MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,751
- 48,392
Mojawapo wa vitu nilivyoshuhudia sana kwa Watanzania, huwa wana unafiki uliopitiliza, yaani jamaa huongea kistaarabu na wanaweza wakakakusifia mpaka ufurahi sana ila subiri uondoke, utasemwa mpaka basi. Watakuita mkuu, wataongea na wewe kwa furaha mpaka uone kama vile uko bingu nyingine, watakupa shikamoo kwa furaha nyingi tu, ila majungu na machungu waliyosheheni kwa ajili yako, dah!
Na ndio tofauti kubwa na Wakenya, maana hapa Kenya huwa unaambiwa kama ilivyo, ukizingua unaambiwa, umeze uteme utajijua mwenyewe ila kama uko uchi utaambiwa tu.
Marehemu rais Magufuli aliogelea kwenye sifa za Watz, waliimba mapambio yake tu, kila siku walimfanya ajione kama mtume fulani hivi, hakuna aliyediriki kusema vinginevyo, labda yule Lissu aliyeondolewa kwa marisasi.
Sasa leo hayupo tena hao hao waliomlamba miguu wameibuka na kuanza kuponda kila alichokifanya, kumbe walikua wanaumia kimya kimya wote. Kuna spika tena mwandani wa karibu sana wa marehemu juzi ameomba michakato ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo izinduliwe, kuna huyu mwingine naye ameponda mradi wa ufuaji umeme, ule wa Stiegler, na watatendelea kuongea wengi sana, kwanza sasa hivi wanajadili upigaji uliovumbuliwa na ukaguzi wa CAG, upigaji ambo haujaonekana tena kwao huko, yaani kipindi chote cha JPM jamaa wamepiga hela ufisadi wa kupitiliza.....kha hawa bana.