMYA>
SASA TUNA ANZA KUAMINI KUWA SERIKALI ILIYOKO MADARAKANI INAFANYA BIASHARA ZA DAWA ZA KULEVYA NA WATOTO WAO HAWAKAMATWI NA WAKIMATWA WANATOLEWA!!!
MTANDAO WA MAHAKIMU NA MAJAJI WOTE WANAOLALAMIKIWA UMETHIBITISHWA NA MANENO YA KAPUYA!!!!!!!!!!!!
 
Kifupi ni kwamba wamem- provoke ili awajibu kwa jazba wapate kuandika wanayoyajua wao. Hawa waandishi wanadhani Tanzania ya 1964 ni hii ya leo.

Ili wajue kosa hilo ni kosa ni pale wakipandisha umri ya huyo aliyebakwa hata awakifikisha kuwa ana miaka 55 bado Kapuya ana kesi ya kujibu.
 
Tanzania ni nchi yetu, magazeti ya udaku/vichochoroni/chooni/pendwa ndio magazeti yetu, na hao ndio waandishi wetu!.
Pasco
 
Mkuu hapo umepotoka labda ulitaka mahojiano yambane prof Kapuya, mwandishi alikuwa Ana balance, mala anasema siyo yeye anamajina Mengi, suala la kufungwa hajakataa, ni mwanafunzi gani mfungwa? Nilikuwa upande wake lakini kwa sasa nimesha mshtukia ni taperi kama taperi mwingine wa kike wa kujaribu kupata amount ya pesa kwa tishio la kukuharibia jina kwa watu maarufu na kwa watu wa kawaida anakuharibia kwa mkeo na magazeti ya udaku kama hivi,. Ni Malaya huyo labda tumtete huyu binti kwa mambo ya kisiasa tu.

Body without head
 
Tanzania mi mchi yetu, magazeti ya udaku/vichochoroni/chooni/pendwa ndio magazeti yetu, na hao ndio waandishi wetu!.
Pasco

natamani ningejua elimu ya hao waandishi ndio ningeridhika
 
Kuna kumbukumbu ya KAPUYA kumtumia pesa huyu binti kila mwezi. Pia KAPUYA hakanushi kufanyiwa kikao cha upatanisho Polisi Osterbay.
Anang'ang'ania hoja ya binti ni mtu mzima, bila Shaka anataka kutumia upenyo huo kuchomoka.
Suala la kuwekwa ndani (gerezani) pamoja na madai mengine hakuondoi hoja ya msingi ya kubakwa kwake na KAPUYA.
Ni vema tunaojadili tubaki kwenye hoja ya msingi ya ubakaji kwa kufuata kumbukumbu za tukio kuripotiwa Polisi Osterbay na kufanyiwa upatanisho pamoja na ushahidi mwingine uliotolewa kuthibitisha ubakaji uliofanywa na KAPUYA.
Nitarudi.
 
natamani ningejua elimu ya hao waandishi ndio ningeridhika
Kwa uandishi wa habari magazetini, sifa ni kujua kusoma na kuandika!.
Utangazaji redioni sifa ni kujua kusema na kusikia
Kwa Utanhazaji wa TV, ujue kusema, kusikia na sura ya kutazamika!.
Pasco.
 
Jamani tanzania makanjanja mnatupoteza oneni aibu na ukanjanja wenu kubakwa ni mwanafunzi tu hata kama anawajukuu si kabakwa
 
mkuu hapo umepotoka labda ulitaka mahojiano yambane prof kapuya, mwandishi alikuwa ana balance, mala anasema siyo yeye anamajina mengi, suala la kufungwa hajakataa, ni mwanafunzi gani mfungwa? Nilikuwa upande wake lakini kwa sasa nimesha mshtukia ni taperi kama taperi mwingine wa kike wa kujaribu kupata amount ya pesa kwa tishio la kukuharibia jina kwa watu maarufu na kwa watu wa kawaida anakuharibia kwa mkeo na magazeti ya udaku kama hivi,. Ni malaya huyo labda tumtete huyu binti kwa mambo ya kisiasa tu.

Body without head
mimi pia nilishawahi kufungwa nikiwa darasa la tatu, so jifunze kujenga hoja na kujadili kwa umakini zaidi.
 
Back
Top Bottom