Sijaelewa kwanini Spika anaandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM badala ya Katibu wa Bunge!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,772
Nilifikiri barua ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai angeandikiwa Katibu wa bunge na nakala kupelekwa kwa Katibu mkuu wa CCM na siyo kinyume chake

Pascal Mayalla nipe uzoefu wako Tafadhali

1643004521632.png
 
Aliyempa Ajira ni Chama cha Mapinduzi, angekuwa mgombea binafsi angemuandikia barua Katibu wa Bunge pekee la sivyo angenyang'anywa Kadi ya Chama akakosa na Ubunge.

acheni amuandikie Boss wake Katibu wa Chama maana yake ni kwa Mwenyekiti wa CCM

George Kahangwa kahojiwa na DW bado anakataa barua isiandikwe kwa Katibu wa Chama

eti hata wakienda Mahakamani watashindwa Kapotea huyu Kahangwa

CCM imeshika Dola kwa kuwa na wabunge wengi hivyo huyo Mama Katibu kateuliwa juzi kwani haogopi rungu kwani anamjua Spika wake na aliyemteua nani mkubwa
 
Dalili za kuchanganyikiwa hizo. Laana ya Lisu inamtafuna. Kwako VUTA-NKUVUTE lete maneno....

Achaga upumbavu Basi. Who is Lissu. Kuna watu wameuliwa duniani. Baba. Mama . Watoto. Na bado miaka wauaji hawajapatikana, itakuwa huyo ambaye dereva kauzwa. Omba ndoa kabisa naye uwe unamweka ndani mwako. Huwezi kuchukua mada kama ilivyo na kujibu bila kupachika ujinga.
 
Aliyempa Ajira ni Chama cha Mapinduzi, angekuwa mgombea binafsi angemuandikia barua Katibu wa Bunge pekee
La sivyo angenyang'anywa Kadi ya Chama akakosa na Ubunge...
Utaratibu wa kuandika barua unajulikana.

Ndio maana barua ya Chadema kuteua wale covid 19 ililetwa bungeni na Dr Mahela wa NEC siyo J J Mnyika.
 
Achaga upumbavu Basi. Who is Lissu. Kuna watu wameuliwa duniani. Baba. Mama . Watoto. Na bado miaka wauaji hawajapatikana, itakuwa huyo ambaye dereva kauzwa. Omba ndoa kabisa naye uwe unamweka ndani mwako. Huwezi kuchukua mada kama ilivyo na kujibu bila kupachika ujinga.
Panic tu hii. Sasa na wewe kama unaona wivu Lisu kupigwa risasi 16 na wewe kapigwe risasi 200 halafu tulia ndani kwako hatutakuuliza.

Eti who is Lisu.....BTW who is you? Idiot?
 
Nilifikiri barua ya kujiuzulu kwa Spika Ndugai angeandikiwa Katibu wa bunge na nakala kupelekwa kwa Katibu mkuu wa CCM na siyo kinyume chake

Pascal Mayalla nipe uzoefu wako Tafadhali
Ili labda Chama chake kiamue kama anayo makosa kimuite na kumuhoji na kama ikibainika kimfutie uanachama na baadae bunge kujulishwa rasmi na Chama chake.
 
Ukiona speaker wa Bunge ambae ni mhimili wa dola unaojitegemea na ambao unapaswa kuwa huru ametoa msimamo wake juu ya jambo fulani halafu ghafla akamuomba msamaha Rais kwa msimamo aliotoa na kubidi ajiuzulu huku wananchi wanakenua meno, jua hilo Taifa limefika mwisho na limekufa.

Ni kweli Ndugai alipaswa kuondoka kwa maovu ambayo ameifanyia nchi hii lakini kumuondoa Ndugai badala ya kuondoa mfumo haitaleta Bunge huru.Atakaekuja uzi utakuwa kama uleule wa Ndugai kwa sababu tatizo halikuwa Ndugai bali ni mfumo.

Sisi kama wananchi tulipaswa kulinda mihimili kuhakikisha kuwa inakuwa huru pamoja na kuhakikisha kuwa tunakuwa na mfumo unaolinda mihimili badala ya kuhangaika na mtu(Ndugai).

Ujinga uliofanyika wa Ndugai kujiuzulu kwa sababu tu alitoa maoni yake kama mhimili huru itampa Rais kiburi zaidi cha kuendelea kunyanyasa mhimili wa Bunge pamoja na mihimili mingine.
 
Back
Top Bottom