MWALLA
JF-Expert Member
- Dec 12, 2006
- 16,952
- 10,500
MIMI nimeamua kuongeza macho mawili kwa sababu nimeshindwa kumuona vizuri mtukufu kutokana na harakati zake za kuitoa nchi kwenye tope zito la mdororo wa uchumi na umaskini wa nchi kwa ujumla wake.
Napata shida pale anaposimama kidete na kutangaza kupambana na maharamia wa uchumi wa nchi hii. Sijaona mpaka wa leo hii ni kipi amekishughulikia haswa kutokana na yale mauozo yaliyoachwa na mkulu aliepita nadhani yanajulikana vizuri tu. Tena kuna mengine mapya ambayo haya yameibukia kwenye kipindi chake hiki yeye mwenyewe. Mfano ishu ya Lugumi, DART nk.
Ukija kwenye yale ya nyuma RICHMOND, EPA, ESCROW, KIWIRA, RADA, nk ni mengi mno mpaka yachefua. Sasa atuambie tu ukweli hawezi kuyagusa hayo ama atabaki akiendelea kutumbua vijipu tu mpaka amalize kipindi chake.
Siwezi kumuona kweli kuwa anainyoosha nchi hii kama ataendelea kufumbia macho haya majanga makubwa yanayoitafuna nchi hii. Nilisahau pia ule mradi wa yule Mr. Ruge wa kutuuzia umeme IPTL eti kila siku anameza nasikia takriban bil 2 kama matumizi ya kila siku na hii kesi sijui imeishiaje maana hakuna mrejesho.
Mtukufu angejiingiza kwenye haya magonjwa makuu akaachana na vjipu uchwara ningeweza kujitahidi angalau nimuangalie kwa macho mawili tu badala ya kuongeza mawili ya ziada.
Tumshauri mtukufu abadili gia kama ni angani au bado tambarale basi ageuze aanze upya.
NITAMUELEWA..