Sijamwelewa wife jamani. .. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijamwelewa wife jamani. ..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Calnde, Oct 29, 2009.

 1. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni jioni, tumepumzika, na mpenzi wangu, mke wangu,katoto ketu ka miaka nane katundu kweli. Basi kanaleta utundu wake, nakafokea, kanazidi, nikakasirika na kukaambia 'we mbona mtudu hivyo, utadhani sio mwanangu?'

  duuh, nikawa nimeharibu, wacha mama yake awake, unadhani wa nani. huniamini ee? akaendeleza maneno kibao ya malalamiko, toka juzi amekasirika. Nimemwomba samahani, kakubali, lakini bado kakasirika kwa msemo wangu.

  wadau napata mashaka,simwelewi, mbona kakasirika?
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Kwani hujui siku zote mtoto ni wa mama!!!?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hahahahaha duh ukiona n'tu anajihami basi ujue kuna kitu around basi wewe chunguza n'jomba utabaini ukweli kachukue kapime DNA utabaini pengine kweli sio wako.
   
 4. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  pls don tel me that,
  miaka nane yote hiyo unataka kuniambia nini
  God forbid jamani
   
 5. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  mkuu, DNA itabidi nipime kwa siri au maana kama nimesema vile akawaka DNA si itakuwa balaa? Lazima atanitimua home mkuu
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  usiende kufanya DNA inakuwa kama humuamini mkeo???
  Itakuwa alikumind kidogo tu ulivomgombeza mtoto lakini si vingine
   
 7. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kitanda hakizai haramu ndugu...mkiambiwa wanawake nao wamo, mara ooh ni watu wa staha ona sasa. Kaza moyo kwenda kapime DNA...ndipo utakapopata jibu na roho yako kutulia. Ila uifanye kisirisiri sana. Na ukigundua wewe endelea naye tuu na usimwambie kitu.
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Ushawahi kuingia delivery room/leba ukajionea watoto wanavyokuja duniani? Kama umewahi basi nitakushangaa lakini kama hujawahi hebu jaribu kuingia mtakapo-plan kuleta mtoto mwingine,then utapata majibu ya maswali yako yoooote.
   
 9. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  ndo kwanza mtoto wa kwanza, sijawahi, ila ukinisaidia ntashukuru mkuu
   
 10. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  mkuu kweli nukigundua nieendelee, hapo sitaweza, atakufa mtu ati! Fikiria mtoto yupo darasa la pili, namlipia pesa nyingi mpaka nachanganyikiwa, alafu nieendelee nae! itakuwa kazi nzito. . .
  Mungu saidia tuu awe wangu
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Oct 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pole sana calnde nadhani wifi ameghafilika kidogo tu but inategemea na mtu inawezekana kabisa hakuna kitu bali ni reaction yake tu over vitu vinavyomuudhi.
   
 12. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Sui kila siku majibu ya DNA yatakufanya utulie, ukiwa na kimavi yaweza kuwa ni mwanzo wa mwisho wako wewe na my wife wako!! Watch out
   
 13. 4X4byfar

  4X4byfar JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole mkulu, ni vijimambo tuu vya maisha hivyo. Utakuwa hujatenda haki kabisa. Maana ingekuwa ni wewe umezaa nje ya ndoa ungemleta mtoto ndani na mama angemlea. Je, kunatofauti gani hapo kama sio ubinafsi. Acheni hizo wanaume nyinyi.
   
 14. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  mwanajamii we ni mwanamama inaelekea,
  Nisaidie, anawezekana kweli wife akamind kivile kama hakuna lolote? Halafu always ni mkimya asiyependa makuu wala mabishani au majibizano, hajawahi kukasirika kiasi hicho toka tumeoana miaka zaidi ya nane sasa, ndo maana nikashtuka kwa nini amereact that much. . . .
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Yeah kweli mkuu nenda kwa siri siri yeye asijue lakini unaweza beba mate tu ya mtoto na kuyapeleka kwa wataalamu wakachunguza na kubaini.
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hapana ndugu,
  Mie nje simegi kabisa. Hata kama umefatilia thread zangu hapa nalaani kabisa hiyo mambo, iweje leo yeye afanye hivyo. . . .
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Hebu niambieni wanapimia wapi na vitu gani vinahitajika ili nipate najibu mazuri, ila akijua atantimua home aisee! Mungu wangu . . . .
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Hehehe mkuu mahospital makubwa haya duhh mzee kwa hiyo unakaa kwake kama unakaa kwake basi inabidi utii amri mkuu............
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Oct 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Calnde kama unamfahamu vema mkeo basi unayo haki ya kumtilia mashaka kwa reaction yake; mimi wangu alikuwaga na tabia ya kumsema mtoto mara oh hii pua mbona kama si yangu; oh mbona sura kama Mahita yaani ilimradi tu lazima amseme. Mimi nilikuwa naona ni utani tu but kuna siku alifululiza tangu asubuhi akitoa accusations zake nikampa jibu moja tu aende akacheck DNA. Sasa sijui kama alicheck kisiri au la sikumsikiaga tena.

  Sasa wewe kama ni mara yako ya kwanza kujoki hivyo na mama amereact hivyo pengine ni kwa vile hajawahi kukusikia ukisema hivyo ndo mana kachukia lakini pia pengine kuna jambo?

  Ushauri: Anza kuchunguza sura, maungo na vinasaba onyeshi kuona kama anaresemble na wewe! Ukishaona japo kimoja (hata kama ni rangi ya nywele) unafanana naye ridhika funga file ila na kama hutakiona basi amini mnafanana utumbo au kisogo so songa mbele mambo ya DNA yatakuchanganya bure kaka yangu achana nayo!
   
 20. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  mkuu wakati tunaoana ye alikuwa amemaliza Masters na alikuwa amekusanya senti na kujenga bonge la hausi Njiro Arusha.. . .
  Mie nilikuwa na nyumba maeneo ya kijitonyama lakini haikuwa kubwa kama yake. Tukakubaliana kuiuza ili tununue usafiri pamoja na miradi flani ya maendeleo. Mie kwa sasa sina nyumba, ila nilinunua kiwanja Moshono Arusha pamoja na Kingine Kidogo maeneo ya Wazo. .

  Tunaishi kwenye nyumba ya wife, japo hajawahi kuninyanyasa wala kuringa. Ananipenda, tunapendana, tunaaminiana, ila hili la juzi limebadilisha kabisa mtizamo wangu kwake!
   
Loading...