Sijaona Mwanamke Anayenifaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijaona Mwanamke Anayenifaa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 25, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanaume mmoja wa nchini Marekani ambaye alikuwa akidai kuwa hataoa mwanamke mpaka pale atakapompata mwanamke mwenye sifa anazozitaka, alisubiria miaka zaidi ya 70 hadi juzi alipofanikiwa kumpata mwanamke mwenye sifa anazozitaka na hatimaye kufunga ndoa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 99.​
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]'Sitaoa mpaka nitakapompata mwanamke mwenye sifa ninazozitaka", alikuwa akisema Gilbert Herrick enzi za ujana wake.

  Gilbert hakujua kama ngoja ngoja yake ingeweza kumfanya afunge ndoa kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 99.

  Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, Gilbert amefanikiwa kufunga ndoa baada ya moyo wake kumzimikia mjane mwenye umri wa miaka 86, Virginia Hartman.

  "Sikuwahi kumpata mwanamke mwenye sifa ninazozitaka mpaka nilipokutana na Virginia", alisema babu Gilbert.

  Gilbert ambaye alikuwa mwanajeshi wa Marekani kwenye vita ya pili ya dunia alikula kiapo cha kumpenda na kumtunza mpaka kifo kitakapowatenganisha yeye na mkewe Virginia ambaye alikuwa ni mjane mwenye watoto watano, mjukuu mmoja na kitukuu mmoja.

  Ingawa Gilbert na mkewe wote wawili hawana tena uwezo wa kutembea wakitembea kwa kutumia baiskeli za vilema, hawakujivunga kuingia ukumbini kufungua dansi kwa muziki nyororo wakati wa sherehe ya harusi yao iliyofanyika jijini New York.

  Alipoulizwa sababu ya kuamua kuoa sasa baada ya kuishi miaka mingi bila kuoa, Gilbert alijibu kwa kifupi "Mapenzi ya kweli".
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
Loading...