Sijapenda: Naibu katibu mkuu wa Chadema mh Benson Kigaila kufanya kazi ya Utarishi!

Hivi kusambaza barua za ofisi kutoka Chadema kwenda taasisi nyingine kama vile Bunge NEC au kwa Msajili wa vyama vya siasa ni kazi ya Naibu katibu mkuu?

Chadema heshimuni vyeo vya Watendaji wenu
Wewe tambua tu ya kwamba kutokana na unyeti wa barua hiyo, ilimpasa aipeleke yeye mwenyewe. Si kila barua inapaswa kupelekwa kwa njia ambazo zimekaririka. Mathalani, huwezi kupeleka posa kwa njia ya utarishi.
 
Hivi kusambaza barua za ofisi kutoka Chadema kwenda taasisi nyingine kama vile Bunge NEC au kwa Msajili wa vyama vya siasa ni kazi ya Naibu katibu mkuu?

Chadema heshimuni vyeo vya Watendaji wenu
Unakumbuka kuna barua moja kutoka tume ya uchaguzi au msajili wa vyama vya siasa kwenda ofisi za CHADEMA ilipelekwa na nani tena kwa pikipiki a.k.a bodaboda!?

Kuna wakati unapotaka kuhakikisha barua imepokelewa kwa 100% na wahusika lazima ufanye hivyo. Angepelekwa messenger au sijui ndiyo huyo tarishi, hiyo barua hadi leo ingekua haijulikani iliko. Unamjua Benson Kigaila, lazima wangepokea tu. Haya yote najua unayajua, pia najua pasi na shaka kwamba hujapenda kupokelewa kwa barua hii, kwa sababu mpira umerudishwa kwa Bunge na Serikali waucheze.

Tusubiri matokeo.
 
Kila jambo linafanyika kulingana na wakati na uzito wake. Kwa uzito wa barua ya safari hii na wakati wenyewe, imebidi ipelekwe hivyo.

Mpira umerudishwa kwa Bunge na Serikali, tusubiri waucheze.
Katiba ya Chadema inasema Rufaa zitasikilizwa ndani ya siku 30
 
Hivi kusambaza barua za ofisi kutoka Chadema kwenda taasisi nyingine kama vile Bunge NEC au kwa Msajili wa vyama vya siasa ni kazi ya Naibu katibu mkuu?

Chadema heshimuni vyeo vya Watendaji wenu
Ungekuwa unajua thamani ya barua hizo usingeandika ujinga huu, unadhani ni sawa na zile unazotongozea mabaamedi.
 
Hivi kusambaza barua za ofisi kutoka Chadema kwenda taasisi nyingine kama vile Bunge NEC au kwa Msajili wa vyama vya siasa ni kazi ya Naibu katibu mkuu?

Chadema heshimuni vyeo vya Watendaji wenu
Moderators, tusifanye JF iwe kijiwe cha clowns! Tunaomba thread za kama hizi mzifutilie mbali. Unajua mwanzisha thread ni clown fulani anayedhani watu wanafurahishwa na thread zake nyingi anazoanzisha wanavyojibizana naye hivyo anafanya kazi ya kuanzisha thread zisizo na maana kila saa. Paw YinYang do what you have to do, because clowns never knows theirs limitations if you give them too much freedom
 
Unatesekea wapi?

Karibu tena.
 
Back
Top Bottom