Sijamuona mbunge wangu tangu bunge la bajeti lilipoisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sijamuona mbunge wangu tangu bunge la bajeti lilipoisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wakurogwa, Sep 16, 2012.

  1. W

    Wakurogwa JF-Expert Member

    #1
    Sep 16, 2012
    Joined: Sep 2, 2011
    Messages: 216
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    Kila wakati najiuliza hivi hawa wabunge kwanini hawakai kwenye majimbo yao? Wanakuwa wapi?Siku za nyuma hadi nilipofikia hatua ya kubadili mtazamo kwamba ngoja kura yangu niipeleke upinzani huenda kutakuwa na afueni lakini bado mbunge wangu simuoni Jimboni.Mimi nipo Jimbo la Mpanda Mjini.Huyu mbunge haonekani yupo wapi?au amebanwa na shughuli za kichama au kamati?Nyie wabunge kumbukeni majimbo yenu acheni tabia ya kuwategemea makatibu wenu na kuongoza majimbo kwa Simu za mkononi.Rudini kutekeleza ahadi zenu bana.Hii ni kwa wabunge wote hawataki kabisa kuonekana majimboni.
     
  2. Baba V

    Baba V JF-Expert Member

    #2
    Sep 16, 2012
    Joined: Dec 29, 2010
    Messages: 19,490
    Likes Received: 133
    Trophy Points: 160
    Umerogwa
     
  3. r

    raymg JF-Expert Member

    #3
    Sep 16, 2012
    Joined: Jun 30, 2012
    Messages: 845
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    Hivi PM anatoka wapi....
     
  4. King Kong III

    King Kong III JF-Expert Member

    #4
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 15, 2010
    Messages: 24,925
    Likes Received: 1,982
    Trophy Points: 280
    Usihofu mbunge wako yupo town atakuja kipindi cha uchaguzi.
     
  5. Marire

    Marire JF-Expert Member

    #5
    Sep 16, 2012
    Joined: May 1, 2012
    Messages: 11,390
    Likes Received: 199
    Trophy Points: 160
    Ondoa mawazo yako sisiem haitarudia kututawala hiki ndio kipindi chenu cha mwisho na ibeni na mkae mkijua jela inawangoja na hakuna pahala mtajificha dunia hii!
     
  6. Kimbunga

    Kimbunga Platinum Member

    #6
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 4, 2007
    Messages: 12,750
    Likes Received: 1,516
    Trophy Points: 280
    Mkuu Wakurogwa nadhani watanzania tumerogwa. Nilidhani ukichagua mbunge ambaye hafanyi kazi Dar basi mtaishi naye huko huko kumbe siyo. Mtu akishakuwa mbunge basi ndio amepata tiketi ya kuhamishia makazi yake Dar na kuwasahau wapiga kura wake. Jana nimesoma gazeti moja nikakuta habari diwani Chagulani (aliyeenguliwa) akimtuhumu Mbunge Wenje kwamba amelitelekeza jimbo na kuhamia Dar. Nikashangaa. Kwa nini wote wanahamia Dar?
     
    Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
  7. Autorun

    Autorun JF-Expert Member

    #7
    Sep 16, 2012
    Joined: Mar 21, 2008
    Messages: 555
    Likes Received: 17
    Trophy Points: 35
    Usiwe nahofu mbunge wako mzima wa afya na tupo nae hapa town na 2nashirikinae vizuri kula bata za town na totoz wazuri
     
  8. Nzenzu

    Nzenzu JF-Expert Member

    #8
    Sep 16, 2012
    Joined: Aug 10, 2011
    Messages: 859
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Jana kaonekana SAMAKI SAMAKI pale Mlimani City anaponda raha1!
     
  9. WAHEED SUDAY

    WAHEED SUDAY JF-Expert Member

    #9
    Sep 16, 2012
    Joined: Jun 24, 2011
    Messages: 6,754
    Likes Received: 957
    Trophy Points: 280
    Tulia yupo dar mlimani city anafanya shopping atakuja tu
     
  10. Ulukolokwitanga

    Ulukolokwitanga JF-Expert Member

    #10
    Sep 16, 2012
    Joined: Sep 18, 2010
    Messages: 8,208
    Likes Received: 3,188
    Trophy Points: 280
    Chagulani na Wenje wana uhasama usijiingize huko Bw Kimbunga. Wenje juzi kati hapa aliitisha mkutano usiokuwa na kibali siku Mwangosi anauwawa. Pia ikumbukwe kuwa mbunge akirudi jimboni hatembelei wapiga kura nyumba hadi nyumba, lazima mpiga kura kama una mahitaji ufanye juhudi za kumtafuta kupitia kwa katibu wake.

    Miaka ya nyuma nilikuwa nafanya survey iliyojumuisha kuwauliza wakulima kama wamewahi kutembelewa na bwana shamba, 86% wakasema hawajawahi. Katika swali lililofuata kuhusu kumualika bwana shamba 98% ya wakulima wakasema hawajawahi.
     
  11. Wingu

    Wingu JF-Expert Member

    #11
    Sep 16, 2012
    Joined: Jan 14, 2011
    Messages: 4,326
    Likes Received: 14
    Trophy Points: 135
    Mkuu hujui msemo Unaosema chumia juani lia kivulini.Mjini kivulini Babu
     
  12. Kimbunga

    Kimbunga Platinum Member

    #12
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 4, 2007
    Messages: 12,750
    Likes Received: 1,516
    Trophy Points: 280
    Bwana shamba ni kazi yake kuwatembelea wakulima na kutoa ushauri na si lazima aalikwe. Mbunge haendi kwa mtu mmoja mmoja lakini ni busara kwamba kabla ya kwenda kwenye kikao cha bunge uwatembelee wapiga kura wako na kupata maoni yao na kero zao. Pia ni busara ukitoka Bungeni ukawapa watu wako mlishonyuma wa nini kiliongelewa bungeni hasa kuhusu jimbo lao. Haya yanafanyika kupitia mikutano.

    La Wenje ni mfano tu nimetoa na wala sitaki wala sitegemei kuingia kwenye mgogoro wao.
     
  13. Kimbunga

    Kimbunga Platinum Member

    #13
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 4, 2007
    Messages: 12,750
    Likes Received: 1,516
    Trophy Points: 280
    Mjini wapo ili kupiga deal tu! Wengi siku hizi nawaona pale Haidery Plaza wana viofisi vyao vya deal!
     
  14. Ukwaju

    Ukwaju JF Bronze Member

    #14
    Sep 16, 2012
    Joined: Oct 19, 2010
    Messages: 7,923
    Likes Received: 500
    Trophy Points: 280
    Naona umeshapata jb sio lazima Mbunge ukae nae kila siku kwani kuna Katibu na Fungu mmeshatengewa,
    Tatizo kila mpiga kura ni njaa anahadithia alivyoweza kuiba kura na kumuongezea mbunge mpaka akashinde, hebu fanyeni kazi nyingine na wao wapumue kwani sio kazi zao kusikiliza matatizo Binafsi ya kila mtu anzieni kwa Balozi - M/Kiti - Diwani na yeye atapeleka Bungeni Serikali ikimkubalia ndio mtaona majibu la sivyo msimlaumu hana kitu jamani.
     
  15. Marire

    Marire JF-Expert Member

    #15
    Sep 16, 2012
    Joined: May 1, 2012
    Messages: 11,390
    Likes Received: 199
    Trophy Points: 160
    Na wabunge wa dar wanakimbilia dubai? Niliona mada hapa jamvini mbunge ABASI MTEMVU wa ccm haonekani jimboni hii mambo imekaaje mazee
     
  16. Marire

    Marire JF-Expert Member

    #16
    Sep 16, 2012
    Joined: May 1, 2012
    Messages: 11,390
    Likes Received: 199
    Trophy Points: 160
    Huyu WENJE mikutano yake hufanya na wamachinga tu palee sahara ni mbunge wangu ni lazma tuseme,na haines ndio kabsaa wameshaiga stail za magamba wanavizia uchaguzi ndio utawaona
     
  17. W

    Wakurogwa JF-Expert Member

    #17
    Sep 21, 2012
    Joined: Sep 2, 2011
    Messages: 216
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    We ulishaona mbunge anapofanya kampeni anatangaza mgombea mwenza?matatizo ya jimbo ni muhimu apewe mbunge mwenyewe na siyo kuongoza jimbo kwa bluetooth au inferred. wacha kutetea ugonjwa wa wabunge walio wengi.
     
Loading...