Sijaona umuhimu wa sekretarieti ya ajira kurudia majina ya waliopata kazi katika matangazo mapya ya kazi

Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
Niende moja kwa moja kwa mada.

Inasikitisha na ni fedheha kwa taasisi kubwa ambayo iko chini ya ofisi ya Raisi kuwaongopea/ kuwahadaa watanzania katika kutenda haki katika kutoa ajira kwa Watoto wa maskini pasipo kuwa na ukiritimba wa namna yoyote.

Leo nilikuwa nikipitia tovoti ya Sekretarieti ya ajira nikakutana na Tangazo la waliofanikiwa kuitwa kazini kupitia kanzi data leo tarehe 25/01/2021 tangazo hili lina kumb. Na. EA. 7/96/01/K/22 na katika kupitia baadhi ya majina nikagundua kuna baadhi ya majina yameitwa tena ilihali watu hao wapo makazini tayari.

Nikafanya kutafuta tangazo la kazi la nyuma kidogo kwa walioitwa makazini tarehe 09/11/2020 likiwa na kumb. Na. EA. 7/96/01/K/317 nikapata kupitia kujiridhisha kama ni kweli hayo majina yapo nikakuta ndio yenyewe.

Ukipitia majina hayo katika " Pdf " nilizoambatanisha hapa chini utagundua ya kwamba tangazo la kazi lililotoka tarehe 09/11/2020 katika kurasa ya 29 - 31 utagundua wameyachukua majina hayo yaani wamefanya "Cut and paste" na kuja kuyabandika katika tangazo lililotoka leo tarehe 25/01/2021 na kuyaweka katika kurasa ya 8 - 11.

Kada zilizohusishwa ni kama zifuatavyo;
1. Shirika la ndege la Tanzania (ATCL)
2. Hospitali ya rufaa ya bugando (BMC)
3. Bohari la dawa (MSD)
4. Tume ya taifa ya umwagiliaji ( NIRC)
5. Chuo kikuu dodoma (UDOM)
6. Hospitali ya kikristo moshi (KCMC)
7. Taasisi ya elimu ya watu wazima (IAE)
8. Ofisi ya mkuu wa mkoa Katavi

Hili linaleta picha gani kwa taasisi hii;

1. Je? Wamekuwa wakiwaadaa watanzania kwamba wanatoa ajira ilihali ni uwongo maana kwa majina yaliyotoka leo katika kanzidata ni 75 ila kwa majina hayo yaliyo rudiwa ukihesabu ni watu 35 hili linatoa tafasiri ya kwamba watu halisi walioitwa kutoka katika ni 40 pekee ila hao 35 wengine ni kuitangaza awamu ya tano kuwa inaajiri ilihali ni uwongo.

2. Je? Nafasi hizo nafasi 35 ambazo zimerudiwa majina ni kwamba zitazibwa kwa kutumia majina mengine ambayo hawataki kuyaweka wazi? Hii inatoa tafasiri /inamaanisha kuna upendeleo ama harufu ya rushwa katika taasisi hii katika ugawaji wa nafasi.
 
Attachments

 • File size
  353.9 KB
  Views
  11
 • File size
  92.7 KB
  Views
  14

Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
Huwa wanatetewa sana humu ila ni makanjanja tu hawana la maana

NB: sijapakua pdf kuhakikisha, ila sekretariet ni makanjanja kama makanisa ya upako na uzima
Nimesikitika kwa kweli maana kiuhalisia mtu asipoitikia wito wa kuripoti kazini kama barua inavyosema basi nafasi hizo hupewa watu wengine sasa iweje kwa hili warudie majina yale yale ni kwamba watu wote waliowaita hawakuitikia wito wa kufuata barua zao kuanzia mwezi Novemba mwaka jana.

Hapa kuna harufu ya udanganyifu kwa umma kwamba serikali hii ina ajiri kitu ambacho sio kweli ama pengine kuna harufu ya rushwa chini kwa chini.
 
zipompa

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
7,409
2,000

naungana na ww yawezekana wanafanya.hivyo kumfurahisha mukuru kuwa nafasi za kazi zinatolewa
 
Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
naungana na ww yawezekana wanafanya.hivyo kumfurahisha mukuru kuwa nafasi za kazi zinatolewa
Yaweza kuwa hivyo pia kuhusu majina ambayo watu huitwa kazini na amamini sasa kuna janja nyingi sana hufanyika (Idadi ya wanaoitwa makazini ni chache kulinganisha na majina yanayotolewa).
 
Okwaaa

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
1,292
2,000
Niende moja kwa moja kwa mada.

Inasikitisha na ni fedheha kwa taasisi kubwa ambayo iko chini ya ofisi ya Raisi kuwaongopea/ kuwahadaa watanzania katika kutenda haki katika kutoa ajira kwa Watoto wa maskini pasipo kuwa na ukiritimba wa namna yoyote.

Leo nilikuwa nikipitia tovoti ya Sekretarieti ya ajira nikakutana na Tangazo la waliofanikiwa kuitwa kazini kupitia kanzi data leo tarehe 25/01/2021 tangazo hili lina kumb. Na. EA. 7/96/01/K/22 na katika kupitia baadhi ya majina nikagundua kuna baadhi ya majina yameitwa tena ilihali watu hao wapo makazini tayari.

Nikafanya kutafuta tangazo la kazi la nyuma kidogo kwa walioitwa makazini tarehe 09/11/2020 likiwa na kumb. Na. EA. 7/96/01/K/317 nikapata kupitia kujiridhisha kama ni kweli hayo majina yapo nikakuta ndio yenyewe.

Ukipitia majina hayo katika " Pdf " nilizoambatanisha hapa chini utagundua ya kwamba tangazo la kazi lililotoka tarehe 09/11/2020 katika kurasa ya 29 - 31 utagundua wameyachukua majina hayo yaani wamefanya "Cut and paste" na kuja kuyabandika katika tangazo lililotoka leo tarehe 25/01/2021 na kuyaweka katika kurasa ya 8 - 11.

Kada zilizohusishwa ni kama zifuatavyo;

1. Shirika la ndege la Tanzania (ATCL)
2. Hospitali ya rufaa ya bugando (BMC)
3. Bohari la dawa (MSD)
4. Tume ya taifa ya umwagiliaji ( NIRC)
5. Chuo kikuu dodoma (UDOM)
6. Hospitali ya kikristo moshi (KCMC)
7. Taasisi ya elimu ya watu wazima (IAE)
8. Ofisi ya mkuu wa mkoa Katavi

Hili linaleta picha gani kwa taasisi hii;

1. Je? Wamekuwa wakiwaadaa watanzania kwamba wanatoa ajira ilihali ni uwongo maana kwa majina yaliyotoka leo katika kanzidata ni 75 ila kwa majina hayo yaliyo rudiwa ukihesabu ni watu 35 hili linatoa tafasiri ya kwamba watu halisi walioitwa kutoka katika ni 40 pekee ila hao 35 wengine ni kuitangaza awamu ya tano kuwa inaajiri ilihali ni uwongo.

2. Je? Nafasi hizo nafasi 35 ambazo zimerudiwa majina ni kwamba zitazibwa kwa kutumia majina mengine ambayo hawataki kuyaweka wazi? Hii inatoa tafasiri /inamaanisha kuna upendeleo ama harufu ya rushwa katika taasisi hii katika ugawaji wa nafasi.
Mkuu kwanza hongera, umekuwa mfwatiliaji wa hadi deep kabisa. Ukweli sisi ambao hatuna ajira wanatuhadaa sana hawa watu. Inafika wakat hadi rafk zako au ndugu wanakuona ww ndo mbabaishaji kuwa kwanini wew huajiriwi wakat kila siku watu wanaajiriwa. Ukweli ni kwamba kati ya ajira 20 tegemea fake zipo 8, ni kama wameelekezwa kufanya hivo ili kumtukuza mkuu wa nchi anaye tekeleza miradi yenye gharama kubwa na kusahau kuna watu hususani masikini wanaumia sanaaa!
 
pido guy

JF-Expert Member
Apr 7, 2016
233
250
Mbaya.zaidi wanatoa tangazo la ajira mtu ana omba anaitwa kwenye usaili wakti tayari yupo kazini sijui huwa yale majina hawayapitii kwanza ili kuakiki kuwa hao waombaji waliomba kweli hawana kazi? wakti kuna watu wengi hawana kazi wako mtaani, wajaribu kuingia kwenye data base zao za taasisi husika ili kubaini na kuhakiki watu waliowaita kama kweli hawana kazi jamani unakuta mtu anatoka mamlaka hii anaenda mamlaka nyingine wakati taasisi ni moja.wafanye uajibikaji wasaidie wasiokuwa na ajira
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,055
2,000
Usaili wa Tanroads ulikuwa na mtoto wa Mfugale,Ndugu wa Spika wakiwamo watoto wengine wa vigogo yaani kwa haraka haraka nimewafahamu watu 9 ndugu wa vigogo yaani taasisi kama Tanroads,Tanapa,BoT nk zenye ulaji mkubwa sio rafiki kwa watoto wa maskini
 
keisangora

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,240
2,000
Wale waliopita Tanroads wamepita kwa maelekezo. Iweje watu alfu moja na zaidi wapitie siku hiyo hiyo kuwamaki afu watangaze watu wa kwenda oral.
Binafsi nilivyopata taarifa kuwa kuna watu wamependekezwa sikujisumbua utumie karibia gharama ya laki 3 afu achukuliwe aliyependekezwa.
Yaani ni bora wawe wanasema kuwa kuna vijana walikuwa wanafanya seap tunao hapa ofisini kwa iyo tunawatafutia permanent ajira ili wawe wanatusaidia hapa ofisini.

Yaani wamepita kwa maelekezo Hao wazee Wa udsm umewaleta kuzuga.
Kuna watu walikuwa na maswali ya oral kabila hawajaitwa na walikuwa wakitafuta majibu kabila hawajaitwa.
Kuna nini hapo . oneeeni vijana hiyana
 
Hili pia limejitokeza katika saili ya TANAPA sitaki kutaja jina la nafasi ndugu yangu alienda fanya usaili baada ya kumaliza mtihani kuna sehemu alienda kupata chakula katika jiji hilo hilo la arusha kwa bahati nzuri alikaa jirani wasimamizi na akawasikia akisema " Wamekuja kupitisha watu wao katika nafasi X" hili linaashiria ya kwamba kwenye taasisi, mashirika na mamlaka kubwa za serikali hizo nafasi hupewa watoto wa wakubwa wa nchi.

Hakuna kipindi ambacho rushwa imekithiri kama awamu hii ya Mh. Magufuli
 
Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
Usaili wa Tanroads ulikuwa na mtoto wa Mfugale,Ndugu wa Spika wakiwamo watoto wengine wa vigogo yaani kwa haraka haraka nimewafahamu watu 9 ndugu wa vigogo yaani taasisi kama Tanroads,Tanapa,BoT nk zenye ulaji mkubwa sio rafiki kwa watoto wa maskini
Mkuu taasisi nyingi kubwa huwa kuna ndugu wengi wa wakubwa wanazugishwa katika saili ila mwisho wa siku huwa wana maswali yote ya written na oral na mwisho wa siku ndio hupata nafasi.

Ajira nyingi za halimashauri hupewa watoto wa maskini.
 
Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
692
1,000
Mkuu kwanza hongera, umekuwa mfwatiliaji wa hadi deep kabisa. Ukweli sisi ambao hatuna ajira wanatuhadaa sana hawa watu. Inafika wakat hadi rafk zako au ndugu wanakuona ww ndo mbabaishaji kuwa kwanini wew huajiriwi wakat kila siku watu wanaajiriwa. Ukweli ni kwamba kati ya ajira 20 tegemea fake zipo 8, ni kama wameelekezwa kufanya hivo ili kumtukuza mkuu wa nchi anaye tekeleza miradi yenye gharama kubwa na kusahau kuna watu hususani masikini wanaumia sanaaa!
Inasikitisha sana, hizo kanzidata zinaficha mengi sana na nimekuja gundua kanzi data ndio " loop hole " ya kuchomeka watu katika taasisi mbalimbali
 
Simba zee 33

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
1,377
2,000
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Sasa hizo ajira zimwtolewa hata kama majina yamejirudia ni sawa tu tofauti na zamani kulikua na ajira feki nyingi sana
Hebu tu Kubali nchi imepata Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake Ndio maana maisha ya watakuwa sasa ni bam bam
 
amaizing

JF-Expert Member
May 3, 2013
3,589
2,000
Yaweza kuwa hivyo pia kuhusu majina ambayo watu huitwa kazini na amamini sasa kuna janja nyingi sana hufanyika (Idadi ya wanaoitwa makazini ni chache kulinganisha na majina yanayotolewa).
Wamenitumia email kuitwa kwa interview na number ya usahili Cha ajabu kwa list ya selected candidates namba hiyo hiyo iko na jina la mtu mwingine na langu halipo...
Hii ni tatizooo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom