Sijaona awamu ya uongozi wenye utata hapa Tanzania kama awamu ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijaona awamu ya uongozi wenye utata hapa Tanzania kama awamu ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 9, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Kila Waziri na kila mkurugenzi katika idara za serikali ya Kikwete anasema kitu chake kinachopingana na mwingine katika jambo hilo hilo.

  Maafa yaliyotokea Arusha hakuna kiongozi ye yote wa serikali aliyetembelea kwenda kuona hali halisi.
  Kikwete anafanya tafrija Ikulu wakati Arusha kuna maiti, majeruhi na mali kuharibika.
  Makamu wa Rais anajipumzisha na kuvinjari mbuga za wanyama wakati yupo pua na mdomo kutoka yaliyotokea mauaji-Arusha.

  Kikwete hajatamka lo lote kwa Wananchi wa Tanzania kuhusu yaliyotokea Arusha.
  Kikwete hatatamka lo lote kuhusu matatizo ya muda mrefu kuhusu Dowens.
  Waziri wa Fedha Mkulo anatoa tamko linalopingana na tamko la Waziri Nishati Ngeleja kuhusu kuilipa Dowens.
  Waziri wa Katiba na Sheria Kombani na Mwanasheria Mkuu wa serikali wanatoa kauli zinazopingana na Rais Kikwete juu ya hoja ya wananchi kuhusu Katiba mpya.

  Nini kinaendelea nchini Tanazania Wanajamii forum?
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Imeandikwa mara nyingi kwenye na Bwana Ngurumo (naamini) kuwa tuna OMBWE (vacuum) la uongozi.
  Kwa Wasomaji wa Biblia: "Siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli; kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe" Amuzi 17:6 [Judg 17:6 - In those days Israel had no king; everyone did as he saw fit].
  JK hana ubavu wa kuwakemea. Ni mambo ya kishikaji shikaji tu!
   
Loading...