Sijapenda nilichokiona kwenye msiba wa Mzee Mkapa

Hujui taratibu za kijeshi kaa kimya

Askari akifariki huwa anazikwa kwa kufanyiwa taratibu zote na wenzake. Na kama hujui tu yaani hata kama ni kijijini ndani remote kiasi gani lazima wafike mpaka wahakikishe kaburi la "mwenzao" linefukiwa ndio wanamaliza taratibu zao na kukabidhi kwa familia. Jeneza lina Bendera ya Taifa, msalaba, na kwa askari na kofia na buti vinawekwa pale juu navyo wanashika wenyewe wakiwa katika uniform

Sasa hapo kwa askari wa kawaida sembuse huyu alikua Amir mkuu?

Vipi na kwenye ndoa je, unataka tusivae staff suit na kitara kiunoni kwenda nacho kanisani?
 
Samcezar,

Aliyefariki ni Rais (Kumbuka alistaafu Mkapa ila sio Cheo chake). So Bro hata Waziri Mkuu haruhusiwi kukamata ule Msalaba. Alikuwa amiri jeshi mkuu. Ndio baba wa wanajeshi. So watoto wake lazima wamshikie kila kitu. Hata wahudumu wa Ikulu ni wanajeshi.
 
Nabii Yeremia aliwaita watu wa namna hiyo kuwa wamefunga ndoa ya uzinzi na mfalme wa kaskazini. Kwamba wamekuwa makahaba. Mimi sio mwinjilisti lakini humanisha kuwa Kanisa limepotoka.
 
Unajua maana ya madhabahu? Sadaka gani ya kuteketezwa inatolewa hapo?? Tofautisha mimbari na madhabahu.. halafu hapo ni uwanja wa uhuru siyo St Peter's hapo

JamiiForums mobile app
Madhabahu yalikuwa ya kutolea sadaka za kuteketeza wanyama watakatifu. Baada ya kifo cha Yesu hakuna tena picha wala mfano bali sadaka halisi alikuwa ni Yesu mwenyewe. So mtoa mada hajakosea bado inaitwa madhabahu tofauti sisi hatuchinji.

Unapenda kukosoa vitu wakati ni mweupe kichwani. Unaambulia aibu tu.
 
Huyu ni Raisi mstaafu na viongozi mbalimbali watashiriki pale ni lazima ulinzi uwe imara na madhubuti wenye hila wapo . Hoja yako siungi mkono
 
Kweli bado JF watu wengi uelewa ni mdogo-umeongea uhalisia kabisa!
1595757128550.png
 
Back
Top Bottom