Sijaelewa utaratibu wa kukaguliwa vitambulisho Uvinza

Lupamba's grandson

JF-Expert Member
Jan 9, 2015
1,232
1,192
Habarini wapendwa,

Niko njiani kuelekea Kigoma kwa kina Brother K ila huu utaratibu wa kugagua vitambulisho hapa Uvinza naona kama hawa jamaa hawako serious.

Wamekuja jamaa wawili wakaomba vitambulisho wenzangu wakatoa, wengine wakasema sijui wamesahau, wengine sijui nini, kila mtu na sababu yake, alipofika kwangu jamaa akaniangalia alafu akaniuliza kwema? Nikamwambia kwema alafu akapita hakunidai.

Sasa sijajua ametumia kigezo gani kunipita mimi? Au the way naonekana, nilivyo shave au nimekaa kama wazee wa suti nyeusi na repel kwenye sikio? Au amejihakikishiaje mimi si mkimbizi labda au?

By the way sina vitambulisho vyote nilipoteza wallet ila niko na lost repot ya kadi za bank na driving lisence na sikutoa chochote.

Swali lipo hapa, hawa jamaa wapo serious na kazi yao? Au wanafanya kwa mazoea? Maana najiuliza kwanini wamemuuliza mwenzangu mimi wanisalimie tu wasiniulize?

Wajuvi wa mambo embu nielewesheni hili.
 
Habarini wapendwa, Niko njiani kuelekea Kigoma kwa Kina BROTHE K ila huu utaratibu wa kugagua vitambulisho hapa uvinza naona kama hawa jamaa hawako serious eeh, Wamekuja jamaa wawili wakaomba vitambulisho wenzangu wakatoa ,wengine wakasema sijui wamesahau ,wengine sijui nini ,kila mtu na sababu yake ,alipofika kwangu jamaa akaniangalia af akaniuliza kwema? Nikamwambia kwema alafu akapita hakunidai, sasa sijajua ametumia kigezo gani kunipita mimi,? Au the way naonekana ,nilivyo shave au nimekaa kama wazee wa suti nyeusi na repel kwenye sikio? Au amejihakikishiaje mimi si mkimbizi labda au?? Wajuvi wa mambo embu nielewesheni hili.
By the way sina vitambulisho vyote nilipoteza wallet ila niko na lost repot ya kadi za bank na driving lisence ,na sikutoa chochote.
Swali lipo hapa ,hawa jamaa wapo serious na kazi yao? Au wanafanya kwa mazoea? Maana najiuliza kwanini wamemuuliza mwenzangu mimi wanisalimie tu wasiniulize??
Huwa wana salamu zao na wanajua mtanzania anajibuje. Ile kujibu fasaha na muonekano wako tu vinatosha wasikutilie mashaka hata Kama huna kitambulisho. Imenitokea Mara nyingi tu.
 
Kuna msemo wasema "wapemba hujuana kwa viremba"
Immigration wanadeal na psychology ya mtu. Nakumbuka kuna Congolese walidakwa walikua wanatokea simbawanga-kigoma the way wametamka neno police.
 
Hayo ndio maisha yanayotakiwa Raia hatakiwi asumbuliwe ukisafiri kuna baadhi ya Nchi raia anagonga pass foleni tofauti na mgeni...Nchi nyingi raia anasalimiwa tuu mambo ya vitambulisho baadae kama wana mashaka nae...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom