Sijapata kuona wanafiki kama Watz, haya huyu muingine (aliyekua timu misifa) aibuka na kuponda mradi wa ufuaji umeme wa Stiegler

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,733
48,293
Mojawapo wa vitu nilivyoshuhudia sana kwa Watanzania, huwa wana unafiki uliopitiliza, yaani jamaa huongea kistaarabu na wanaweza wakakakusifia mpaka ufurahi sana ila subiri uondoke, utasemwa mpaka basi. Watakuita mkuu, wataongea na wewe kwa furaha mpaka uone kama vile uko bingu nyingine, watakupa shikamoo kwa furaha nyingi tu, ila majungu na machungu waliyosheheni kwa ajili yako, dah!
Na ndio tofauti kubwa na Wakenya, maana hapa Kenya huwa unaambiwa kama ilivyo, ukizingua unaambiwa, umeze uteme utajijua mwenyewe ila kama uko uchi utaambiwa tu.

Marehemu rais Magufuli aliogelea kwenye sifa za Watz, waliimba mapambio yake tu, kila siku walimfanya ajione kama mtume fulani hivi, hakuna aliyediriki kusema vinginevyo, labda yule Lissu aliyeondolewa kwa marisasi.
Sasa leo hayupo tena hao hao waliomlamba miguu wameibuka na kuanza kuponda kila alichokifanya, kumbe walikua wanaumia kimya kimya wote. Kuna spika tena mwandani wa karibu sana wa marehemu juzi ameomba michakato ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo izinduliwe, kuna huyu mwingine naye ameponda mradi wa ufuaji umeme, ule wa Stiegler, na watatendelea kuongea wengi sana, kwanza sasa hivi wanajadili upigaji uliovumbuliwa na ukaguzi wa CAG, upigaji ambo haujaonekana tena kwao huko, yaani kipindi chote cha JPM jamaa wamepiga hela ufisadi wa kupitiliza.....kha hawa bana.

Watanzania ni watu wanafiki na waoga
sana. Mbona wanangoja mtu afariki ili waanze kumponda? Kama wao ni wanaume kamili nilitegemea wangemponda akiwa bado yupo hai. Mbona huku Wakenya wanamponda Uhuru kwa sababu ya madeni mengi anayochukua kila siku na wala hatufichi mapungufu yaliyo huku? Hawa watu wapunguze uoga na unafiki. Ponda mtu akiwa bado yupo hai ili ajuwe mapungufu yake.
 
Halafu kitu cha hovyoo zaidi ni yaani hao wanaomponda marehemu leo hii, muda akiwa hai usingewaambia kitu, walikua wanamsifia tena kwa mapovu, yaani ungedhani wapo radhi kufa kwa ajili yake, ndio unafiki uliokubuhu. Kha! Magufuli kama akiwa huko ana uwezo wa kuangalia duniani aone yanayotendeka.....hehehe
 
Watanzania ni watu wanafiki na waoga
sana. Mbona wanangoja mtu afariki ili waanze kumponda? Kama wao ni wanaume kamili nilitegemea wangemponda akiwa bado yupo hai. Mbona huku Wakenya wanamponda Uhuru kwa sababu ya madeni mengi anayochukua kila siku na wala hatufichi mapungufu yaliyo huku? Hawa watu wapunguze uoga na unafiki. Ponda mtu akiwa bado yupo hai ili ajuwe mapungufu yake.
Tony kila Mara ninatumia neno kwamba wakenya hamna akili na uwezo wenu wa kufikiria ni mdogo, japo ninajua sio vizuri kutumia msemo huu, lakini ninalazimika kutumia kutokana na ujinga wenu

1)Huyo Prof. Muhongo hajapinga wala kuponda mradi wa uzalishaji umeme unaoendelea, huyo aliyefungua huu uzi unamjua vizuri kichwa chake, hupaswi kumsikiliza bila kujiridhisha, huyo ni mkikuyu "hard liner".

Alichosema ni kwamba, katika miradi yenye kurudisha pesa haraka, umeme wa kuzalisha kwa maji, haumo kawaida unachukua muda mrefu kurudisha pesa, Kama tunataka kufikia per capital ya $2500 by 2025 tunahitaji kuongeza bidhaa mpya zenye kutoa faida haraka.

Kwamba wakenya hawajikombi kwa viongozi, mumesahau Sonko alivyokua akimsifia Uhuru Kenyatta wakati alivyokua Governor wa Nairobi?, alivyoondolewa kazini umesikia aliyosema kuhusu ufisadi wa Uhuru Kenyatta na familia ya Kenyatta, kwanini asingelisema alipokua Governor.

Rutto sasa hivi anailaumu serikali kwa kukopa, wakati yeye ni Naibu rais, kabla ya ndoa yake na Uhuru kuvunjika alikua akitetea kila jambo lililifanywa na serikali.
 
Wakuu,,, hii imekaaje, kama si unafik ni nini???
mkorinto, passioner255, lwiva, Mwanzi1, babayao255, luangalila, Naby Keita tuusan, Darmian
»»»
KATIKATI YA MAJONZI:
Ndiyo Nagutuka kuwa Tuliyempoteza ni Shujaa Aliyepitwa na Wakati!
Anaandika Peter Simon Msigwa
Sitaki kuwabishia wale wanaomwita Shujaa. Tofauti yangu na wao ni fikra tu. Kuna fikra za kisasa na fikra za kizamani!
Ukweli ni kwamba Mpendwa wetu JPM alikuwa ni mtawala wa zamani sana aliyejikuta amepata fursa ya kutawala nchi katika zama za sasa. Hakuwa "compatible" na ulimwengu wa leo hata kidogo!
Kwanini nimsingizie? Mifano ipo mingi sana. Nigusie machache:
1. Kwanza, lugha zake za kuita wazungu mabeberu ni lugha za miaka ya hamsini na miaka ya sitini. Ni lugha zilizotumiwa na vijana wa zamani wa kiafrika, akina Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Jomo Kenyatta, Patrice Lumumba na wengine wakati wakipigania uhuru wa nchi zao kwenye miaka ile ya 1950's na 1960's.
Kusingizia wazungu kuwa ndio wanaokwamisha uchumi na maendeleo ya Tanzania hasa katika kipindi hichi cha takribani miaka 60 baada ya uhuru ni kukosa maono na kushindwa kujua mahitaji ya sasa, vikwazo vya sasa na namna sahihi ya kukabiliana navyo!
Kutokujua kwake ajenda za kimataifa zinazohusu uchumi na changamoto za dunia, kuliifanya Tanzania ionekane kama kisiwa na kituko duniani!
Kwa hiyo, kwa watu wote ambao walidhani na bado wanadhani tupo kwenye zama hizo, basi JPM ni Shujaa wao! Shida ni moja tu, ni Shujaa aliyepitwa na wakati! Mashujaa wa leo hawapambani tena na Wazungu kwa kususa kupanda ndege za kwenda Ulaya au Marekani kwenye Mikutano ya wakuu wa nchi, wala hawapambani kwa kufokafoka na kutumia lugha mbaya mbaya za kizamani! Mashujaa wa leo huvutia, husukuma na kulinda maslahi ya kiuchumi ya nchi zao kwa kutumia maarifa na weledi wa "diplomasia ya kiuchumi" (economic diplomacy). Kwa uelewa zaidi kuhusu diplomasia ya uchumi, tafadhali soma hotuba yangu niliyoitoa katika Bunge la Bajeti la mwaka 2018/19 nikiwa Waziri Kivuli na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
2. Pili, uamuzi wake wa kuhimiza matumizi ya "kupiga nyungu" kuliko njia za kisayansi za kupambana na Corona, nao pia ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa kabisa. Shida ni moja tu, ulikuwa ni ushujaa uliopitwa na wakati. Historia inatukumbusha kuwa ushujaa kama huo alishafanyika miaka mingi sana nyuma, enzi zile Mzee wetu Kinjekitile Ngwale alipohamasisha wapiganaji watumie maji katika kukabiliana na risasi za wazungu kwa Imani kuwa risasi zao zingegeuka maji na kutowadhuru. Matokeo ya ushujaa wa Kinjekitile kwenye vita vya maji maji na matokeo ya ushujaa wa JPM kwenye vita ya Corona yote tumeyaona.
3. Tatu, alikuwa ni mtawala aliyekuwa na mamlaka na uhuru wote wa kiserikali ikiwemo kukusanya kodi, kuandaa dira, sera, mipango, bajeti na kutekeleza miradi ya maendeleo. Ajabu, bado eti aliamini wapinzani ndio wanaozuia na kukwamisha maendeleo ya Tanzania! Alipata kusema mbunge anayepinga bajeti ya serikali yake sio mzalendo, jambo ambalo Spika, Naibu Spika na aliyekuwa Waziri wa Fedha walikubaliana naye. Kwake yeye uzalendo ulikuwa na maana moja tu - nayo ni kuunga mkono fikra na maamuzi yote ya Rais! Kila aliyekwenda kinyume naye alishughulikiwa.
Wakati wa utawala wake mambo mengi yaligeuka kichwa chini miguu juu. Kwa mfano, baadhi ya majaji na mahakimu walishindwa kutoa hukumu za haki!
Polisi walitekeleza amri zisizo halali!
Baadhi ya viongozi wa dini walifurahia kuitwa kwenye dhifa za kitaifa na matukio ya kuipigia debe serikali wakisahau wito wao Mkuu wa Kitume!
Wandishi wa habari waliweka kalamu zao chini au walijikuta wakiandika vitu ambavyo nafsi zao ziliwasuta!
Baadhi ya wasanii walikuwa wasanii kweli kweli kwa maana halisi ya neno usanii! Walijua nini Shujaa anataka (sifa). Nao hawakufanya ajizi. Walitumia usanii wao kikamilifu kumpatia kile alichotaka hata kama hakikuwa cha kweli!
Hakika, hichi kilikuwa ni kipindi ambacho ujinga na unafiki vilipewa hadhi kubwa na kuketishwa kwenye kiti cha enzi, huku ukweli na akili vikifukiwa ardhini!
Haikuwa kazi rahisi kuibadili nchi kichwa chini miguu juu kiasi hicho! Kwa hiyo, sitaki kuwa mbishi. Ni kweli alikuwa Shujaa. Shida ni moja tu, alikuwa ni Shujaa aliyepitwa na wakati!
Ushujaa kama huu wa JPM wa "kutaka lake liwe tu", unapatikana sana katika hadithi za wafalme wa zamani kwenye simulizi kama za "Alfu Lela Ulela", "Hekaya za Abunuwasi", "Mfalme Juha" n.k. Wafalme walikuwa wakitaka lao liwe basi lazima liwe hata kama ni fyongo.
Kinyume chake, Mashujaa wa leo hawaongozi tena nchi kwa kulazimisha fikra zao pekee, bali kwa kupokea ukosoaji na ushauri wa kutosha.
Hii ndiyo kusema kuwa utawala wa JPM haukupaswa kabisa kuwepo katika dunia ya sasa. Ulipaswa uwepo kabla ya Nyerere au labda kidogo baada ya zama za kina Mzee Kinjekitile Ngwale.
JPM alichelewa sana kuboresha fikra na mitazamo yake ili kuendana na mahitaji ya dunia sasa. Ni jambo la kuhuzunisha kuwa hadi umauti unamfika bado hakuwa amefanikiwa ku- upgrade software yake. Aliendelea kutawala nyuma ya wakati katika kipindi chote cha utawala wake. Kwa maneno mengine alikuwa "the most incompatible and irrelevant ruler of our contemporary world".
Wengine wanamwita Shujaa wa Afrika. Wengine Mtakatifu lakini ukweli usiokufuru ni kwamba JPM alijulikana sana duniani sio kwa umahiri wake, bali kwa kutokujua nini kinaendelea duniani! Matokeo yake akawa kituko, "the world laughing stock"
Utawala wa JPM umetufunza jambo moja kubwa na la msingi sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kwamba bado wapo watu wanaofikiri na kuenenda nyuma ya wakati. Tena miongoni mwao bado wapo wanaoweza kupata nafasi kubwa za uongozi hata kwa bahati tu kama alivyopata JPM. Wakipata nafasi hizo basi wanaweza kuirudisha nchi yetu nyuma ya wakati uliopo. Wakatenda mambo yaliyo kinyume na yasiyoendana kabisa na mahitaji ya sasa. Kwa hiyo, tunahitaji Katiba mpya kabisa na iliyo imara sana itakayoweka tunu, mifumo na misingi ya kumdhibiti kiongozi yeyote yule ili asiende nje sana ya matakwa na matarajio ya Taifa.
Tuache uvyama, tuna nchi ya kujenga. Tuandike Katiba Mpya ya kulilinda Taifa letu leo na kesho. Mashujaa wa zamani (kina JPM) bado tunao wengi huku mitaani.Tukifanya mchezo, ipo siku mmoja wa Mashujaa wa aina hii ataukwaa tena urais halafu tutaanza kujuta tena. Walisema Wahenga "Majuto ni Mjukuu mwishowe huja kinyume".
Hakika, tuliyempoteza ni Shujaa aliyepitwa na wakati. Nilipenda aendelee kuwa nasi duniani. Nilipenda abadilike na kuendana na dunia ya sasa. Lakini Mwenyezi Mungu alimpenda zaidi. Namshukuru sana kwa kutunyoosha. Namshukuru kwa funzo kubwa alilotuachia, ametupa fursa na namna ya kuimarisha mifumo na misingi ya nchi yetu vizuri. Kabla yake hatukuwahi kuona nyufa zilizopo katika Katiba yetu kiasi hichi! Ametusaidia kuonesha jinsi Taifa letu lilivyo legelege. Ahsante sana. Pumnzika kwa amani John Pombe Magufuli, ewe Shujaa wa Wakati Wako, Mwanahalisi wa Tanzania na Mpiganaji hodari wa Afrika kwa kadri ya fikra za wakati wako.
 
Mojawapo wa vitu nilivyoshuhudia sana kwa Watanzania, huwa wana unafiki uliopitiliza, yaani jamaa huongea kistaarabu na wanaweza wakakakusifia mpaka ufurahi sana ila subiri uondoke, utasemwa mpaka basi. Watakuita mkuu, wataongea na wewe kwa furaha mpaka uone kama vile uko bingu nyingine, watakupa shikamoo kwa furaha nyingi tu, ila majungu na machungu waliyosheheni kwa ajili yako, dah!
Na ndio tofauti kubwa na Wakenya, maana hapa Kenya huwa unaambiwa kama ilivyo, ukizingua unaambiwa, umeze uteme utajijua mwenyewe ila kama uko uchi utaambiwa tu.

Marehemu rais Magufuli aliogelea kwenye sifa za Watz, waliimba mapambio yake tu, kila siku walimfanya ajione kama mtume fulani hivi, hakuna aliyediriki kusema vinginevyo, labda yule Lissu aliyeondolewa kwa marisasi.
Sasa leo hayupo tena hao hao waliomlamba miguu wameibuka na kuanza kuponda kila alichokifanya, kumbe walikua wanaumia kimya kimya wote. Kuna spika tena mwandani wa karibu sana wa marehemu juzi ameomba michakato ya ujenzi wa bandari ya Bagamoyo izinduliwe, kuna huyu mwingine naye ameponda mradi wa ufuaji umeme, ule wa Stiegler, na watatendelea kuongea wengi sana, kwanza sasa hivi wanajadili upigaji uliovumbuliwa na ukaguzi wa CAG, upigaji ambo haujaonekana tena kwao huko, yaani kipindi chote cha JPM jamaa wamepiga hela ufisadi wa kupitiliza.....kha hawa bana.

Ila Prof Muhongo mnamuonea tu. Aliamua kukaa kimya tu ila hakuwahi kutoa pambio saana wala kusupport huo mradi.
 
13 May 2019
Tazama maelezo na mapendekezo ya Spika wa Bunge kuhusu uamuzi wa Serikali kusitisha mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo

Spika Ndugai Aishangaa Serikali Kusitisha Mradi wa Bandari Bagamoyo

Wow! Sasa ilitokeaje akaufyata, na ndio hicho yule CAG wa kitambo anasema wote hao ni wasaka tonge, wanasklizia upepo unakovuma......
 
Wengi wao walikuwa hawamkubali Jiwe sasa ile alikuwa katili libidi waigize Ili maisha twende ndio maana saizi wanafunguka

Jiwe mwenyew alikuwa jizi huku likijifanya kupigania wanyonge
 
Back
Top Bottom