Uchaguzi 2020 Sijaelewa lengo la CCM kumhudhurisha mama Maria Nyerere kwenye mkutano wao

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,346
1,303
Juzi CCM walioonekana kukaa meza moja na familia ya Baba wa Taifa, Mama Maria pamoja watoto wake Makongoro na Madaraka. Dhumuni bado sijaelewa, ila tu kwa sababu ya kampeni nilijua ni kupata huruma ya familia hii. Katika kipindi hiki vihoja na vingi na bila kutokuwa makini unaweza ukafanya mengi mno ya hovyo na mengine ya msingi.

Haijapita hata muda wajumbe wa hiyo hiyo CCM iliwakataa watia nia toka familia hiyo kwa kuwapa jumla ya kura saba tu. Kwa namna nyingine wajumbe wa CCM hawawataki hiyo familia kuwa miongoni mwa wanaongoza katika serikali iwe kwa kura au kwa kuteuliwa. Kwa kuongezea ushahidi, Makongoro alipogombea ubunge wa Afrika Mashariki aliangukia pua licha ya kudumu kipindi cha nyuma alipochaguliwa kwa kuwa ndugu yake Vincent Kiboko alikuwepo bungeni hivyo alishawishi upande mwingine uwapitishe.

Kwa kuhitimisha, ni kwa nini mwenyekiti asingeweza kupindua meza na kuwateua kuwa wagombea kama alivyofanya kwa kina Silinde, Katambi, Gwajima na wengine? Hivi mlimsikia vizuri Mama Maria? Usemi wake ni kuwa walimlazimisha kuongea na hata kuja pale ni kuongeza tu idadi.

Jamani, naomba kama ni kumuenzi Nyerere naye mtendeeni haki kama kina Karume na Mwinyi. Familia hii ibaki kuwa Royal kwa kuheshimiwa na si kutumika katika kampeni tu. Lala pema Baba wa taifa.

CCM mnamchafua Baba wa Taifa
 
Sisi sote tunapita
Hakuna mtu mwenye Mji udumuo hapa duniani
Jiangalie sana jinsi upitavyo

Maendeleo yanae Vyama
 
Sioni sababu ya kumsumbua Mama Maria, wafanye kampeni wenyewe.
 
onjwayo,
Wangekuwa watu wa kabila moja na Meko wangeweza kuteuliwa ila tatizo Nyerere alikuwa mzanaki. Na sasa hivi chama kinaendeshwa kikabila.
 
Japokuwa mwalimu Nyerere alitukanwa na kupakwa matope na Lissu lakini bado CCM inathamini mchango wa mwl.Nyerere kupitia mjane wake.
 
Mama NYERERE Ni mwana ccm na kadi yake ni kati ya kadi 10 za mwanzo unasemaje amehudhurishwa, 2015 kada namba moja wa chadema Mzee mtei alihudhuria kampeni, sema mwaka huu mzee wa watu kaingia mitini kwa sababu Mbowe kachanganya mawe ya tochi na gunzi tochi haiwaki mzee kapotezea
 
CCM shenzi sana, bila aibu wamehariri maneno yake!
Adjustments.jpg
 
Mama apumzike, Katika hili event planners waliteleza ila Cha muhimu ni kuwa JPM ameshamueleza Mama na wana mara kuwa watapandia ndege ndege hapo hapo sio mpaka waje mwanza au waende Serengeti.
 
Juzi CCM walioonekana kukaa meza moja na familia ya Baba wa Taifa, Mama Maria pamoja watoto wake Makongoro na Madaraka. Dhumuni bado sijaelewa, ila tu kwa sababu ya kampeni nilijua ni kupata huruma ya familia hii. Katika kipindi hiki vihoja na vingi na bila kutokuwa makini unaweza ukafanya mengi mno ya hovyo na mengine ya msingi.

Haijapita hata muda wajumbe wa hiyo hiyo CCM iliwakataa watia nia toka familia hiyo kwa kuwapa jumla ya kura saba tu. Kwa namna nyingine wajumbe wa CCM hawawataki hiyo familia kuwa miongoni mwa wanaongoza katika serikali iwe kwa kura au kwa kuteuliwa. Kwa kuongezea ushahidi, Makongoro alipogombea ubunge wa Afrika Mashariki aliangukia pua licha ya kudumu kipindi cha nyuma alipochaguliwa kwa kuwa ndugu yake Vincent Kiboko alikuwepo bungeni hivyo alishawishi upande mwingine uwapitishe.

Kwa kuhitimisha, ni kwa nini mwenyekiti asingeweza kupindua meza na kuwateua kuwa wagombea kama alivyofanya kwa kina Silinde, Katambi, Gwajima na wengine? Hivi mlimsikia vizuri Mama Maria? Usemi wake ni kuwa walimlazimisha kuongea na hata kuja pale ni kuongeza tu idadi.

Jamani, naomba kama ni kumuenzi Nyerere naye mtendeeni haki kama kina Karume na Mwinyi. Familia hii ibaki kuwa Royal kwa kuheshimiwa na si kutumika katika kampeni tu. Lala pema Baba wa taifa.

CCM mnamchafua Baba wa Taifa
Ilikuwa aibu ya ajabu kwa ccm!
 
Wewe nawe. Mambo ya juzi huko unatuletea Leo? Hebu kuwa current basi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom